Papa akutana na Waziri Mkuu wa Lebanon
Najib Mikati akutana na Baba Mtakatifu Francisko katika Jumba la Kitume mjini Vatican Ijumaa tarehe 13 Desemba 2024.Mazungumzo ya faragha ya dakika 20,yakifuatiwa na kubadilishana zawadi:Kutoka kwa Papa amempatia Ujumbe wa Siku ya Amani ya Dunia kwa Kiarabu mwaka huu,ulitiwa saini katika hafla hiyo.
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 13 Desemba 2024 alikutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Lebanon, Najib Mikati, katika Jumba la Kitume mjini Vatican pamoja na ujumbe wake, mkutano ulidumu kwa dakika 20. Mazungumzo ya faragha kati ya viongozi hao wawili yalifanyika katika Ukumbi wa Maktaba ya Jumba la Kitume kuanzia saa 3.35 hadi 3.55, ikifuatiwa na kubadilishana zawadi za kiutamaduni.
Mazungumzo kati ya vizazi
Katika zawadi hiyo, Papa alimpatia Waziri Mkuu mchongo wa shaba unaoitwa mazungumzo kati ya vizazi pamoja na nyaraka mbalimbali za Papa na Ujumbe wa Siku ya Amani Duniani kwa Kiarabu 2024, ambao alitia saini katika hafla hiyo. Waziri Mikati alijibu kwa zaidi inayoonesha Kuzaliwa kwa Yesu iliyoundwa na Padre kutoka Chuo Kikuu cha Antonine.
13 Desemba 2024, 16:28