杏MAP导航

Tafuta

2025.01.19-Papa-katika kipindi cha "Che tempo che fa" nchini Italia. 2025.01.19-Papa-katika kipindi cha "Che tempo che fa" nchini Italia. 

Papa:Mwanamke atakuwa Gavana wa mji wa Vatican!

Katika mahojiano ya Papa na mwandishi wa Habari wa Italia Fabio Fazio katika kipindi cha:“Che tempo che fa”,alitangaza mwanamke mwingine mtawa atakapewe hadhi ya kuwa Gavana wa Vatican.Papa Francisko alijibu swali kuhusu masuala nyeti ya mipango mipya ya utawala wa Trump kwa kufukuza wahamiaji:ikiwa itakuwa hivyo itakuwa bahati mbaya,hatuwezi kuwafanya walio maskini zaidi walipe gharama ya kukosekana kwa usawa katika jamii.

Vatican News

Awali ya yote kuna mapya, mwanamke, Sr Raffaella Petrini, kuanzia mwezi Machi atakuwa Gavana wa Mji wa Vatican. Baadaye mtazamo wa uchungu ambao utajitokeza kwa kuwafurusha kwa wingi wahamiaji wa Marekani, furaha kwa ajili ya kusimamisha mapigano Gaza, na matashi mema kwa ajili ya suluhisho mbili. Na bado, makaribisho ya wahamiaji, Jubilei, ufunguzi wa Mwaka Mtakatifu katika gereza, mapambano ya nyanyaso, na afya binafsi. Mada za sasa na changamoto za ulimwengu ambazo Kanisa Baba Mtakatifu, wamekabiliana nazo katika mahojiano na Mwandishi wa habari Fabio Fazio katika kipindi cha kiitaliano cha "Che Tembo Che fa," kilichofanyika usiku wa tarehe 19 Januari 2025 kwenye chaneli ya Tisa nchini Italia.

Hata hivyo fursa kama hii tayari kunako 2022 Papa Francisko alikuwa ameruhusu mahojiano katika kipindi kile kile, na cha pili kunako 2024 na kwa njia hiyo  katika mahojiano mapya ya karibu saa nzima hivi, ilikuwa ni fursa hata kwa ajili ya kuwakilisha wasifu wake wenye kichwa cha  Spera kilichohaririwa na mwandishi wa Habari Carlo Musso, na kuchapishwa na Mondadori na kimetolewa katika Nchi 100 ambapo ni: kazi ya kina sana" inayojumuisha historia nyingi zinazotoa maana ya mimi ni nani."

Sr Petrini  Gavana wa mji wa Vatican

Papa Francisko mara baada ya kutuliza hali yake ya mkono ulioshutuka siku ya Alhamisi(Januari 16) alisema “kwa sasa ni nafuu na alitangaza kuwa kuanzia mwezi Machi, baada ya Kardinali Vergéz Alzaga, kustaafu, Katibu wake Sr Raffaella Petrini ndiye atachukua nafasi ya kuwa Gavana wa mji wa Vatican. Kwa hiyo ni mwanamke mwingine atakayeongoza ofisi muhimu, baada ya kutangazwa kwa Sr Simona Brambilla kama Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maisha ya Kitawa. “Kazi ya wanawake katika Curia zote ni muhimu na ambayo imekwenda taratibu na inaeleweka vizuri. Sasa tunao wengi,” Papa alitoa maoni yake.  Papa aliorodhesha nafasi zilizopewa na sura ya wanawake mjini Vatican na kuongeza; katika utawala, Katibu wa Gavana atakuwa pia mwanamke pia ambaye ni Sista.”  Kwa hiyo "Wanawake wanajua jinsi ya kusimamia vyema kuliko sisi wanaume."

Mpango wa kufukuza wahamiaji wengi huko Marekani

Papa Francisko alijibu baadaye swali kuhusu Marekani katika nuru ya uvumi fulani kuhusu uwezekano wa mpango wa kufukuzwa kwa wahamiaji wengi mara tu baada ya Rais Donald Trump kuapa. Kuhusiana na suala hilo kama likitendeka, Papa alifafanua kama"bahati mbaya", kwa sababu "huwafanya maskini kuwa na bahati mbaya ambao hawana chochote cha kulipa gharama ya usawa".

