Papa kwa wakuu wa Seminari Kuu na Ndogo za Ufaransa:Wao ni kama Eli,kuwatia moyo na kuwalekeza vijana
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko akikutana mjini Vatican na Wakuu wa Seminari Kuu na Ndogo za chini Ufaransa, Jumamosi tarehe 25 Januari 2025 alionesha furaha ya kuwakaribisha katika maadhimisho ya hija yao ya Jubilei, ambapo wamekusanyika kutafakari majiundo ya kipadre. Hii ni njia ya utambuzi ambayo wanachukua jukumu muhimu. Wao ni kama kuhani mzee Eli aliyemwambia kijana Samweli: “Akikuita, sema, Nena, Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikia”(1Sam 3:9). Wao ni uwepo wa kutia moyo na kuwapa dira vijana waliokabidhiwa uangalizi wao. Mtakatifu Paulo VI alithibitisha kwamba “mtu wa sasa anasikiliza mashahuda kwa hiari zaidi kuliko waalimu, au kama anawasikiliza walimu, ni kwa sababu wao ni mashuhuda” (Katekesi tarehe 2 Oktoba 1974). Hii hakika inatumika kwa wakufunzi katika seminari. Ushuhuda wao thabiti wa maisha ya Kikristo unafanyika ndani ya jumuiya ya elimu, ambayo washiriki wake katika seminari, ni askofu, mapadre na watawa, maprofesa, na wafanyakazi. Jumuiya hii, hata hivyo, inaenea popote mseminari anapotumwa: katika parokia, harakati za kitume na familia.
Kwa hivyo Papa ameongeza kusisitiza kuwa malezi ya jumuiya ni ya umoja – hata kama ni Jumuiya inayogusa vipimo vyote vya mtu na mwelekeo wa kuelekea kwenye utume. Ili mseminari aweze kutoa ushuhuda huu na kuwa nafasi nzuri kwa ukuaji wa padre wa siku zijazo, ni muhimu kutunza ubora na uhalisi wa mahusiano ya kibinadamu yanayopatikana huko, sawa na yale ya familia, sifa za ubaba na udugu. Ni katika hali hiyo tu ndipo kuaminiana kunaweza kuanzishwa, ambayo ni muhimu kwa utambuzi mzuri. Mseminari basi ataweza kuwa yeye mwenyewe, bila woga wa kuhukumiwa kiholela; kuwa wa kweli katika mahusiano na wengine; kushirikiana kikamilifu katika malezi ya mtu mwenyewe ili kugundua, pamoja na waundaji, mapenzi ya Bwana katika maisha ya mtu na kujibu kwa uhuru. Watahiniwa wanaojiwasilisha kwenye seminari, leo hii zaidi ya hapo awali, ni tofauti sana kutoka kwa kila mmoja. Wengine ni wadogo sana, wengine tayari wana uzoefu wa maisha marefu; wengine wana imani ya muda mrefu na kukomaa, na kwa wengine ni ya hivi karibuni sana, kutokana na miktadha ya kijamii na wanafamilia mbalimbali, kutoka tamaduni mbalimbali; na juu ya yote, walihisi wito ndani ya harakati nyingi za kiroho ambazo Kanisa linafahamu leo hii..
Papa Francisko amesisitizia hilo kuwa “Kuna wagombea wengi ambao wanatoka kwenye harakati. Kwa hakika ni changamoto kubwa kutoa malezi ya kibinadamu, kiroho, kiakili na kichungaji kwa jumuiya hiyo yenye watu mbalimbali.” Kazi yao si rahisi. Ndio maana umakini kwa safari ya kila mtu na vile vile usaidizi wa kibinafsi ni muhimu zaidi kuliko hapo awali. Hii ndiyo sababu ni muhimu kwamba timu za mafunzo zikubali utofauti huo, kwamba wajue jinsi ya kuukaribisha na kuusindikiza. Wasiogope utofauti! Wanao lakini ni zawadi! Elimu katika kuwakaribisha wengine, jinsi walivyo, jinsi walivyo, itakuwa dhamana, kwa siku zijazo, ya ukuu wa kidugu na ambao kimsingi umeungana. Kusudi la seminari ni wazi la “kuunda wanafunzi wamisionari "kwa upendo" na Bwana, wachungaji wa kuwa harufu ya kondoo", wanaoishi kati yao ili kuwahudumia na kuwapelekea huruma ya Mungu.” Katika hili Papa amesisitiza kuwa hiyo inapendekeza idadi fulani ya vigezo, ambavyo haviwezekani kuafikiana, ili kutoa upangaji. Seminari, hata hivyo, haipaswi kutafuta mafunzo ya yanaoyofanana na ambayo wote wafikiri kwa njia sawa, ambao wanafikiri kwa ladha sawa na chaguo sawa, hii sio nzuri
Neema ya sakramenti hukita mizizi katika kila kitu kinachorutubisha utu wa pekee wa kila mtu, utu unaopaswa kuheshimiwa, ili kuzalisha matunda ya ladha mbalimbali, ambayo watu wa aina mbalimbali wanahitaji. Na kati ya mambo ambayo ni muhimu kuzingatia, Papa Francisko alipenda kuakisi mambo matatu. La kwanza ni kuhakikisha kuwa uhuru wa kweli wa ndani unaundwa kwa mgombea.Papa amesema “Msiogope uhuru huu! Changamoto zitakazojitokeza kwake katika maisha yake zinahitaji kujua, kuakisiwa na imani na kusukumwa na upendo, kwa jinsi ya kuhukumu na kuamua kwa kichwa chake mwenyewe, wakati mwingine dhidi ya sasa au kuhatarisha, bila kujilinganisha na yaliyopangwa majibu tayari au dhana tangulizi za kiitikadi au kwa wazo moja la wakati huu.” Papa amesema kuwa “Akili ikomae na moyo ukue na mikono ikue.” Mambo matatu ambayo ni lazima yawe madhubuti, na thabiti ni kile mtu unachofikiri, anachohisi na anachofanya. Kwa njia hiyo ni Lugha tatu: ile ya akili, ya moyo na ya mikono. Na kuwe na mshikamano kati ya haya matatu.”
