Papa Francisko: usipoteze wakati chochea ndoto ya wema!
Na Angella Rwezaula- Vatican.
Katika Dominika ya 17 ya Mwaka A wa Kanisa tarehe 30 Julai 2023, Baba Mtakatifu Francisko ametoa tafakari yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,mjini Vatican, siku chache kabisa kabla ya Baba Mtakatifu Francisko kuelekea huko Lisbon katika Siku ya Vijana Duniani 2023 ambao wanamsubiri kwa shuku kubwa. Akianza kutafakari jii ya Injili ya Siku ambayo Yesu anatoa mifano kuhusu Ufalme wa Mungu, alisema “Leo Injili inasimulia mfano wa mfanyabiashara aliyekuwa akitafuta lulu za thamani. Hawa, asema Yesu, “alipokwisha kupata lulu ya thamani kubwa, akaenda akauza alivyo navyo vyote na kuinunua” (Mt 13:46). Hebu tusimame kwa muda kuhusu ishara za mfanyabiashara huyu, ambaye hutafuta kwanza, kisha kupata na hatimaye kununua.” Ishara ya kwanza ni Kutafuta. Hii inahusu mjasiriamali huyu ambaye hasimami lakini anatoka nyumbani na kuwa njiani katika kutafuta lulu ya thamani. Hasemi: “Inatosha yale niliyo nayo, lakini anakwenda kutafuta nzuri zaidi. Na huu ni mwaliko kwetu sisi na bila kujifungia katika ukawaida, katika ukiburi kwa yule hasiyefurahia, lakini ili afikie katika shauku kwa kukuza ndoto nzuri, kutafuta mapya ya Bwana, na kwa sababu Bwana sio kurudiarudia, daima kukupelekea mapya, daima kufanya mambo mapya ya maisha (Mdo 21,5).
Baba Mtakatifu akiendelea amesema “Ishara ya pili ya mfanya biashara ni kupata. Yeye ni mtu mwerevu ambaye anao mtazamo na anajua lulu kubwa yenye thamani. Hii siyo kitu rahisi. Tufikirie kwa mfano wafanyabishara mashuhuri wa Mashariki, mahali ambapo wanakuwa katika meza zilizojaa bidhaa, na wakiwa wamekaa na kujaa kando ya kuta na watu wengi wakipita barabarani wabatazama: au baadhi ya vimeza vinavyoonekana kwenye miji mingi vikiwa vimejaa vitabu na vitu vingine. Wakati mwingine, soko hizi mahali ambapo watu husimama kutazama vizuri, unaweza hata kugundua lulu; vitu vyenye thamani, yaani vitabu visivyopatikana ambavyo kwa kuchanganywa yote haivionekani kwa haraka.
Lakini mfanyabiashara ana mtazamo makini na anajua kung’amua lulu. Hata hiyo Papa alikazia kusema kuwa ni mafundisho kwetu sisi, kila siku, nyumbani, njiani, kazini , likizoni ambapo kuna uwezekano wa kutambua yaliyo mema. Na ni muhimu kujua kufatua kile ambacho ni muhimu: kufanya mazoezi ya kujua vito vya thamani ya maisha na kuvitofauitisha na mikusanyiko ya vitu visivyotumika na visivyo na thamani. Kutokana na hilo Baba Mtakatifu Francisko ameomba kuwa tusipoteze wakati na huru kwa ajili ya mambo ya bure, yakupitisha wakati na ambayo hutuacha watupu ndani, wakati maisha yanatuzawadia kila lulu yaani azima ya thamani ya kukutana na Mungu na wengine.”
Ishara ya mwisho, ambayo Baba Mtakatifu amedadavua ni kwamba mfanyabiashara alinunua lulu. Baada ya kutambua thamani yake kubwa aliuza kila kitu, akatoa sadaka kwa kila wema ili aweze kuwa nayo. Alibadilisha kwa kila hesabu yake katika ghara yake; hakuna kingine zaidi bali ile lulu: ndio utajiri pekee, maana ya uwepo wake na wakati wake ujao. Hata hiyo ni mwaliko kwetu. Baba Mtakatifu Francisko ameuliza, je ni lulu hiyo ambayo inaweza kutufanya tuache yote, ambayo Bwana anazungumza na sisi? Ni Yeye mwenyewe, Yesu.” Yeye ni lulu ya thamani ya maisha; ya kutafuta, ya kupata na kuwa ya kwako. Ni muhimu kuwekeza kila kitu kwake kwa sababu unapokutana na Kristo, maisha yanabadilika
Kwa maana hiyo Papa ameomba kufuatilia ishara hizo tatu za mfanyabishara, kuhusu kutafuta, kupata na kununua na kujiuliza baadhi ya maswali. Kwa kuanza na “Kutafuta: je mimi katika maisha yangu niko natafuta? Ninahisi kuwa sawa nimefika, ninafurahia, au ninafanyia zoezi la shauku yangu ya wema? Ishara ya pili kupata: je ninafanyia zoefu ya kufanya mang’amuzi kwa kile kilicho chema na ambacho kinatoka kwa Mungu, kwa kutambua kuacha kile ambacho kinaniachia kidogo au mtupu? Na mwisho kununua: je ninajua kutumia kwa ajili ya Yesu? Je Yeye yuko nafasi ya kwanza na ni wema mkubwa wa maisha yangu. Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu alishauri kuwa ni vema leo hii kumwambia kuwa: “Yesu wewe ni wema wangu kuu zaidi. Maria atusaidie kutafuta kupata na kukumbatia Yesu kwa kila lolote la kwetu.