Hali ya afya ya Papa Hospitalini Gemelli imeendelea kuimarika
Vatican News
Hali ya kiafya ya Baba Mtakatifu imethibitishwa kuimarika tena leo.
Alibadilisha matibabu ya oksijeni ya mtiririko wa juu kwa Ventimask. Kutokana na ugumu wa picha ya kliniki, siku zaidi za utulivu zinahitajika ili kufafanua wazi utabiri huo.
Asubuhi, Baba Mtakatifu alifanyiwa mazoezi ya kupumua, akibadilishana na kupumzika. Alasiri, baada ya mazoezi ya ziada, alitumia muda wake katika maombi kwenye kikanisa cha nyumba yake ya kibinafsi kwenye ghorofa ya 10, ambapo alipokea Ekaristi. Kisha akajishughulisha na shughuli za kazi ndogo ndogo.
Hii ndiyo taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Habari ya Vatican Alhamisi jioni tarehe 27 Februari 2025 ambayo ilifika wakati Papa anaendelea kutibiwa ugonjwa wa nimonia ya pande mbili, katika Hospitali ya Gemelli ya Roma. Ikumbukwe alilazwa tangu siku ya Ijumaa, tarehe 14 Februari 2025 kufuatia na ugonjwa wa Mkamba(bronchitis.)
Hata hivyo katika Taarifa kwa waandishi wa habari siku ya Alhamisi asubuhi, tarehe 27 Februari, ilibainisha kuwa Papa alikuwa amelala vizuri na akatoka kitandani na kuendelea na matibabu kwenye kiti chake cha sofa. Na kwamba anabaki katika roho nzuri ya utulivu.
katika taarifa nyingine Alhamisi tarehe 27 Februari 2025 pia Ofisi ya Wanahabari, Vatican ilibainisha kuwa Katekesi ya Jubilei iliyotarajiwa kufanyika Jumamosi, tarehe Mosi Machi 2025, imefutwa kutokana na Papa kuendelea kuwa hospitalini.