杏MAP导航

Tafuta

Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo yananogeshwa na kauli mbiu “Mahujaji wa Matumaini.” Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 11 Januari 2025 amezindua mzunguko wa Katekesi kama sehemu ya maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo. Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo yananogeshwa na kauli mbiu “Mahujaji wa Matumaini.” Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 11 Januari 2025 amezindua mzunguko wa Katekesi kama sehemu ya maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo.  (ANSA)

Katekesi Kuhusu Mwaka wa Jubilei: Yohane Mbatizaji Nabii wa Matumaini

Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo yananogeshwa na kauli mbiu “Mahujaji wa Matumaini.” Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 11 Januari 2025 amezindua mzunguko wa Katekesi kama sehemu ya maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo. Lengo ni kuweza kukutana na waamini pamoja na mahujaji kutoka sehemu mbalimbali za dunia, wanaopania kuanza upya kwa kukita maisha yao kwa Mwenyezi Mungu. Kuanza Upya Katika Mungu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Katika Kanisa Katoliki maadhimisho ya Jubilei ni mwaka wa toba na maondoleo ya dhambi; upatanisho, na wongofu wa ndani unaojikita katika Sakramenti ya Kitubio. Jubilei ni mwaka wa Kristo Yesu. Katika Agano Jipya, Kristo Yesu anajionesha kuwa ndiye utimilifu wa nyakati akisema “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenipaka mafuta niwahubirie maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafunga kufunguliwa, vipofu kuona tena, kuwaletea wafungwa uhuru, na kutangaza mwaka uliokubalika kwa Bwana.” Lk 4:18-19. Kumbe maadhimisho ya Jubilei yanaitwa kwa haki kuwa ni maadhimisho ya “Mwaka Mtakatifu” kwa sababu unasimikwa katika Liturujia ya Kanisa inayowajenga kila siku wale waliomo katika Kanisa wawe Hekalu la Roho Mtakatifu, Makao ya Mungu katika Roho, mpaka kuufikia utimilifu wa Kristo. Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo yananogeshwa na kauli mbiu “Mahujaji wa Matumaini.” Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 11 Januari 2025 amezindua mzunguko wa Katekesi kama sehemu ya maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo. Lengo ni kuweza kukutana na waamini pamoja na mahujaji kutoka sehemu mbalimbali za dunia, wanaopania kuanza upya kwa kukita maisha yao kwa Mwenyezi Mungu.

Matumaini ni fadhila ya Kimungu
Matumaini ni fadhila ya Kimungu   (ANSA)

Mababa wa Kanisa wanasema, Matumaini ni fadhila ya Kimungu inayowawezesha waamini kutamani heri ya Ufalme wa mbinguni na uzima wa milele kwa kutumainia ahadi za Kristo Yesu na kutegemea, siyo nguvu zao wenyewe, bali msaada wa neema ya Roho Mtakatifu kwa sababu Mwenyezi Mungu daima ni mwaminifu katika utekelezaji wa ahadi zake. Kwa njia ya Fumbo la Utatu Mtakatifu, waamini wanaweza kuhesabiwa haki kwa neema yake ili wapate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama tumaini lao. Fadhila ya matumaini inajibu tamaa ya heri ilivyowekwa na Mungu katika moyo wa kila mtu. Yachota matumaini yanayovuvia matendo ya watu. Huyatakasa ili kuyapanga kwa ajili ya Ufalme wa mbinguni nyakati za upweke. Hufungua moyo katika kungoja heri ya milele. Akielekezwa na matumaini anakingwa na ubinafsi na anaongozwa kwenye furaha itokanayo na mapendo.

Jubilei: Mahujaji wa matumaini
Jubilei: Mahujaji wa matumaini   (ANSA)

