杏MAP导航

Tafuta

Watu wakikimbia ghasia nchini Congo. Watu wakikimbia ghasia nchini Congo.  (AFP or licensors)

Ukaribu wa Papa kwa watu wa Jamhuri ya Congo:rejesheni amani na usalama haraka iwezekanavyo

“Ninaelezea wasiwasi wangu kuhusu hali mbaya ya usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Ninatoa wito kwa pande zote katika mzozo huo kujitolea kukomesha uhasama na ulinzi wa raia wa Goma na maeneo yaliyoathiriwa na operesheni za kijeshi.Ni wito wa Papa mara baada ya katekesi tarehe 29 Januari 2025.Papa alikumbusha nchi za vita na kusema:“Na tusisahau kuombea amani:Palestina,Israel,Myanmar na nchi nyingi zinazopigana. Vita daima ni kushindwa."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya katekesi yake, Baba Mtakatifu Francisko akiwageukia waamini na mahujaji waliofika katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, Jumatano tarehe 29 Januari 2025 pamoja na salamu zake alionesha ukaribu kwa mataifa yale yanayojaribiwa na vurugu na vita. Papa alisema “Ninaelezea wasiwasi wangu kuhusu hali mbaya ya usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ninatoa wito kwa pande zote katika mzozo huo kujitolea kukomesha uhasama na ulinzi wa raia wa Goma na maeneo mengine yaliyoathiriwa na operesheni za kijeshi. Pia ninafuatilia kwa wasiwasi kile kinachotokea katika mji mkuu Kinshasa, nikitumaini kwamba aina zote za unyanyasaji dhidi ya watu na mali zao zitakoma haraka iwezekanavyo. Wakati ninaomba kwa ajili ya kurejeshwa kwa haraka kwa amani na usalama, ninatoa wito kwa mamlaka za umma na Jumuiya ya kimataifa kufanya kila jitihada kutatua hali ya migogoro kwa njia za amani.”

Salamu kwa mahujaji

Papa Francisko aidha liendelea kutoa salamu kwamba “Ninawakaribisha kwa moyo mkunjufu mahujaji wanaozungumza Kiitaliano. Hasa, ninawasalimu parokia ya Mtakatifu Malaika Mkuu Mkaeli wa  huko Manfredonia - (makofi) watu hawa wanapiga kelele nyingi… -, ambayo ninawahimiza kushuhudia Injili kwa furaha katika maisha yao ya kila siku. Kisha Papa alitoa salamu kwa  “Chama cha Mashujaa wa Kiitaliano wa Shirika la Kijeshi la Malta na Kijiji cha Elimu cha Polizzi Generosa.

Msisahau 'vita ni kushindwa'

Papa kama kawaida akikumbuka vita alisema: “Na tusisahau kuombea amani: Palestina, Israel, Myanmar na nchi nyingi zinazopigana. Vita daima ni kushindwa! Tuombe amani.”

Sikukuu ya Mtakatifu Yohane Bosco

Hatimaye, mawazo yake yaliwaendea vijana, wagonjwa, wazee na wenye ndoa wapya. Papa Francisko amekumbuka kumbukumbu ya kiliturujia ya Mtakatifu Yohane Bosco,(tarehe 30 Januari) kuhani na mwalimu. Papa amesema kuwa “Mtazame yeye kama mwalimu wa maisha na mjifunze kutokana na uzoefu wake wa kiroho kumtumaini Mungu, Baba mwenye huruma, katika kila hali. Na ametoa baraka zake kwa wote.

Baada ya Katekesi
29 Januari 2025, 11:09