杏MAP导航

Tafuta

2025.01.16 Papa akutana na  Walezi wa Jumuiya ya Chuo cha Mapadre wa Argentina Roma. 2025.01.16 Papa akutana na Walezi wa Jumuiya ya Chuo cha Mapadre wa Argentina Roma.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa akutana na Mapadre wa Chuo cha Argentina Roma:unyenyekevu na kushinda kiburi!

Papa Francisko alikutana na Jumuiya ya chuo cha kipadre cha Argentina cha Roma.Katika hotuba aliyoakabidhi ameeleza mfano wa Mtakatifu Brochero na kukabiliana na vita vikali vya Habari Njema:wito wa Padre ni kutunza maisha yetu ya ndani,kuchochea moto kuwaka,kwa unyenyekevu mkubwa,kulala chini kwa sababu "tukisimama"katika kiburi chetu tuko hatarini."

Na Angella Rwezaula – Vatican.      

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 16 Januari 2025, alikuta na, Jumuiya ya Chuo cha Kipadre cha Argentina cha Roma, katika Maktaba ya Jumba la Kitume mjini Vatican. Papa aliwakabidhi Mapadre na walezi hotuba iliyotayarishwa ambayo awali ya yote anabainisha  kwamba “Leo ninapaswa  kuwasindikiza katika adhimisho la Misa Takatifu na chakula cha jioni. Sihitaji kuwaambia kuwa bado nina hamu ya kula nyama choma. Lakini, kama mnavyojua, kuwa wachungaji inatuweka wakati mwingine mbele yetu na wakati mwingine nyuma, kulingana na mipango ya Yule Bwana wa maisha yetu. Kwa vyovyote vile, ili nisisahau harufu ya ardhi yetu, ningependa kutoa maoni yangu juu ya jambo ambalo nilisoma hivi majuzi kuhusu Cura Brochero na ambalo linaonekana kufaa sana kwenu, mnaoendelea kujitayarisha kukabiliana na vita vikali vya Injili.

Mfano wa Mtakatifu Brochero

Papa anakazia kusema kuwa Nitakachowambia juu yake kinarejea roho yake ya kikuhani, na jambo la kwanza, muhimu ni kauli iliyotolewa na marafiki zake kwamba "Brochero hawezi kuwa kitu chochote isipokuwa kuhani". (Kwa kifupi ni José Gabriel del Rosario Brochero, aliyeitwa Cura Gaucho au Cura Brochero (Mtakatifu wa Rosa de Río Primero, alizaliwa tarehe 16 Machi 1840 - Villa del Tránsito, na kifo chake tarehe 26 Januari 1914), alikuwa Padre wa Argentina; Alitangazwa kuwa Mwenyeheri tarehe 14 Septemba 2013 na kutangazwa kuwa Mtakatifu tarehe 16 Oktoba 2016 na Papa Francisko.)

Kwa njia hiyo Papa akifafanua anasema ni lazima tuchukue kwa uthabiti utambulisho huu wa kikuhani, kujipenyeza wenyewe na ukweli kwamba wito wetu si nyongeza, njia ya malengo mengine, hata kama ni wacha Mungu, kama vile kujiokoa. Sivyo kabisa. Wito ni mpango wa Mungu katika maisha yetu, kile ambacho Mungu anachokiona ndani yetu, kile kinachosongesha macho yake ya upendo, ningethubutu kusema kwamba kwa namna fulani ni upendo alionao kwetu na ni katika hili kwamba ndiyo mizizi ya asili yetu ya kweli.” Na hapa Mtakatifu Cura Brochero  anaelezea maana ya kukumbatia "kazi ya kikanisa" – Papa anaongeza  mnajua kwamba ni usemi ambao siupendi, lakini kwamba, Cura Brochero anavyoelewa, katika hamu yake ya kufa akikimbia kama farasi “chesche”, anakaribia sana na  Mtakatifu Paulo(rej. 2 Tim 4:7).

Kufanya kazi kwa manufaa ya wengine

Na anatuambia: "kufanya kazi kwa manufaa ya wengine hadi wakati wa mwisho wa maisha", zawadi kamili ya mtu mwenyewe, sadaka kwa Mungu katika ndugu kwa kutumia na kujitumia kwa ajili ya Injili. Wakati huo huo, "Kupambana - anaendelea mtakatifu - na maadui wa kiroho, kama puma wanaopigana wamelala chini wakati hawawezi kujilinda wakiwa wamesimama." Kwa hiyo ni, kutunza maisha yetu ya ndani, kuchochea moto kuwaka, kwa unyenyekevu mkubwa, kwani ni "kulala chini" kwa sababu "tukisimama" katika kiburi chetu sisi tuko  hatarini zaidi.

Udugu wa kikuhani

Ujumbe mwingine muhimu ni udugu wa makuhani. Kwanza kabisa na Askofu, ambaye [padre] anajiona kama askari rahisi, wa kuiga matendo ya mashujaa [wa nchi ya baba], wakipambana pamoja naye, bega kwa bega, hadi rangi ya mwisho. Na pamoja na ndugu zake mapadre anataka kuwashirikisha yote aliyo nayo, anawaalika wamrekebishe kwa kujiamini na anafanya hivyo nao kwa unyoofu, akiwataka waishi maisha ya uchaji Mungu, kwa kuungama mara kwa mara “kwa mtu mmoja na kwa pamoja na  mwingine, kushiriki maisha yote, ya kimwili na ya kiroho na ya kitume."

Hatimaye, Papa anabainisha kuwa jinsi gani inawezaje kuwa vinginevyo, ile ya Ekaristi. Pamoja na kwamba  kazi yake ilikuwa ngumu, Brochero akupuuza kamwe, akitumia sehemu kubwa ya usiku kwenye uwanja wa wazi, kati ya mashamba ya mahindi, huku akingojea kwenye banda, na kuamka - kwa sababu hakuona kuwa inafaa kusumbua 'alfajiri ili  kuwa na uwezo wa kuingia kuadhimisha. Hiyo ilitoa heshima kwa fumbo ambalo, mbali na kuwekewa, lilipenya zaidi ya maneno elfu ya ufasaha wa kufumba. Kwa kuhitimisha Papa anasema kuwa Na Yesu awabariki na Bikira Mtakatifu awalinde. Na, mbele za Bwana juu ya altare  wasisahau kumuombea.

Papa na Mapadre wa Argentina
16 Januari 2025, 15:57