Papa Francisko:kutuliza ni kazi ya moyo,familia zilizojeruhiwa zinapaswa kusindikizwa!
Vatican News
"Piazza San Pietro", gazeti jipya la Basilika lenye majibu ya Papa kwa waamini. Weka moyo wako kwenye uwanja. Hili ndiyo jambo kuu katika mahusiano,Baba Mtakatifu Francisko ameandika hayo akijibu swali katika toleo jipya la “Piazza San Pietro”(Uwanja wa Mtakatifu Petro) – gazeti la kila mwezi la Kanisa Kuu la Vatican linalopembua tema za imani, kiroho na maisha ya kila siku kwa njia ya michango mbalimbali, akijikita katika safari ndani ya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, katika barua iliyotumwa kwake na Giorgio, baba mmoja wa Roma ambaye anasimulia uzoefu wake mgumu wa kutengana na mke wake. "Ni kuanzia moyoni tu familia zetu zitaweza kuunganisha akili na nia tofauti na kuzituliza ili Roho aweze kutuongoza kama mtandao wa ndugu, kwa sababu kutuliza pia ni kazi ya moyo" alifafanua Papa Francisko, na hii ni "muujiza wa kijamii" ambao unawezekana tu ikiwa moyo wetu "umeunganishwa na ule wa Kristo" na kwa njia hiyo tu "itawezekana kuacha na kuzuia vurugu katika familia."
Historia ya Giorgio
Giorgio alimwambia Papa kwamba alitengana baada ya miaka 5 ya ndoa na binti wake kwa ombi la mke wake "ambaye alikuwa na mwanamume mwingine." Miaka kadhaa baadaye, mwanamke huyo alimwomba hakimu pasipoti ya mtoto na "kuhamia Athene na mpenzi wake mpya, mwenye asili ya Kigiriki", lakini hakimu alikataa. Mwezi mmoja baadaye Giorgio alikamatwa kwa sababu polisi walikuta dawa za kulevya kwenye gari lake huku binti yake akiwa naye. “Nikiwa gerezani nilisali kwa muda mrefu kwa Padre Pio wa Pietrelcina,” alieleza. Baada ya siku 8, kimiujizawaligundua ukweli na kuniachia huru,"(hivyondivyo mahakimu na polisi waliniambia). Kisha mama-mkwe wa zamani na washirika wengine wawili walitiwa hatiani. Giorgio anamwambia Papa kwamba amebadilisha "uovu uliopokelewa kuwa mzuri kwa wengine" na kwa hivyo ameshinda "chuki na kisasi" ndani yake, nikichukua "njia pekee iliyookoa maisha yangu, ya kuwa na mwitikio kwa kuhusisha watu wengi kwa miaka mingi katika hali sawa na yeye, kupata marekebisho hayo ya sheria ya familia ambayo yanahakikisha haki ya watoto wa wazazi waliotengana kuwa na uwezo wa kupenda tu wazazi na babu na bibi zao." Giorgio alimwomba Papa Francisko kushiriki "utetezi wa haki hii isiyokiukwa ya watoto ambayo inapaswa kulindwa daima na kusisitiza kwamba tunapaswa kuacha ukatili unaotumia na kuwanyonya watoto kwa mabishano, udhalilishaji na unyanyasaji unaoweza kusababisha majanga makubwa sana ya familia na mauaji na kujiua.”
Ushuhuda wa amani
Papa alieleza, kuwa “historia yake ni ushuhuda wa amani, ambayo inatia moyo katika ulimwengu uliochochewa na vita na chuki, ambayo inalingana na msukosuko mkubwa wa tumaini, ambao badala yake uko sikuzote kwa ajili ya kila mtu.” Baba Mtakatifu alibanisha kwamba “kwa jina la masilahi ya mtu binafsi, yakiwemo ya kihisia, unyanyasaji na dhuluma hufanywa, wakifikiri kwa njia hii kwamba wanajijengea ustawi na badala yake wanajidhuru” na kwamba hilo hutokea “katika uvamizi na unyanyasaji wa mizozo ya ulimwengu, kama katika maisha ya kibinafsi na ya familia na anatumaini, huku akishiriki kile Giorgio anapendekeza, kwamba kuna sheria zinazozidi kutosha kuruhusu watoto wa wazazi waliotengana kukutana na kukua kihisia na kwa upendo na wanafamilia wao wote."
Kusindikiza familia zilizojeruhiwa
Katika majibu yake kwa Giorgio, kutoka kurasa za "Piazza San Pietro",Papa Francisko anapendekeza kwamba jumuiya za Kikristo "zisindikizane na familia zilizojeruhiwa ili watoto wasiwe mateka wa baba na mama zao."Wakati fulani sisi ni “mateka wa ubinafsi wa moyo wa mwanadamu, unaotufanya kuwa wabaya. Ubinafsi hautufanyi kuwa wazuri,” aliongeza Papa, ambaye alihimiza kuwa tusiwafanye watoto kuwa mateka wa baba au mama, lakini watoto wa kupendwa na kuwalinda na kututaka tuwe waangalifu hata katika zawadi kwa watoto wetu, kwa sababu wanaweza kuwa usaliti wa kweli ili kuwaondoa kutoka katika upendo wa mume au mke. "Hivyo zawadi ni kama kupaka rangi ya upendo, udanganyifu, ambao unachukua ukweli kutoka katika upendo, na hivyo ndiyo kwa heshima na huruma, ndiyo kwa haki ya huruma na hakuna kisasi na chuki, mitandao na mikutano lazima kukuzwa ili kueneza tumaini kwamba tunaweza kujiweka huru kutoka katika vifungo vya uovu, ili kujiponya wenyewe, kuinuka na kubadilisha uovu kuwa wema,” anahitimisha Baba Mtakatifu.
Katika toleo la Januari la:"Piazza San Pietro", pamoja na maneno ya Papa, picha zilizochukuliwa na mpiga picha wa Marekani Steve McCurry zinasimama, mwandishi maarufu "Msichana wa Afghan, " mwenye uwezo wa kuanzia upigaji picha wa mitaani, kwa kupiga picha za vita na mijini, katika picha zake anarejesha uzuri na hali ya kiroho ya kitovu cha Ukristo. Kisha Kardinali Pietro Parolin anazindua “kilio dhidi ya vita vya dunia vilivyomegeka vipande vipande”, huku mchango wa Susanna Tamaro unaoitwa “Tumaini huzaliwa kutokana na imani”, hutuongoza kutafakari umuhimu wa kuamini nyakati ngumu.