Katika katekesi ya Papa kuhusu ari ya kitume,Bakhita anafundisha kusamehe
Na Angella Rwezaula,- Vatican.
Katika mwendelezo wa Katekesi kuhusu ari ya kitume, Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 11 Oktoba 2023 kwa waamini na mahujaji wengi waliofika kutoka pande za dunia, katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Mjini Vatican, amejikita kutazama sura ya mtakatifu mwingine. Kwa njia hiyo akianza amesema, katika mchakato wa safari ya katekesi kuhusu ari ya kitume ambayo tunatafakari, leo hii tuongozwe na ushuhuda wa Matakatifu Josephina Bakhita, Mtakatifu wa Sudan. Kwa bahati mbaya ni mezi kadhaa, Sudan imepasuliwa na migogoro isiyosemekana ya silaha ambayo leo hii inazungumziwa kidogo; Tuombee watu wa Sudan, kwa sababu waweze kuishi kwa amani! Lakini, umaarufu wa Mtakatifu Bakhita ulishinda kila mipaka na kufikia wote wanaokataliwa utambulisho wao na hadhi.
Baba Mtakatifu amesema kuwa, alizaliwa huko Darfur–na ambayo imepigwa Darfur! – kunako 1869, na alitekwa nyara kutoka familia yake akiwa na umri wa miaka saba na kufanywa mtumwa. Watekaji nyara wake walikuwa wakimwita “Bakhita”, maana yake “fortunata” yaani bahati. Yeye alipitia kwenye mikono ya mabwana nane, waliokuwa wanamuuza mmoja kwa mwingine… Mateso ya kimwili na kiakili ambayo alikuwa mwathirika tangu akiwa mdogo yalimwacha bila kuwa na utambulisho. Alipata ukatili na vurugu: kwenye mwili wake alikuwa na makovu zaidi ya miamoja. Lakini Yeye mwenyewe alishuhudia kuwa: “Nikiwa mtumwa sikukata tamaa kamwe, kwa kuwa nilikuwa nikihisi nguvu za ajabu ambazo zilinisaidia.”
Baba Mtakatifu ameongeza kusema kuwa mbele ya hayo ninajiuliza: Je Siri ya Mtakatifu Bakhita ni ipi? Tunajua mara nyingi mtu aliyejeruhiwa anajeruhi mara nyingine tena; Aliyedhulumiwa anakuwa mdhalimu kwa urahisi. Badala yake, wito wa wanyonge ni kujikomboa wao wenyewe na watesi wao kwa kuwa warejeshaji wa ubinadamu. Ni katika udhaifu wa walioonewa tu ndipo nguvu ya upendo wa Mungu unaowakomboa wote wawili hufunuliwa. Mtakatifu Bakhita anaeleza ukweli huu vizuri sana. Siku moja mlezi wake alimpatia msalaba mdogo, na yeye, ambaye hakuwahi kumiliki chochote, aliuweka kama hazina yenye wivu. Kwa kuutazama, alipata ukombozi au uhuru wa ndani kwa sababu alihisi kueleweka na kupendwa na kwa hiyo alikuwa na uwezo wa kuelewa na kupenda: huu ndiyo mwanzo, Papa amesisitiza.
Yeye alihisi kueleweka, alihisi kupendwa na hapo akawa na uwezo wa kuelewa na kupenda wengine. Kwa hakika Yeye mwenyewe atasema: "Upendo wa Mungu daima umenisindikiza kwa njia ya siri ... Bwana alinipenda sana: lazima tupende kila mtu ... Lazima tuwe na huruma!". Hii ndiyo nafsi ya Bakhita. Hakika, kuhurumia kunamaanisha mateso pamoja na waathriwa wa ukatili mwingi waliopo ulimwenguni na pia kuwahurumia wale wanaofanya makosa na dhuluma, sio kwa kuhalalisha, lakini kwa sababu ya ubinadamu.
Papa ameongeza kusema kwamba hii ni bembelezo, kwamba yeye anatufundisha, ubinadamu. Tunapoingia kwenye mantiki ya mapambano, ya mgawanyiko kati yetu, ya hisia mbaya, mmoja dhidi ya mwingine, tunapoteza ubinadamu. Na mara nyingi tunafikiri kwamba tunahitaji ubinadamu, kuwa binadamu zaidi. Ubinadamu zaidi. Na hii ndiyo kazi ambayo Mtakatifu Bakhita anatufundisha: kufanya ubinadamu, kujifanya kuwa binadamu na kuwafanya wengine kuwa binadamu, Papa amekazia. Baba Mtakatifu akiendelea amesisitiza kuwa Bakhita, aligeuka kuwa mkristo, akabadilishwa na maneno ya Kristo ambayo alikuwa anatafakari kila siku: “Baba, wasamehe, kwa maana hawajui watendalo” (Luka 23:34). Ndiyo maana alisema: “Kama Yuda angemwomba Yesu msamaha yeye pia angepata huruma au kusamehewa”. Tunaweza kusema kwamba maisha ya Mtakatifu Bakhita yamekuwa mfano halisi wa msamaha.
Ni vizuri sana kusema juu ya mtu, "alikuwa na uwezo, aliweza kusamehe". Kila mara. Na siku zote aliweza kufanya hivyo kiukweli: maisha yake ni mfano wa msamaha. Kusamehe maana hapo tutasamehewa. Papa ameomba tusisahau hili kwamba: msamaha, ambao ni mahangaiko ya Mungu kwetu sote. Na kwa ajili yake, msamaha ulimweka huru. Msamaha aulipokea kwanza kupitia upendo wa huruma wa Mungu na kisha msamaha kutolewa na hii ilimfanya kuwa mwanamke huru, mwenye furaha, mwenye uwezo wa kupenda. Bakhita aliweza kupata huduma si kama utumwa, lakini kama ishara ya kujitolea bure. Na hii ni muhimu sana: alifanywa mtumwa kwa hiari, aliuzwa kama mtumwa, lakini basi alichagua kwa hiari kuwa mtumishi, kubeba mizigo ya wengine mabegani mwake.
Mtakatifu Josephine Bakhita, kwa mfano wake, anatuonesha njia hatimaye ya kuwa huru kutoka katika utumwa na hofu zetu. Anatusaidia kufichua unafiki na ubinafsi wetu, kushinda chuki na migogoro. Na daima anatutia moyo. Papa ameongeza kusema kuwa, msamaha hauondoi chochote bali unaongeza, lakini msamaha unaongeza nini?, heshima: msamaha hauondoi chochote kutoka kwako, lakini unakuongeza heshima kwa mtu, hutufanya tujiangalie kwa wengine, tuwaone kuwa dhaifu kama sisi, lakini daima ni kaka na dada katika Bwana. Kwa hiyo msamaha ni chemchemi ya ari inayogeuka kuwa huruma na wito kwa utakatifu mnyenyekevu na wa furaha, kama ule wa Mtakatifu Bakhita.