Hija ya Kitume ya Papa Francisko Cyprus na Ugiriki:pongezi kwa uwazi na ukarimu!
Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.
Baada ya mkutano wake na wakleri katoliki, watawa na makatekista waliokusanyika katika Kanisa Kuu la Kimaronite la Mama yetu wa Neema la Nicosia mwanzoni mwa ziara yake ya Kitume huko Cyprus, Papa Francisko aliendelea na kukutana na Rais wa Cyprus Nikos Anastasiades na kufuatiwa na kubadilishana zawadi na anwani mbali mbali zilizotolewa kwa serikali na wawakilishi wa kidiplomasia waliopo. Rais Anastasiades alimshukuru Papa Francisko kwa ziara yake nchini Cyprus, kwa kuweka wazi historia ndefu ya taifa hilo ya kukaribisha watu katika ardhi yake na jukumu muhimu ambalo limechukua kutokana na eneo lake la kijiografia kati ya magharibi na mashariki, huku ikipendelea kuishi pamoja kwa amani na kuwakaribisha watu wengine.
Muundo wa makabila mbalimbali ni sifa ya taifa hilo, alibainisha Rais huto, wakati akieleza kuunga mkono kazi ya Vatican katika kuhimiza amani na mazungumzo duniani kote. Pia alibainisha jinsi Cyprus imeweza kukaribisha wakimbizi na wahamiaji wengi katika ardhi yake na kumshukuru Papa Francisko kwa yote aliyofanya katika eneo hilo hasa wahamiaji 50 kutoka Cyprus hadi Italia. Aidha alisisitiza changamoto iliyogawanya Cyprus kwa muda mrefu na ambayo inaendelea. Video fupi na picha vinaonesha tukio la Mkutano huo na Papa.