Papa Francisko atakutana na mapadre wa Roma tarehe 6 Machi
Baba Mtakatifu anarudia kukutana na mapadre wake katika Kanisa kuu la Mtakatifu Yohane wa Laterano.Na utamaduni wa Alhamisi ya kwanza ya kipindi cha Kwaresima utapaishwa.
Vatican News
Baada ya kukutana na mapadre wa Jimbo kuu la Roma mwishoni mwa 2023 na miezi ya kwanza ya 2024, kutokana na baadhi ya mikutano iliyoandaliwa katika majimbo ya sekta mbalimbali za jiji la Roma, Baba Mtakatifu Francisko anarejea tena kukutana na mapadre wake wote Alhamisi tarehe 6 Machi 2025 katika Basilika ya Mtakatifu Yohane huko Laterano.
Jimbo la Roma lilitangaza hayo huku likisisitiza kwamba mapokeo ya kiutamaduni ya Alhamisi ya kwanza ya kipindi cha Kwaresima yanafanywa kwa upya.
Mkutano wa mwisho na mapadre wa jimbo, watawa na mashemasi wa kudumu katika huduma ya kichungaji ya jimbo la Roma ulifanyika kunako tarehe 13 Januari 2024.
31 Januari 2025, 18:08