杏MAP导航

Tafuta

Tuwaombee marehemu wote nchini Sweden walioshambuliwa kwa risasi. Tuwaombee marehemu wote nchini Sweden walioshambuliwa kwa risasi. 

Huzuni wa Papa kuhusu shambulio dhidi ya shule moja nchini Sweden

Katika telegramu iliyotiwa saini na Kardinali Parolin,iliyoelekezwa kwa Waziri Mkuu wa Sweden Kristersson,Papa Francisko anatoa rambirambi zake kwa waathrika wa shambulio kutoka kwa kijana wa miaka 35 katika shule ya watu wazima huko ?rebro akiombea roho za marehemu na anatumaini wapone kwa haraka waliojeruhiwa.

Vatican News

Baba Mtakatifu Francisko  amehuzunishwa sana na shambulio la silaha lililotokea katika shule ya watu wazima katika mji wa  Örebro, Magharibi mwa mji  Mkuu  Stockholm, nchini Sweden, siku ya Jumanne tarehe 4 Februari 2025 na kusababisha vifo vya watu 11 na majeruhi kadhaa. Katika telegram iliyotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akiielekeza kwa Waziri Mkuu wa Sweden, Ulf Kristersson, Papa Francisko alielezea uhakika wa "ukaribu wake wa kiroho kwa wale wote ambao wameathiriwa na tukio hili la kiwehu," na  ambalo lilifafanuliwa  kuwa "shambulio baya zaidi" katika historia ya nchi hiyo, kwa mujibu wa Waziri mkuu katika mkutano na waandishi wa habari saa chache baada ya tukio hilo.

Kwa njia hiyo Papa Francisko  anatoa sala zake “kwa ajili ya kupumzika  roho za marehemu wote na kwa ajili ya faraja ya wanafamilia na marafiki walio na huzuni na kwa ajili ya kupona haraka majeruhi.” Katika wakati huu mgumu kwa taifa, Baba Mtakatifu  “anawaombea watu wa Sweden  zawadi za umoja na amani kutoka kwa Mwenyezi Mungu."

Shambulio hilo

Shambulio hilo lilitokea tarehe 4 Februari 2025 mchana, ambapo kijana mwenye umri wa miaka 35 alifyatua risasi katika chuo kilicho na vituo vya elimu ya watu wazima, na kusababisha vifo vya watu 11 na wengine 15 kujeruhiwa, mhusika pia alifariki katika shambulio hilo, ambalo bado halijajulikana nia yake lakini mamlaka kwa sasa inafutilia mbali sababu za kiitikadi.

05 Februari 2025, 16:52