杏MAP导航

Tafuta

Mazishi ya Askofu Mkuu Anastasios wa Tirana nchini Albania. Mazishi ya Askofu Mkuu Anastasios wa Tirana nchini Albania.  (AFP or licensors)

Katika rambi rambi za Papa anakumbuka huduma ya bidii ya kichungaji ya marehemu Askofu Mkuu Anastas

Katika ujumbe wake kwa Kanisa la Kiorthodoksi la Albania,Baba Mtakatifu Francisko anatoa salamu za rambirambi kufuatia kuondokewa na Askofu Mkuu Anastas wa Tirana,Durr?s na Albania yote na kutoa heshima kwa kujitolea kwake bila kuyumbayumba kwa imani na kujitolea kwake kichungaji.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko alituma salamu za rambi rambi kwa Kanisa la Kiorthodox la Albania kuafuatia na kifo cha Askofu Mkuu Anastas. Katika salamu hizo anabainisha kuwa “kwa kupokea habari za kifo cha Anastas, Askofu Mkuu wa Tirana, Durrës na Albania yote,” anaelezea “rambi rambi kwake na Wajumbe wote wa Sinodi Takatifu na mapadre, wamonaki na waamini wapendwa wa Kanisa la Albania, pamoja uhakika wa sala zake kwa sababu Mungu, Baba Yetu wa huruma, aweze kumjalia, zawadi ya kazi yake.”

“Imani ya Jumuiya ya kiorthodox nchini Albania kwa hakika imekiti mzizizi katika maisha ya Mpendwa kaka Yetu ambaye alikuwa makini katika huduma ya kichungaji na alisaidia watu kugundua upya utajiri na uzuri baada ya miaka mingi ya ukana Mungu uliowekwa na Serikali na kulitesa Kanisa.” Katika mtazamo huo, Papa Francisko anakumbuka “Mkutano wake na Mkuu huyo katika fursa ya Ziara yake ya kwanza ya Kitume nje ya Italia, ambaye alimkumbatia kidugu na kwa maneno yake waliyobadilishana katika fursa hiyo.”

Baba Mtakatifu anaandika kuwa “Wakati wa maisha yake marefu, na huduma yake kama kuhani na kama askofu, daima alionesha kujikita kwa kina katika Injili alihudumu na kutangaza Bwana katika miktadha yote ya kijiografia na kiutamaduni, huko Ugiriki Afrika na Albania. Alifanya hivyo kwa kufuata mfano wa Mtakatifu Paulo, ambaye alijitoa sana kwa Kristo hata angeweza kusema, “Nimekuwa mambo yote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa angalau mmojawapo”(1Kor 9:22).”

Akichukua jukumu la kuongoza Kanisa la Kiorthodox la Albania, Papa anaongeza kuandika “ alitaka kupenya ndani kabisa ya mioyo ya wale waliokabidhiwa uangalizi wake, hasa katika mila na utambulisho wao, bila kupoteza kamwe ushirika na Makanisa mengine ya Kiorthodoksi. Wakati huo huo, alijihusisha pia kwa nia njema katika mazungumzo na kuhimiza kuishi pamoja kwa amani na Makanisa na dini nyingine. Alipofika Albania, makasisi fulani walimkaribisha kwa salamu ya Pasaka katika Kigiriki, “Christos Anesti!” Alijibu kwa Kialbania, akionyesha tamaa yake kubwa ya kuishi pamoja na watu wake na kutoa ushahidi juu ya upendo wa Mungu, ambao unashinda giza na uonevu wote, kati ya wale walioteseka sana. Kwa kuwa sasa maisha yake ya hapa duniani yamefikia kikomo, ninaomba kwamba, kwa huruma zake Mungu Baba Mwenyezi, Heri yake iweze kuusifu Utatu Mtakatifu milele, pamoja na waungamaji wote wa imani na wachungaji ambao wamelitangaza neno. ya wokovu kwa watu kila mahali na wakati wowote.

Papa atuma rambi rambi Albania
30 Januari 2025, 17:31