Papa Francisko:tukumbuke tarehe ya ubatizo wetu kama siku ya kuzaliwa upya!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko alianza tafakari yake kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana katika Siku ambayo Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Ubatizo wa Bwana Yesu Kristo katika mikono ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji kwenye Mto Yordan na ikiwa ni siku ya kumalizika kwa kipindi cha Maadhimisho ya Siku kuu zote za Noeli na mwaka mpya Dominika tarehe 12 Januari 2025. Baba Mtakatifu akiwageukia waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican alisema: “Ndugu wapenda Kaka na dada, Dominika Njema! Siku kuu ya ubatizo wa Yesu ambayo leo tunaadhimisha inatufanya tufikirie mambo mengi, hata ubatizo wetu.”
Papa Francisko aliendelea kusema: “ Ni kwa watu wake ambao alikwenda kupokea ubatizo kwa ajili ya msamaha wa dhambi. Ninapenda kukumbuka wimbo wa liturujia ya leo ambapo Yesu anakwenda kubatizwa na Yohane na roho tupu na miguu peku.” Papa alirudia hilo. Na “Yesu alipopokea ubatizo, Roho ulijidhihirisha yenyewe na Epifania ya Mungu ilitokea, ambayo ilifunua uso wake ndani ya Mwana na kufanya sauti yake isikike akisema: "Wewe ni Mwanangu mpendwa;(Lk 3, 22). Uso na sauti. Ndizo “sifa mbili za kibinadamu ambazo Mungu anafanya kuwa zake.”
Papa Francisko alisema: “Kwanza kabisa uso. Katika kujidhihirisha kuwa Baba kwa njia ya Mwana, Mungu anaweka mahali pa pekee pa kuingia katika mazungumzo na ushirika na wanadamu. Ni uso wa Mwana mpendwa.”
Pili, sauti: "Wewe ni Mwanangu mpendwa" (Lk 3,22). Hii ni ishara nyingine inayoambatana na ufunuo wa Yesu.” Kwa njia hiyo Papa alisisitiza kuwa: “Wapendwa kaka na dada, siku kuu ya leo inatufanya kutafakari uso na sauti ya Mungu, ambayo inadhihirika katika ubinadamu wa Yesu. Je, ninahisi kupendwa na kusindikizwa na Mungu au nadhani Mungu yuko mbali nami? Na tumezoea kusikia sauti yake? Papa Francisko aliuliza maswali hayo na kuendelea.”
Papa aliendelea: “Ninawauliza swali: je, kila mmoja wetu anakumbuka tarehe ya Ubatizo wetu? Hii ni muhimu sana! Fikirieni: siku gani nilibatizwa? Na ikiwa hatukumbuki, basi tutakapofika nyumbani, tuulize wazazi au Wazazi wa Ubatizo tarehe ya Ubatizo.” Papa alisisitiza: “Na tusherehekee tarehe kama hii ya siku mpya ya kuzaliwa yaani ile ya kuzaliwa katika Roho wa Mungu. Msisahau. Hii ni kazi ya kufanya nyumbani, kutafuta tarehe yangu ya ubatizo. Tujikabidhi kwa Bikira Maria, tukiomba msaada wake. Na tusisahau tarehe ya Ubatizo!” Alihitimisha Papa Francisko.