Dibaji ya Papa,katika kitabu cha Kopp chenye kichwa:‘Urithi wa Kikristo,Iraq’:Nawakumbuka katika sala
Dibaji ya Papa Francisko
Kwa shukurani ya kumbukumbu ya ziara yangu ya kitume nchini Iraq ambaye licha ya janga la Uviko, na mashaka ya usalama, nilitimiza ziara hiyo kunako Machi 2021 ili kueleza kwa wakristo na watu wote wenye mapenzi mema katika Nchi hiyo upendo wangu na mshikamano wangu. Nchi hiyo inachukua nafasi daima na kila wakati katika moyo wangu katika sala. Licha ya matatizo mengi ambayo Iraq inakabiliana nayo, ninatazama Nchi hiyo kwa matumaini, kwa sababu inayo nguvu maalum. Nguvu hiyo awali ya yote ni watu hao hao nchini Iraq, wale wote wanaoshiriki ujenzi wa jamii ya raia, ambao wanahamasisha demokrasia katika Nchi na ambao wanajibidisha kwa ajili ya mazungumzo ya wazi na ya kweli kati ya dini. Kwa njia hiyo, ziara yangu kwa Mkuu Ayatollah wa Najaf, Sayyid Ali Al-Sistani ilikuwa muhimu na ya maana. Mkutano ule ulikuwa unataka kuwa alama kwa ulimwengu wote kwamba : kufanya vurugu katika jina la dini ni matumizi mabaya ya dini.
Kama watu wa dini tunawajibika kuelekeza amani na lazima kuiishi, kufundisha na kueneza amani hii. Katika muktadha huo ninafikiri hata ziara yangu huko Ur, kusini mwa Iraq, kwa maana kama wawakilishi wa dini mbali mbali, tulizungumza na kusali pamoja, chini ya maelfu na maelefu ya nyota zilizotazamwa na baba yetu Ibrahimu alipoinua macho yake angani. Urithi wa utajiri katika historia ya bimillenaria del cristianesimo kisayansi karibu haijavumbuliwa. Ninafikiri shule za kiteknolojia za wakristo wa kwanza wa Mesopotamia , uwepo wa amani kwa mamia ya miaka kati ya wakristo na waislamu kati ya Eufrate na Tigri na tamaduni mbali mbali za ibada ya kikatoliki katika kanda, mapambano kati ya madhehebu ya kikristo, katika nyakati za mateso mwanzoni mwa karne ya XX na visasi vingine vya kisiasa na kwa mwendelezo wa uwepo wa Kikristo hadi sasa. Haya yote yanapendeza kwamba katika kazi ya Matthias Kopp, urithi huu na historia hiyo inakuja kuonesha katika muktadha wao mafunzo ya kidini, katika wingi na kwa kuzingatia fasihi nzito.
Mwandishi kwa namna ya pekee anaweka umakini katika jitihada za kikanisa nchini Iraq na katika shughuli za Vatican, kwa wawakilishi wake wa kidiplomasia, ambao wanamulika uhasishaji mwingi wa Mapapa kwa ajili ya Iraq na wakristo wanaoishi ndani mwake. Kwa njia hiyo imezaliwa zawadi kama anavyoandika mwandishi mwenyewe, kwa wakristo nchini Iraq, ambao ninawatia moyo kujihusisha kwa kina zaidi utajiri wao mkubwa wa kihistoria na kudumisha uhai wa urithi wao: kwa wakati ujao ambao hata leo hii unahatarishwa kwa sababu ya uhamiaji na ukosefu wa uhakika kisiasa. Ninataka kueleza kwa kina na kuamini kwamba haiwezekani kufikiria Iraq bila wakristo, kwa sababu pamoja na waamini wengine wote wanawakilisha kwa nguvu utambuzi maalum wa Nchi, ambao tangu karne za kwanza pamekuwa ni mahali pa kuishi, kuvumiliana na kukubalina wao kwa wao. Kwa hiyo Iraq inaweza na kwa watu wake kuonekana, katika Mashariki ya Kati na katika Ulimwengu kwamba inawezakana kuishi pamoja kwa amani licha ya tofauti zao. (Hotuba ya Papa kwa wawakilishi wa Makanisa ya Kikiristo Iraq 28 Februari 2022).