杏MAP导航

Tafuta

2025.01.28 I vescovi indiani riuniti in plenaria 2025.01.28 I vescovi indiani riuniti in plenaria 

Papa Francisko kwa Maaskofu wa India:Kuishi kisinodi!

Papa Francisko ametuma ujumbe kwa washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini India waliokusanyika huko Orissa:Kusaidia Kanisa Mahalia,kuongeza matumaini ya safari ya kisinodi.Kusaidia makanisa mahalia kutekeleza matunda ya safari ya sinodi.Jubilei katika ishara zilizojitokeza katika Sinodi na changamoto za maisha ya Kikristo huo India.

Na Angella Rwezaula - Vatican.


Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe kwa washiriki wa Mkutano wa XXXVI Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini India (CCBI), ambao ni mkubwa wa kitaifa barani Asia na wa nne kuwa mkubwa kwa ngazi ya Ulimwengu, ambao unawakilisha majimbo 132 na maaskofu 209. Mkutano huo unafanyika katika Chuo Kikuu cha Jimbo Kuu la Cuttack-Bhubaneswar, katika serikali ya Orissa. Mkutano huo unaoongozwa na mada ya “Ishara ya Matumaini wakati wa Jubilei.” Katika ujumbe uliosomwa mwanzoni mwa Kazi na Askofu Mkuu George Antonysamy, Makamu Rais wa Baraza la Maaskofu CCBI, Baba Mtakatifu Francisko anawahakikisha msaada wake kwa maaskofu wa India ambao anawatia moyo kuongoza makanisa mahalia katika hali ya sasa kwenye maelekeza yanyaojikita kuanza na Sinodi.

Papa Francisko anasali ili maamuzi yao yanaweza kuwasaidia Makanisa mahalia na kutambua jinsi gani ilivyo bora kukamilisha matunda ya safari ya kisinodi na kuwahuisha waamini wengi katika miito yao ya kuwa mitume wa kimisionari. Akigusia Jubilei, inayoendelea, alisema kuwa Kanisa la India, linaendelea kuwa ishara ya matumaini kwa ajili ya taifa zima, kwa kutafuta kufungua daima milango yake wazi ili kupokea maskini na walio katika mazingira magumu na ili wote waweze kuwa na matumaini katika wakati ujao ulio bora.

Mada na uingiliaji kati


Kama ilivyoripotiwa na Baraza la Maaskofu lenyewe, kikao cha wajumbe wote kilifunguliwa kwa kuingilia kati Askofu Mkuu Leopoldo Girelli, Balozi wa Vatican nchini India na Nepal, ambaye pia aliongoza adhimisho kuu la Misa Takatifu. Askofu Mkuu John Barwa, S.V.D., kisha akawakaribisha maaskofu wote waliokuja kwa ajili ya tukio hilo huko Orissa, nchi ya "tamaduni hai za kikabila. "Katika hotuba yake, Kardinali Filipe Neri Ferrão, rais wa CCBI na Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Asia, aliakisi "changamoto zinazokua na muhimu kwa maisha ya Mkristo na uhuru wa kidini nchini India." Kadhalika aliakisi katika suala hili kupitishwa kwa sheria za kupinga uongofu wa kulazimisha katika majimbo 18 na kuongezeka kwa idadi ya matukio yaliyoripotiwa ya jeuri dhidi ya Wakristo. Alitoa wito wa mshikamano, sala na hatua za pamoja ili kudumisha utu na uhuru wa Kanisa: "Pamoja na hali ngumu, Kanisa nchini India bado liko hai na thabiti." Mojawapo ya mada zilizochaguliwa kwa ajili ya kutafakari ni "Kutambua njia za sinodi za utume.

Papa atuma ujumbe kwa maasakofu wa India

 

30 Januari 2025, 17:29