Papa akisalimiana na waandishi wa habari kwenye ndege kuelekea
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Katika safari ya ndege kuelekea jijini Budapest, Ijumaa tarehe 28 Aprili 2023 kama ilivyo kawaida katika ziara zake za Kitume, Baba Mtakatifu Francisko aliwasalimia waandishi wa habari 73 (Wahungaria 8, na wa mataifa kumi ambao wamendamana naye kwenye ndege ya shirika la Ndege ITA ambayo imepaa kutoka katika Uwanja wa Kimataifa wa Fiumichino majira ya saa 2:21 asubuhi. Baba Mtakatifu akianza na salamu kwa waandishi wa habari na wapiga picha amesema: "Muwe na safari njema nyote! Na kwa kutania kuhusu sauti ya kipaza sauti ambayo hapo awali ilitoa matatizo ya sauti: alisema: "Hii ni kama watoto watukusu, inasikia ...". Haya yamebainishwa na waandishi wa habari wa Vatican waliko kwenye msafari na Baba Mtakatifu kwa siku hizi kuanzia 28-30 Aprili 2023.
Mashtaka dhidi ya Wojtyla
Baadaye Baba Mtakatifu Francisko aliwasalimia waandishi wa habari mmoja baada ya mwingine, akitafuta namna ya kutoa maneno ya matani. Mwandishi wa shirika la PAP la Poland alimshukuru kwa kumtetea Matakatifu Yohane Paulo II, yaani katika maneno yake yaliyosemwa wakati wa Sala ya Malka wa Mbingu mnamo tarehe 16 Machi kuhusiana matamshi yaliyotamkwa kwenye TV ya moja kwa moja na kaka wa Emanuela Orlandi, raia wa Vatican ambaye alitoweka miaka 40 iliyopita akiwa na umri wa miaka 15. Maneno ya Pietro Orlandi, yaliyonukuliwa kwenye audio ya sauti, ambapo alizungumza juu ya tabia zinazodaiwa za Papa wa Kipoland kwamba alikuwa akitoka jioni na kuwa “hakika sio kubariki nyumba”. “Madai ya kuudhi na yasiyo na msingi”, alisema Papa kutoka dirisha la Jumba la Kitume siku chche zilizopita. Kwa hiyo amerudia kusema “Upuuzi wa mashtaka haya" kwa kwa waandishi katika ndege akimjibu mwandishi wa habari kutoka nchi ya Papa Wojtyla.
Zawadi kwa kumbukumbu ya wahamiaji waliokufa huko Cutro
Papa baadaye alijibu maswali kuhusu afya yake kwa tabasamu na kukusanya zawadi mbalimbali zilizotolewa na waandishi wa habari. Kimsingi alipewa, chupa ya mtoto na dira ya ramani, Vilivyotolewa na Eva Fernandez, mwandishi wa habari wa Kihispania kutoka Radio Cope, anayejulikana kwa upekee na uhalisi wa zawadi zinazotolewa kwa Papa katika kila safari ya kitume. Chupa na ramani ya dira ni ukumbusho wa ajali mbaya ya meli ya Cutro, huko Calabria, mnamo tarehe 26 Februari 2023 ambayo ilisababisha vifo vya zaidi ya watu 80. Mkasa ambao Papa alikuwa ameelezea uchungu wake wote.