Papa Fransisko anapongeza juhudi za kujitolea huko Valencia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 30 Januari 2024, amekutana na Maaskofu, waseminari na walezi Kanda ya Kikanisha nchini Hispania ya Valencia, Valencia, Orihuela-Alicante, Segorbe-Castellan, Mallorca, Menorca na Ibiza. Katika hotuba yake, Baba Mtakatifu Francisko, ameeleza hisia zake akifikiri, siku kuu ya Noeli ambayo bila shaka ni utamaduni na uzoefu wa Mungu aliyejifanya matope kwao. Hii ni kutokana na Eneo hilo nchini Hispania ambalo lilikumbwa na mafuriko makubwa yaliyosababishwa na kimbunga Dana mwishoni mwa 2024 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 200 na uharibifu mkubwa.
Papa alisema kuwa “ Si rahisi kueleza hisia zangu ninapofikiria kuhusu sikukuu za Noeli bila shaka zisizo za kawaida na uzoefu huo wa maisha wa "Mungu alifanyika matope" ndani yenu. Maumivu na maombolezo ambayo, licha ya ukali laini , yaliwafungua matumaini kwa sababu, kwa kutulazimisha kugonga mwamba na kuacha kila kitu ambacho kilionekana kutuunga mkono, huturuhusu kwenda mbali zaidi. Sio jambo ambalo tunaweza kufanya peke yetu, ni giza kubwa ambalo wamepitia na wanaendelea kupitia.”
Papa alifikiria juu ya usaidizi wa watu wengi na sura za kujitolea kwa watu, ambao waliweza kuakisi huruma ya Mungu. Huu ndio uwanja ambao wameitwa kufanya kazi. “DANA sio jambo la kawaida ambalo tunatumaini kuwa halitatokea tena, ni udhihirisho wa kile ambacho kila mwanadamu hupitia wakati anapaswa kukabili hasara na kujisikia peke yake, kuchanganyikiwa na kuhitaji msaada ili kuweza kuendelea. Yesu anasema waziwazi: kwa sababu amenitia mafuta, ili kuponya waliovunjika moyo, kutangaza mwaka wa neema ya Bwana” (taz. Isa 61:1; Lk 4:18).” Papa aliendelea kusema kuwa “ Tayari tuko katika Mwaka huu wa Neema, ambao nilitaka kuuweka wakfu kwa matumaini, na ambao mtaishi kwa nguvu zake zote kwa kutafakari maneno haya.” “Wakati mwingine nimesema kwamba tumaini sio tumaini, tu bali matumaini ni usemi mwepesi, wa kitu kingine. Hatuwezi kuchukulia mateso ya watu kuwa kirahisi na kujaribu kuwafariji kwa mielekeo na kutenda wema. Tumaini letu lina jina, yaani Yesu, kwamba Mungu ambaye hakuchukizwa na matope yetu na ambaye, badala ya kutuokoa kutoka katika matope, yeye alifanyika matope kwa ajili yetu, ” alisisitiza Papa.
Na kuwa kuhani ni kuwa Kristo mwingine, inakuwa tope katika machozi ya watu, na mnapoona watu wamevunjika, kwa sababu huko Valencia kuna watu waliovunjika, watu wamepoteza maisha yao vipande vipande, mjitoe kama Kristo anavyofanya katika Ekaristi. Kwa njia hiyo Papa Francisko anahimisha kuwa Tafadhali, wajitoe bure, kwa sababu kila kitu walicho nacho wamepokea bure, na wasisahau kuhusu kutoa bure. Papa Francisko ahikitimisha huku akiwaombea.