Papa Francisko aonesha huzuni kufuatia Ajali ya Ndege huko Washington
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 30 Januari 2025, katika telegramu aliyoituma kwa Rais wa Marekani, Donald Trump alionesha "ukaribu wake wa kiroho" kwa wale walioathiriwa na ajali iliyotokea huko Washington, kwenye Mto Potomac, karibu na Uwanja wa Ndege wa Ronald Reagan kati ya helikopta ya kijeshi, ikiwa na askari watatu, na ndege ya kibiashara iliyokuwa na abiria 60 na wafanyakazi 4, ambazo ziligongana kwa sababu ambazo bado hazijawekwa wazi na zote mbili zilianguka.
Waokoaji waliojishughulisha na uokoaji wa miili hiyo hawakuelezea kama wangepata manusura na waliripoti kuwa hali ya kazi ni ngumu sana na huenda itachukua siku kadhaa. “Nikizikabidhi roho za marehemu kwa rehema na upendo za Mwenyezi Mungu, ninatoa rambirambi zangu nyingi kwa familia ambazo sasa zinaomboleza kifo cha mpendwa wao,” aliandika Papa Francisko, ambaye alihakikishia sala zake “pia kwa wale waliohusika katika jitihada,”huku aliliombea taifa zima baraka za Mwenyezi Mungu na faraja na nguvu.”