杏MAP导航

Tafuta

2024.01.24 "GMCS -  Giornata mondiale delle comunicazioni sociali"

Ujumbe wa Papa kwa Siku ya 59 ya Upashanaji Habari Ulimwenguni 2025:Mawasiliano ya matumaini

Papa Francisko anawaalika wataalamu wa vyombo vya habari kupendelea njia isiyo ya uadui ya kuwasiliana na kutoa taarifa ambazo haziuzi udanganyifu au hofu lakini zinazojua jinsi ya kutafuta na kueneza historia zinazosukana na wema kwa kuufanya ulimwengu uache kutosikia kilio cha maskini.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Wawasilianaji wa upole katikati ya vita vilivyotengenezwa kwa maneno, ambayo mara nyingi huwasha chache ya vita vinavyotengenezwa na mabomu na damu. Wanawake na wanaume sawa na kwa wachimba dhahabu, kuwinda "cheche za mema," za historia zinazopanua moyo na kuzalisha udugu, huku zikiondoa kutojali, kutoaminiana na chuki. Kwa kifupi, wawasilianaji wa matumaini popote walipo wanaweza kuweka kiota. Hiyo ndiyo ndoto ya kuona wataalamu wa vyombo vya habari katika Mwaka wa Jubilei 2025. Baba Mtakatifu Francisko amezungumza hayo katika ujumbe wake wa Siku wa 59 ya Hupashanaji Habari duniani  uliochapishwa siku ya Ijumaa tarehe 24 Januari 2025,  katika siku ambayo Mama Kanisa anafanya kumbukumbu ya Mtakatifu Francis wa Sales, Msimamizi wa Waandishi wa Vyombo vya habari. Na  Ujumbe wake unaongoza na kauli Mbiu iliyotolewa katika kifungu cha Barua ya Kwanza ya Mtakatifu Petro kisemacho: “Shirikishaneni kwa upole matumaini yaliyomo moyoni mwenu(1Pt 3,15-16).

Mawasiliano yanayoibua woga na kukata tamaa,ubaguzi,chuki na itikadi

Ujumbe huo wa Papa ulioanzia kwenye uchunguzi wa njia za sasa za kutoa taarifa ambazo anasisitiza kuwa mara nyingi huwa hazina matumaini. Papa Francisko anaandika kwamba kuna mawasiliano ambayo huibua woga na kukata tamaa, ubaguzi na chuki na itikadi.” Kuhusiana na hilo mara nyingi sana hurahisisha ukweli kwa kuupunguza kuwa kauli mbiu  ya kuchochea hisia za kisilika hadi kufikia hatua ya kueneza habari za uwongo au potofu kwa ustadi wa kutuma jumbe zinazokusudiwakusisimua akili za watu, kuchokoza na kuumiza. Njia ya kujieleza, ambayo inasaliti mawasiliano yanayotokana na uchokozi kuanzia  maonesho ya mazungumzo hadi "vita vya matusi kwenye mitandao ya kijamii, dhana ya ushindani, na upinzani kuna hatari wakati wote, hadi udanganyifu  kwa maoni ya umma.

Ndoto ya Papa:Mawasiliano ya kusindikiza kaka na dada katika tumaini

Katika kukabiliana na hali hii iliyoakisiwa na matukio ya kutia wasiwasi  na sio kwa uchache kile ambacho Papa anafafanua kama utawanyiko uliopangwa wa tahadhari, unaosababishwa na mifumo ya kidigitali ambayo inatuonesha kulingana na mantiki ya soko na kurekebisha mtazamo wetu wa ukweli, ni muhimu, kuepuka mantiki ya mawasiliano ambayo yanahitaji kutambua na kisha kushambulia adui. Matumaini ya Papa Fransisko, au tuseme ndoto yake ni  ile ya  mawasiliano yanayoweza kutufanya kuwa wenzi katika safari ya kaka na dada zetu wengi, ambayo yanawasha upya matumaini ndani yao katika wakati wa taabu. Kwamba yanazungumza kwa moyo yakiamsha si miitikio ya shauku ya kufungwa na hasira, bali mitazamo ya uwazi na urafiki; yenye uwezo wa kuzingatia uzuri na matumaini hata katika hali zinazoonekana kukata tamaa.

Kutunga historia zenye matumaini

Dhana inayotia msukumo wa maono ya Papa, ambayo tunayosoma katika ujumbe wake  inatokana na waraka wa kwanza wa Mtakatifu Petro, ambamo mtume huyo anawaalika Wakristo “wawe tayari siku zote kumjibu mtu awaye yote awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yake:”  Msukumo ambao  Papa Fransisko anabainisha kuwa una ujumbe wa aina tatu za kawaida za mawasiliano ya Kikristo: kujua jinsi ya "kuona mabaki ya mema yaliyofichwa hata wakati kila kitu kinaonekana kupotea; kujua jinsi ya kurejesha uzuri wa upendo wa Mungu na upya wake, na kujua jinsi ya kuwasiliana kwa upole. Papa Francisko anabanisha kuwa "Ninaota mawasiliano ambayo hayauzi udanganyifu au hofu, lakini yanaweza kutoa sababu za matumaini."

Lazima tupone magonjwa ya kimbele mbele na kujitosheleza

Na ili kufanya hivyo, Papa anaonesha, njia kwamba "lazima tupone kutokana katika magonjwa' ya kimbele mbele na kujitoshereza, na kuepuka hatari ya kujizungumza sisi wenyewe." Na kutunga mawasiliano hata zaidi katika mwelekeo wa Jubilei, iliyojaa "athari za kijamii",Papa Francisko kwa mara nyingine tena anapendekeza matumizi ya historia zenye matumaini, historia hizo za wema wa kugunduliwa na kusimuliwa kwa kuzifuatilia"katika mikunjo ya habari. Inapendeza kupata mbegu hizi za tumaini na kuzifanya zijulikane na ili ulimwengu uwe angalau kiziwi kidogo kwa kilio cha wa walio maskini, kutojali kidogo na kufungwa kidogo." 

Ujumbe wa Papa wa Siku ya 59 ya Hupashanaji habari 2025
24 Januari 2025, 11:05