Hoja ya pili Papa amesema inahusu kukomaa kwa mtahiniwa wa ubinadamu wenye usawa na uwezo wa mahusiano ya kibinadamu. Kuhani lazima awe na mwelekeo wa upole, ukaribu na huruma. Hizi ndizo sifa tatu za Mungu: upole, ukaribu na huruma. Mungu yu karibu, ni mpole, ni mwenye huruma. Mseminari asiye na uwezo wa hili hana jema. Ni muhimu,” Papa ameeleza. Hakuna haja ya kusisitiza juu ya hatari inayowakilishwa na watu ambao ni dhaifu sana na wenye misimamo mikali, au na matatizo ya kihisia. Kwa upande mwingine, mtu mkamilifu hayupo na Kanisa linaundwa na washiriki na wadhambi dhaifu ambao wanaweza daima kutumaini maendeleo; Utambuzi wao juu ya jambo hili lazima wawe wa busara na wavumilivu, wakiwa na tumaini. Papa amesisitiza kuwa wasiogope udhaifu na mapungufu ya waseminari wao! Wasiwashutumu haraka na kujua jinsi ya kuwasindikiza. Kile kilichoitwa kifo cha kishahidi cha subira; kiwaongoze.
Jambo la tatu ni mwelekeo wa wazi wa wito wa kipadre kuelekea utume. Papa amesema kuwa “Padre ni wa utume . Padre anayefanya kazi na kubaki Monsinyo, si wa utume. Hii si sawa. Kuhani ni wa uutume wa kimisionari siku zote.” Ingawa, bila shaka, kuwa kuhani kunahusisha utimilifu wa kibinafsi, mtu hafanyiki kwa ajili yake mwenyewe, bali kwa Watu wa Mungu, kuwafanya wamjue na kumpenda Kristo. Sehemu ya kuanzia ya nguvu hii inaweza kupatikana katika upendo wa kina zaidi tu na upendo wa dhati kwa Yesu, unaostawishwa na malezi mazito katika maisha ya ndani na kwa kujifunza Neno la Mungu. Ni vigumu kufikiria wito wa kipadre usio na mwelekeo thabiti wa kujitolea, ukarimu na kujitenga na nafsi yao, unyenyekevu wa dhati; na hili linahitaji kuthibitishwa.
Yesu pekee ndiye anayemjaza kuhani wake furaha. Kwa sasa haishangazi kwamba njiani, wengine huishia kidogo kidogo "kujitumikia". Kwa njia hiyo ameomba wawe waangalifu hasa kwa upenda wa fedha. Papa ametoa mfano mmoja kuwa “Bibi yangu kila wakati alituambia: "Shetani huingia kupitia mifukoni." Kwa hiyp Tafadhali umaskini ni kitu kizuri sana. Watumikie wengine. Na muwe waangalifu na taaluma. Papa amekazia kuwaomba wajihadhari na mambo ya dunia, wivu na ubatili... ikiwa upendo kwa Mungu na kwa Kanisa wakati inakuwa si chochote ila ni kisingizio cha kujisherehekea hiyo ni mbaya sana. Na Padre anapata kikanisa fulani na akawa tausi ni mbaya. Upendo huo kwa Mungu na Kanisa usiwe kisingizo bali ni wa kweli. Papa Francisko ameashukuru Gambera ota kwa ziara na kwa huduma wanayotoa kwa Kanisa. Kazi yao si rahisi, lakini Papa aliwahimiza kudumu kwa uaminifu na matumaini, chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu na ulinzi wa Bikira Maria. Kwa hilo aliwabariki kutoka moyoni mwake, jumuiya zao na tafadhali, wasisahau kumuombea.