Papa Francisko:Je tunamtambua Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu na Mwokozi?
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko akitoa tafakari yake labla ya sala ya Malaika wa Bwana Dominika, kwa aliongozwa na kifungu cha Injili ya Luka ambacho kinachorejeea ziara ya Yesu kwenye sinagogi huko Nazareti. Papa alitaja wakati ambapo Yesu alijitangaza Mwenyewe utimizo wa unabii wa Isaya, tangazo ambalo liliwashangaza na kuwapa changamoto wasikilizaji Wake. Papa alieleza kwamba wakati huu aliwauliza wenyeji wenzake Yesu swali la kuamua: “Je, ni mtoto wa seremala tu ambaye anajivunia jukumu ambalo si lake, au yeye ndiye Masihi, aliyetumwa na Mungu kuokoa watu? kutoka katika dhambi na maovu yote?”
Papa alisema “Hebu wazia mshtuko na mshangao wa watu wa Nazareti, aliongeza, “Walifikiri kwamba wanamjua Yeye vizuri sana na hili, badala ya kuwezesha kufunguka kwa akili na mioyo yao, liliwazuia kufanya hivyo, kama pazia linalofunika nuru.” Hata leo hii, Papa alisema, kifungu hiki cha Injili kinawaalika waamini kukabiliana na ufahamu wao wenyewe wa Yesu. Tukio hili pia linatukia huku akibainisha kwamba sisi pia tunaweza kuanguka katika mtego wa kufikiri kwamba tayari tunamjua Yesu. Tumekua pamoja Naye, shuleni, parokiani, katika katekisimu, katika nchi yenye utamaduni wa Kikatoliki... Na hivyo kumuona kwetu kuwa yeye ni mtu ambaye yuko karibu sana.
Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu aliwahimiza Wakristo kujiuliza iwapo kweli wanamtambua Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu na Mwokozi. “Je, tunahisi mamlaka ya pekee ambayo Yesu wa Nazareti anazungumza nayo? Je, tunatambua kwamba Yeye ndiye mtangazaji wa tangazo la wokovu ambalo hakuna mtu mwingine anayeweza kutupa? Aliuliza Papa. Kwa kuhitimisha alitoa mwaliko kwetu sote kutafakari kuhusu hitaji letu la wokovu na akaeleza kwamba ni pale ambapo tunapokubali tu, ndipo mwaka huu unaweza kuwa Mwaka wa Neema. Na hivyo tutafute mwongozo kutoka kwa Maria, Mama wa Mungu. Tumgeukie kwa ujasiri Maria, Mama wa Mungu na Mama yetu, ili atusaidie kumtambua Yesu.”