Sudan Kusini:Papa,asikiliza historia ya watawa waliouawa na majambazi
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Padre Luka Hassan Arnu, wa Jimbo la El Obeid nchini Sudan ambaye amezungumza mbele ya Papa Francisko na Sista Regina, ambaye alikumbusha kwamba alifika Juba pamoja na washirika wengine kuabudu Bwana na kusherehekea umoja wa watu wa Mungu wa nchi hizo mbili. Na alimhakikishia Papa Francisko kwamba katika Sudan na Sudan Kusini licha ya kuwepo kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe na madhara yote yanayotokea, Kanisa halijawahi kuacha kutekeleza jukumu lake la kikuhani, kinabii na kichungaji. Kupitia taasisi za kichungaji, afya na elimu, Kanisa huratibu na kutoa huduma kwa wengine, licha ya kuwa na rasilimali chache. Ni katika Mkutano huo wa Papa Francisko na watu hao waliowekwa wakfu, Jumamosi tarehe 4 Februari 2023, katika ziara yake ya kitume nchini Sudan Kusini iliyoanza alasiri tarehe 3 Februari, ambayo inamalizika tarehe 5 Februari 2023.
Wakati huo huo, katika ushuhuda wa Padre Luka mbele ya Papa alikumbuka changamoto nyingi zinazolikabili Kanisa la nchi hizo mbili ndugu, lililoungana katika Baraza moja la Maaskofu, (yaani, Baraza la Maaskofu Katoliki Sudan SCBC), linaloongozwa na Askofu wa Jimbo lake, Yunan Tombe Trille Kuku Andali. “Ukanamungu wa kimfumo, kutojali matendo ya kidini, migogoro ya kikabila na mapigano ya ardhi na maliasili zingine, njaa, huduma duni za kijamii kutokana na uhaba wa chakula, bei ya juu, ukosefu wa kazi na mishahara duni. Haya yote, alisisitiza Padre Luca kuwa ni kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu na ukosefu wa nia za viongozi wao wa kisiasa kushirikiana kwa ajili ya amani. Na alihitimisha ushuhuda wake kwa maombi kwa Mungu ili aweze kwa ziara hiyo ya kihistoria, aguse mioyo ya Wasudan na awalette amani ya kudumu. Na ameomba kwa maombezi ya Bikira Mtakatifu Maria, Malkia wa Amani, na Mtakatifu Josephine Bakhita, mzaliwa wa magharibi mwa Sudan na kufariki huko Schio, katika eneo la Vicenza nchini Italia.
Kwa hiyo katika hotuba yake Baba Mtakatifu Francisko kwa maaskofu, mapadre, mashemasi, wanaume na wanawake watawa na waseminari katika Kanisa kuu la Mtakatifu Teresa mjini Juba, Papa amechukua sura ya maji ya Mto Nile unaovuka nchi, ambayo tayari Ijumaa tarehe 3 Februari ilikuwa imeongoza roho ya hotuba yake alipozungumza na mamlaka ya Sudan Kusini, na aliirudisha sura ya Musa kuweza kutoa maelekezo muhimu kwa wale amnao wameitwa kuwa Wachungaji katika nchi hiyo. Baba Mtakatifu Francisko amesema: “Musa akiwa na fimbo mkononi, Musa akiwa amenyoosha mikono, Musa akiwa ameinua mikono. Huo ndio mwito wa Papa Francisko juu ya wajibu wa kuitikia wito wa Mungu wa kuwa vyombo vya wokovu kwa watu, na kwambe wasiondoe mitazamo yao kwenye mateso yao na kujifanya kuwa uwepo wa kinabii katikati ya historia yao.
Baba Mtakatifu Francisko aidha amebainisha kwamba kiukweli, maji ya mto mkubwa hukusanya vilio vya mateso ya jamii zao, hukusanya kilio cha uchungu wa maisha mengi yaliyovunjika, hukusanya majanga ya watu wanaokimbia, mateso ya mioyo ya wanawake na hofu iliyowekwa machoni pa watoto. Hofu zinaonekana machoni pa watoto. Wakati huo huo, hata hivyo, maji ya mto mkubwa yanawatudisha kwenye historia ya Musa na, kwa hiyo, ni ishara ya ukombozi na wokovu. Kiukweli, Musa aliokolewa kutoka katika maji hayo na akiongoza familia yake katikati mwa Bahari ya Shamu, alikuwa chombo cha ukombozi, sura ya msaada wa Mungu ambaye aliona mateso ya watoto wake, alisikia kilio chao na kushuka ili kuwaweka huru.