Kwaresima,Kard.De Donatis ataongoza Liturujia ya Majivu huko Aventino,Roma
Vatican News
Siku ya Jumatano tarehe 5 Machi 2025, itakuwa ni siku ya kuanza kipindi cha Kanisa cha Kwaresima kwa mwaka 2025, kwa kupakwa majivu, kuashiria mwanzo wa wakati wa maandalizi ya Pasaka, ambapo saa 10.30 jioni masaa ya Ulaya na saa 12.30 jioni masaa ya Afrika Mashariki na Kati, Kardinali Angelo De Donatis, Mhudumu mkuu wa Toba ya Kitume na Mwakilishi wa Papa Francisko, kutokana na kulazwa kwake katika Hospitali ya Gemelli, ataongoza liturujia hiyo katika Kanisa la Mtakatifu Anselmi huko Aventino, ambayo itafuatiwa na maandamano ya toba kuelekea katika Basilika ya Mtakatifu Sabina, Roma
Hiyo ni taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Maadhimisho ya Liturujia za Kipapa, Ijumaa tarehe 28 Februari 2025. Maandamano hayo yatahudhuriwa na makadinali, maaskofu wakuu, maaskofu, watawa Wabenediktini wa Mtakatifu Anselmi, Mapadre wadominikani wa Mtakatifu Sabina na baadhi ya waamini. Mwishoni mwa maandamano, hayo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Sabina, sherehe ya Ekaristi itafanyika kwa ibada ya kubariki na kupakwa majivu.