杏MAP导航

Tafuta

 Vita nchini Sudan vinasababisha hali ngumu ya kibinadamu. Vita nchini Sudan vinasababisha hali ngumu ya kibinadamu.  (AFP or licensors)

Papa atoa wito wa kusitisha mzozo nchini Sudan

Kusitisha mzozo Sudan unaopelekea hata mahangaiko ya kibidamu Sudan Kusini,wasiwasi kuhusu eneo la Catatumbo nchini Colombia,ambako raia wengi wameuawa na mapigano kati ya makundi yenye silaha,Siku ya Ukoma duniani,Siku ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari dhidi ya wahahudi,hitimisho la Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano na Msafara wa amani wa Chama cha Matendo Vijana Katoliki Italia ni mada za Papa mara baad ya Sala ya Malaika wa Bwana.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 26 Januari 2025, Baba Mtakatifu kwa kuwageukia umati wa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, alizindua kwa mara nyingine tena ombi la kukomesha mzozo nchini Sudan, ulioanza mnamo Aprili 2023, huku akisema unasababisha "mgogoro mkubwa zaidi wa kibinadamu ulimwenguni, na athari kubwa hata huko Sudan Kusini." Kwa njia hiyo alizikaribisha pande zinazozozana nchini Sudan kuacha mapigano na kuketi kwenye meza ya mazungumzo, akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono mazungumzo ya amani na kuwezesha misaada ya kibinadamu. "Niko karibu na watu wa nchi zote mbili na kuwaalika kwenye udugu, mshikamano, ili kuepuka aina zote za vurugu, na kutojiruhusu kudanganywa," alisema Papa.

Mapigano ya makundi ya silaha huko Colombia

Baba Mtakatifu aidha alielezea wasiwasi wake kuhusu hali katika eneo la Catatumbo nchini Colombia, ambako raia wengi wameuawa na mapigano kati ya makundi yenye silaha, ambayo yamewalazimu zaidi ya watu 30,000 kutoka makwao. "Ninaonesha ukaribu wangu kwao na kuomba," alisema.

Siku ya Ukoma Duniani

Papa Francisko  akiendelea alikumbuka Siku ya Ukoma Duniani, iliyoadhimishwa Dominika  tarehe 26 Januari. Papa alihimiza kila mtu kuunganisha wagonjwa na Ugonjwa wa Hansen katika jamii.

Mia 80 ya kumbukizi ya maangamizi ya Kiyahudi

Kabla ya Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya Maangamizi ya Wayahudi ifanyikayo kila mwaka ifikapo tateje 27 Janauri, Papa alikumbusha kuwa mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 80 tangu kukombolewa kwa kambi ya mateso ya Auschwitz. “Hofu ya kuangamizwa kwa mamilioni ya Wayahudi na watu wengine wa imani tofauti katika miaka hiyo haipaswi kamwe kusahauliwa au kukataliwa,” alisema, huku akikumbuka kielelezo cha mshairi ambaye ni  mzaliwa wa Hungaria,  Edith Bruck, anayeishi Roma. Papa alisema Wakristo wengi waliuawa pia katika kambi za kifo za Wanazi, “ambao miongoni mwao kulikuwa na wafiadini wengi. Ninatoa  ombi langu kwa upya  kwa kila mtu kufanya kazi pamoja ili kutokomeza janga la chuki dhidi ya Wayahudi, pamoja na kila aina ya ubaguzi na mateso ya kidini," alisema. "Kwa pamoja, tujenge ulimwengu wa kidugu zaidi, wa haki, tukiwaelimisha vijana kuwa na mioyo iliyo wazi kwa wote, katika roho ya udugu, msamaha na amani."

Salamu kwa wanajibilei wa Mawasiliano

Papa vile vile aliwasalimia wanataaluma wote wa vyombo vya habari waliofika Roma kushiriki katika Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano, iliyoanza tangu tarehe 24 Januari na  aliwahimiza waandishi wa habari "daima wawe wasimulizi wa matumaini."

Salamu kwa washiriki wa Msafara wa Amani

Papa Francisko aidha alimwalika kijana katika dirisha la Jumba la Kitume na kumpa kipaza sauti.  Awali ya yote aliwasalimu wale wote ambao, walikuwa wakiimba, nyimbo na nderemo, na ambao walikuwa ni wa Msafara na kufuka Njia ya Conciliazione hadi katika Uwanja wa Mtakatifu  Pietro. Ni mvulana kutoka Chama cha matendo ya vijana Katoliki aliyewakilisha, mamia ya washiriki katika  "Msafara wa Amani", na  ambaye alisoma kwa niaba ya wenzake wote nchini Italia kwa kutoa wito kwamba wao, kama watoto, wanawahutubia watu wazima. Ukubwa sio tu kwa umri lakini katika jukumu la hatima ya ulimwengu.” Kwa njia hiyo Papa Francisko aliwambia kuwa “Mkikusanyika pamoja tangu asubuhi ya leo, mmetafakari juu ya uwepo wa Yesu katika maisha yenu, mkiwashuhudia wenzenu  vizuri kwa kukaribisha na udugu. Na sasa hebu tuwasikilize watu hawa wazuri ambao wanataka kutuambia jambo fulani," alisema Papa na kumruhusu mwakilishi wao.

Kijana aliyesoma ujumbe kwa niaba ya wenzake
Kijana aliyesoma ujumbe kwa niaba ya wenzake   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)
Papa baada ya Angelus
26 Januari 2025, 16:30