Mapokezi ya wahamiaji na kupungua kwa watoto Italia

Mada ya wahamiaji ambayo Papa Francisko alirudia kwa maneno manne ili kuweza kukabiliana na dharura ambapo: “ Wahamiaji wanapaswa kupata kazi, kusindikizwa, kuhamasishwa na kufungamanishwa.” Na alirudia juu ya mada ambayo ni pendwa kuhusu ukupungua kwa watoto ambao unatazama nchi ya Italia ambayo umri wa kati ni kuanzia miaka 46.” Kwa maoni yake alisema:“ Ikiwa hawazai watoto, wafanye waingie wahamiaji.”

Suluhisho la kuwa na Serikali mbili na umuhimu wa amani

Katika mahojiano hayo hapakukosekana na swali kuhusu Mashariki ya Kati na mwanzo wa kusitisha mapigano huko Gaza na kuachiliwa kwa wanawake waliotekwa nyara na Hamas. Kama Papa Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana Dominika tarehe 19 Januari 2025 alivyoeleza shukrani kwa waliongilia kati na kuwapongeza na baadaye alitoa maoni ya uwezekano wa Nchi mbili: “ Ninaamini kuwa hiyo ndiyo suluhisho. Uwezekano kwa baadhi wanao na wengine hapana.” Papa aliongeza: “Amani ni mkuu wa vita lakini inahitaji ujasiri” na ili kufanya hivyo ni kwa sababu, wakati mwingine unapoteza kitu lakini unapokea sana.“ Vita kinyume chake daima ni kushindwa” Papa alisisitiza na kusema thamani ya mchakato wa majadiliano  na kutangaza na kukashifu mapato “makubwa” ya viwanda vya kutengeneza silaha vinavyosababisha “maangamizi.”

Tusisahau wafungwa

Papa Francisko baadaye alizungumzia matumaini, kiini cha Jubilei: Ni nanga katika mchanga, ambamo inashikiria na kusisisitiza akifikiria mahubiri ya ufunguzi wa Mlango Mtakatifu katika Gereza la Rebbibia. Ni ishara isiyo na kifani ambayo Papa alipenda kutimiza “ kwa sababu katika moyo daima kuwa wafungwa.” Tusisahau wafungwa,” ndiyo wito wake “  wengi walio nje ndiyo walio na makosa mengi zaidi yao.”

Aibu na uchungu kwa vifo vya mauaji ya kimbari

Siku chache kabla ya Siku ya Kumbukizi ya tarehe 27 Januari, kuhusu mauaji ya kimbari ya Wayahudi, Papa Francisko alisema anavyohisi “hisia ya huruma na aibu” kwa janga lile ambalo aliweza kugusa kwa mkono wake katika ziara yake huko Auschwitz kunako 2016, kwa maelezo, filamu na shuhuda za mwanamke mashuhuri Edith Bruck, mshairi wa Hungaria wa umri wa miaka 92 ambaye ni mhanga wa mauaji ya kimbari.

Nyanyaso, vijana, dhambi

Nafasi nyingine katika mahojiano kulikuwa na mada nyingine za nyanyaso, ambapo alisema: “nyanyaso ni ubaya mkubwa sana, ambao lazima kupambana sana”: dharura kwa vijana ambao lazima “kuwasindikiza; ukaribu wa wote bila umalaika katika maono ya dhambi na bila kuweka yote katika dhambi za mwili.” "Inanichukiza wakati watu wengine kila wakati wanatafuta hilo katika Ungamo," Papa alisema. Na ninarudia: “Hakuna dhambi isiyoweza kusamehewa; hakuna. Kwa maana Mungu anataka kuwa na kila mtu pamoja naye, kama watoto, kama ndugu miongoni mwetu."

Kujikwaa katika kikanisa cha Sistine

Papa Francisko hatimaye alifichua simulizi ya udadisi kama vile "jikwao lake la kwanza" kwenye ngazi za Kikanisa cha Sistine mara baada ya kuchaguliwa kwake, wakati akienda kusalimiana na Kardinali aliyekuwa katika kiti cha magurudumu: "Papa asiyeweza kukosea alianza na kitu ambacho kilishindikana: alijikwaa!" Na kwa kumalizia na ombi la Mwaka Mtakatifu wa Jubilei 2025 Papa alimwambia kwamba: "Usiruhusu fursa hii kupita. Nenda mbele na uwe jasiri. Na usipoteze hisia zako za ucheshi."

Papa na Che tempo che Fa

 

20 Januari 2025, 09:55