Papa amelala salama usiku na yupo anapumzika
Vatican News
“Papa alilala usiku kucha kwa utulivu na yupo anapumzika.” Ndivyo maelezo ya asubuhi hii Jumatano saa 2.06 saa za Ulaya na saa 4.06 Masaa ya Afrika Mashariki na kati tarehe 26 Februari 2025 yaliyotolewa katika Ukumbi wa Vyombo vya habari vya Vatican katika taarifa kwa waandishi wa habari.
Hata hivyo Jumanne jioni tarehe 25, Februari 2025 taarifa ya Ofisi ya Vyombo vya habari vya Vatican ilisasisha kuhusu afya ya Baba Mtakatifu Francisko aliyelezwa tangu tarehe 14 Februari 2025 katika Hospitali ya Gemelli, Roma ikibainisha kuwa "hajapata matatizo ya kupumua, na vigezo vyake vya damu bado ni thabiti. Utabiri unabaki kulindwa.
Jioni hii Papa alifanyiwa uchunguzi wa X-ray uliopangwa kwa ajili ya ufuatiliaji wa picha ya ugonjwa wa mkamba wa sehemu mbili na Utabiri unabaki kuhifadhiwa. Asubuhi ya Jumanne Februari 25, mara baada ya kupokea Ekaristi, aliendelea na shughuli zake za kazi."