Papa ameikumbatia Mongolia katika ziara ya 43 ya kitume
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Ulikuwa ni upepo mwanana uliomkinga na joto kali ambao ulimkaribisha Baba Mtakatifu Francisko Jijini Ulaanbaatar, mji mkuu wa Mongolia ambapo Papa alitua saa 3.51 asubuhi (saa za huko) ambapo atakuwa huko hadi tarehe 4 Septemba 2023 , katika ziara yake ya 43 ya kitume ya Upapa wake. Na kama ilivyotajwa tayari katika siku za hivi karibuni na kama ilivyorudiwa na radio na televisheni za nje na ndani ambazo zinasisitiza hali ya kihistoria ya ziara hiyo, kwa hakika ni ziara ya kwanza ya Papa katika nchi hiyo ya Asia ya Kati.
Habari kutoka vyombo vya habari vinaendelea na mzunguko unaongeza udadisi wa kujua sehemu isiyo ya Kikatoliki ya idadi ya watu, kwa hiyo wengi, hasa ni Wabuddha wa Tibet, kwa kuwasilisha tabia maarufu katika ulimwengu wote. Kwa mujibu wa wawakilishi wetu wa habari Vatican, ambao tayari wako huko wanatujulisha kuwa katika mitaa ya jiji ni vigumu kupata mabango mengi kama tulivyozea kuona katika kila ziara za kimataifa za Papa, mbali na kuona umati wa watu.
Hii ni kwa sababu ni makaribisho ya kiasi yaliyotengwa kwa ajili ya Papa lakini yenye hisia za dhati, na hali ya shukrani hasa kwa upande wa kundi dogo la Kikatoliki. Furaha yao kubwa kwa mujibu wa Wamisionari wa Consolata wamesema “ndivyo hivyo kama inavyotokea kwa jamaa yako mpendwa ambaye unajua yuko karibu kutembelea nyumbani kwako.” Kwa hiyo hata katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chinggis Khan, ukimya ulionekana kutawala juu ya kuwasili kwa Papa, kama kile ambacho Papa mwenyewe aliwaalika kutafakari wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari wakati watoka Roma. Na maneno ambayo Kadinali Giorgio Marengo, Msimamizi wa kitume wa Ulaanbaatar, akiwa mstari wa mbele aliwakaribisha kwenye uwanja wa ndege na kutoa shukrani.
Karibu saa 4.00 asubuhi, Shirika la Ndege ya ITA A330 ilitua kwenye Uwanja wa Ndege ambapo Wawakilishi wa Baraza la Kitume, Askofu Mkuu Fernando Duarte Barros Reis, na mkuu wa itifaki walipanda ndege kutoka ngazi ya mbele kumsalimia Baba Mtakatifu, ambaye baadaye alishuka kwa lift. Chini ya ngazi ya mbele, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Bibi Batmunkh Battsetseg, alimngojea Papa. Kwa kawaida Nchini Mongolia ni ofisi hiyo daima ambayo hukaribisha wakuu wa nchi za kigeni.
Mwanamke mwingine, msichana aliyevalia deel nyekundu (hilo ni vazi la kitaifa la hariri na pamba), alimpatia Papa kikombe cha mtindi kavu, ambayo ni sahani ya kiutamaduni ya kienyeji na ladha ya siki iliyotengenezwa na maziwa yake, kutoka kwa wanyama wa kawaida pamoja na ng'ombe, mbuzi na farasi. Papa aligusa kikombe kwa mkono wake na kisha akachukua kipande. Hakukuwa na hotuba, lakini Kikundi cha Walinzi walitoa Heshima na askari waliovalia sare za jadi nyekundu, bluu na manjano (rangi za bendera ya Kimongolia) na salamu za wajumbe husika. Pia alikuwepo Askofu José Luis Mumbiela Sierra, askofu wa Jimbo la Utatu Mtakatifu huko Almaty, kama rais wa Baraza la Maaskofu la Asia ya Kati.
Papa Francisko na waziri huyo walikwenda kwenye Sebule ya Watu Mashuhuri (VIP )kwa mazungumzo mafupi. Mwishoni, Papa Fransisko alipokelewa na kuhamishwa kwa gari hadi Ubalozi wa Vatican huko Ulaanbaatar, kusini mwa jiji, katika wilaya ya Khan Uul, mojawapo ya maeneo makuu ya viwanda katika eneo hilo. Katika jengo hilo la orofa nne la matofali, ambapo bendera ya bluu ya kumkaribisha ilibandikwa katika siku za hivi karibuni, ikiwa pamoja na ile ya kipapa, ambapo Baba Mtakatifu atakaa wakati wa siku hizi za ziara yake na atabaki katika mji mkuu huu Ulaanbaatar. Kama ilivyopangwa, sherehe rasmi ya kumkaribisha zitafanyika asubuhi, Jumamosi tarehe 2 Septemba 2023, katika eneo la Uwanja wa Sukhbaatar ambapo ni Ikulu ya Serikali na mkutano na mamlaka ya kiraia utafanyika ikiwa ndiyo hatua ya kwanza ya Ziara yake ya Baba Mtakatifu Francisko. Wakati huohuo, baada ya kufika katika Nchi hiyo Papa alikaribishwa na kundi la wazee na wagonjwa, kisha baadhi ya watoto wakamsalimia mlangoni na kumzawadia maua.
Telegramu kwa mamlaka za nchi zimefurika
Wakati wa safari ya takriban masaa 9 na nusu kwa ndege, Papa Francisko, pamoja na ile iliyoelekezwa kwa Rais wa Jamhuri ya Italia Sergio Mattarella, alituma telegramu kwa nchi zingine alizopita juu yake wakati wa safari. Katika ujumbe uliotumwa kwa rais wa Kroatia, Zoran Milanovi? alikumbuka ziara yake ya hivi karibuni mjini Vatikani (mnamo 2021) akitoa baraka tele kwa taifa, pamoja na zawadi ya amani na furaha. Kwa mujibu wa msemaji wa rais wa Bosnia na Herzegovina, Zeljmko Kom?i?, Papa aliwahakikisha maombi yake na kuomba baraka kuu za umoja, udugu na maelewano juu ya taifa. Maombi ya amani na umoja wa taifa pia yalioneshwa katika telegramu iliyoelekezwa kwa rais wa Serbia Aleksandar Vu?i?, na amani na ustawi alimtakia rais wa Montenegro, Jakov Milatovi?. Tena, zawadi ya umoja, furaha na amani zimeambatana na baraka za upapa kwa ajili ya Bulgaria kupitia telegramu kwa Rais Rumen Radev. Katika ujumbe wake kwa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdo?an na kwa watu wote, Papa Francisko aliwahakikishia maombi yake, huku akitoa baraka za Mungu kwa ajili ya maelewano ya kidugu na amani juu ya taifa.