Papa,Katekesi ya Jubilei 2025:Yesu ni tumaini la Israeli linalotimizwa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika mzunguko wa Katekesi ya Jubilei 2025 inayohusu, Yesu Kristo Tumaini letu” Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 29 Januari 2025, alijikita na mada ya “Utoto wa Yesu: Ataitwa Yesu (Mt 1,21).Tangazo kwa Yosefu.” Kwa kuongozwa na Somo la Injili ya Matayo( Mt 1,18-21), ambalo baada tangazo kwa Maria kuwa Mama wa Mungu pia Yosefu kutaka kumuacha kwa siri baada ya kujua kwamba ni Mjazito, Baba Mtakatifu alisema kuwa: Leo tunaendelea kumtafakari Yesu katika fumbo la asili yake kama inavyosimuliwa katika Injili za utoto wake. Ikiwa Luka anaturuhusu kufanya hivyo ni kwa sababuYosefu anachukua ukoo halali wa Yesu, kumpandikiza kwenye shina la Yese na kumuunganisha na ahadi aliyopewa Daudi. “Yesu, kwa hakika, ndiye tumaini la Israeli ambalo linatimizwa”: Yeye ni uzao aliyeahidiwa kwa Daudi(taz. 2 Sam 7:12; 1 Nya 17:11), ambaye anaifanya nyumba yake “ibarikiwe milele”(2 Sam 7:29) ); ni chipukizi linalochipuka kutoka kwenye shina la Yese(taz. Isa 11:1),“chipukizi la haki” lililokusudiwa kutawala kama mfalme wa kweli, anayejua jinsi ya kutekeleza sheria na haki(taz. Yer 23:5; 33:15).
Baba Mtakatifu Francisko aliendelea kusisitiza kuwa, Yosefu anaingia katika tukio katika Injili ya Mathayo kama mchumba wa Maria. Kwa Wayahudi, uchumba ulikuwa kifungo halisi cha kisheria, ambacho kilitayarisha kile ambacho kingetokea mwaka mmoja baadaye, yaani, sherehe ya ndoa. Hapo ndipo mwanamke huyo alipopita kutoka chini ya ulinzi wa baba hadi kwa mume wake, akihamia nyumbani kwake na kujitolea kwa zawadi ya uzazi. Ni katika kipindi hicho ambacho Yosefu aligundua ujauzito wa Maria na upendo wake uliwekwa kwenye jaribu kali. Akikabiliwa na hali kama hiyo, ambayo ingesababisha kuvunjika kwa uchumba, Sheria ilipendekeza masuluhisho mawili yanayoweza kutokea: au kitendo cha kisheria cha umma, kama vile kumwita mwanamke mahakamani, au hatua ya faragha kama vile kuwasilisha barua ya talaka kwa mwanamke huyo.
Mathayo anamfafanua Yosefu kama mtu "mwenye haki" (zaddiq), mtu anayeishi kwa Sheria ya Bwana, ambaye alichota msukumo kutoka kwayo katika kila tukio la maisha yake. Kwa hiyo, akifuata Neno la Mungu, Yosefu alitenda kwa uangalifu: hakujiruhusu kulemewa na hisia za kisilika na woga wa kumkaribisha Maria nyumbani kwake, bali alipendelea kuongozwa na hekima ya kimungu. Alichagua kutengana na Maria bila ugomvi, faraghani(taz.Mt 1:19). Na hii ndiyo hekima ya Yosefu inayomruhusu kutofanya makosa na kuwa muwazi na mtiifu kwa sauti ya Bwana. Kwa njia hii Yosefu wa Nazareti anamkumbusha Yosefu mwingine, mtoto wa Yakobo, aliyepewa jina la utani “Bwana wa ndoto”(rej. Mwa 37:19), aliyependwa sana na baba yake na kuchukiwa sana na ndugu zake, ambapo Mungu alimwinua kwa kumfanya aketi kwenye mahakama ya Farao. Kwa hiyo sasa, Yosefu wa Nazareti anaota nini? Anaota muujiza ambao Mungu anafanya katika maisha ya Maria, na pia muujiza ambao anafanya katika maisha yake mwenyewe: kuchukua ubaba wenye uwezo wa kulinda, kutunza na kusambaza urithi wa kimwili na wa kiroho.
Tumbo la uzazi wa Mchumba wake lina mimba ya ahadi ya Mungu, ahadi ambayo ina jina ambalo hakika ya wokovu linatolewa kwa wote (taza Mndo 4:12). Katika usingizi wake Yosefu anasikia maneno haya: “Yosefu, mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria mkeo nyumbani kwako. Kwa maana mtoto ambaye alichukuliwa mimba kutoka kwa Roho Mtakatifu; atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao”(Mt 1:20-21). Akikabiliwa na ufunuo huo, Yosefu hakuomba uthibitisho zaidi, aliamini. Yosefu alimwamini Mungu, alikubali ndoto ya Mungu kwa maisha yake na ya mchumba wake. Hivyo aliingia katika neema ya wale wanaojua jinsi ya kuishi ahadi ya kimungu kwa imani, matumaini na upendo.
Katika haya yote, Yosefu hakusema neno, bali aliamini, alitumaini na alipenda. Hakuonesha kwa "maneno matupu", bali kwa ukweli halisi. Yeye ni wa ukoo wa wale ambao mtume Yakobo, aliwafafanua kuwa "wanaoweka Neno katika matendo" (rej. Yakobo 1:22), akilitafsiri katika matendo, katika mwili, na katika maisha. Yosefu alimwamini Mungu na kutii: "Kuwa kwake macho ya ndani kwa ajili ya Mungu ... kwa hiari kunakuwa utiifu" (Benedikto XVI, Utoto Yesu, Milano-Vatican 2012, 57). Papa Francisko kwa kuhitimisha aliosema “tumwombe Bwana neema ya kusikiliza zaidi ya kunena, neema ya kuota ndoto za Mungu na kumkaribisha Kristo kwa uwajibikaji ambaye tangu tunabatizwa anaishi na kukua katika maisha yetu.”