Matumaini ya Kikristo yanakita mizizi yake katika Heri za Mlimani ambazo kimsingi ni muhtasari wa mafundisho makuu ya Kristo Yesu kwa wanafunzi wake. Matumaini ni “nanga ya roho”, hakika na thabiti; ni silaha inayowalinda waamini katika mapambano ya wokovu. Matumaini ni fadhila ya Kikristo inayojikita katika unyenyekevu na nguvu ya kuweza kusonga mbele katika safari ya maisha, licha ya vikwazo na magumu yaliyopo. Matumaini kwa Mwenyezi Mungu kamwe hayawezi kumdanganya mwamini kwani Mwenyezi Mungu daima ni mwaminifu katika kutekeleza ahadi zake. Mungu ni chemchemi ya furaha na amani mioyoni mwa waja wake. Rej. KKK 1817-1821. Baba Mtakatifu anawaalika waamini kumwomba Mwenyezi Mungu fadhila na zawadi ya matumaini ili kuanza tena upya hija ya maisha. Yohane Mbatizaji ni Nabii aliyefunga Agano la Kale, akawa daraja ya Agano Jipya, aliyemwandalia njia na hatimaye, wakati ulipowadia akamtambulisha Kristo Yesu kuwa ni Masiha, Mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi za ulimwengu. Mtakatifu Yohane Mbatizaji alihubiri juu ya uwepo wa Masiha ambaye atajifunua kwao. Yohane Mbatizaji akawataka watu kutubu na kumwongokea Mwenyezi Mungu na hivyo, kuanza kutembea katika mwanga wa matumaini ya maisha mapya kama njia makini ya kuweza kumpokea Masiha wa Bwana, atakayetambulika kwa uwepo wa Roho Mtakatifu juu yake na huyu ndiye atakayebatiza kwa Roho Mtakatifu. Wakati ulipotimia Yesu akajitokeza hadharani kando ya Mto Yordani, baada ya kukaa nyumbani kwao mjini Nazareti kwa muda wa miaka thelathini, ili aweze kubatizwa. Baada ya kubatizwa, Roho Mtakatifu akamshukia Kristo Yesu na mara sauti kutoka mbinguni ikasikika ikisema, “Huyu ni Mwana wangu niliyependezwa naye”, Mt 3:17 alama ambayo Yohane Mbatizaji alikuwa akiisubiria na kwamba, Kristo Yesu ni Masiha wa Bwana.

Yohane Mbatizaji alikuwa ni Nabii wa Matumaini
Yohane Mbatizaji alikuwa ni Nabii wa Matumaini   (Vatican Media)

Kristo Yesu akajionesha kuwa ndiye Mwana kondoo wa Mungu anayeichukua na kuondoa dhambi ya ulimwengu. Yohane Mbatizaji ndiye aliyemtambulisha kuwa Kristo Yesu ndiye Mwana kondoo wa Mungu na wale wanafunzi wa kwanza wa Yohane Mbatizaji wakawa ni wafuasi wa kwanza wa Yesu! Baba Mtakatifu Francisko anasema, kwa hakika Yohane Mbatizaji ni Nabii wa Matumaini. “Nami nawaambia, Katika wale waliozaliwa na wanawake hakuna aliye mkuu kuliko Yohane; lakini aliye mdogo katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko yeye.” Lk 7:28. Watu wengi walimwendea Yohane Mbatizaji, wakitaka kuanza upya safari ya maisha yao. Hari na mwamko huu, uwasaidie waamini katika maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 kuanza upya. Yohane Mbatizaji awasaidie waamini kuwafungulia lango la matumaini kama ilivyokuwa kwa wana wa Israeli, waliotamani kuanza upya. Huu ni uzoefu wa mchakato wa matumaini unaopania kuwahamasisha watu waanze upya. Haya ni maneno yaliyotolewa na Kristo Yesu wakati ambapo Yohane Mbatizaji alipokuwa kifungoni na kwamba, hata leo hii kuna akina Herode wanataka kuliangamiza Kanisa. Baba Mtakatifu Francisko anawauliza waamini na mahujaji ikiwa kama nyuma yao kuna shauku ya kutaka kuanza upya safari ya maisha.

Waamini wawe tayari kujikita katika mchakato wa upya wa maisha
Waamini wawe tayari kujikita katika mchakato wa upya wa maisha   (ANSA)

Baba Mtakatifu anakaza kusema, kuna haja ya kuomba fadhila ya matumaini kwa ajili ya kuganga na kutibu madhara ya uharibifu wa mazingira nyumba ya wote; matumaini kwa watu waliovunjika na kupondeka moyo; watu ambao “wamegeuziwa kisogo.” Yaani “Watu wa Mungu waonje na kutambua ukuu wa Mungu katika maisha yanayong’ara katika Kristo Yesu, na hatimaye, awabidiishe katika huduma na upendo wa udugu wa kibinadamu kwa kutambua kwamba, wao bado ni wadogo. Wajenge utamadui wa kuwatambua wadogo na kuwasikiliza, tayari kuanza upya.

Mahujaji wa Matumaini
11 Januari 2025, 15:42