杏MAP导航

Tafuta

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Cyprus na Ugiriki:Papa ametoka Cyprus kuelekea Ugiriki

Baada ya kumaliza siku mbili katika hija yake ya kitume huko Cyprus,Papa Francisko ameanza siku ya tatu ya kitume kuelekea Ugiriki Jumamosi asubuhi tarehe 4 Desemba 2021.Video fupi inaonesha tukio la kuagwa.

Na Sr Angella Rwezaula – Vatican.

Baada ya siku mbili akiwa huko Cyprus, katika ziara yake ya kitume, Papa Francisko ameondokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Larnaca 2:30 asubuhi, Jumamosi tarehe 4 Desemba 2021. Kabla ya kuondoka Papa amekaribishwa na kuagwa rasmi kwa afla maalum mbele Ikulu ya rais huko Atene. Ratiba yake akiwa Ugiriki ni kukutana kwa faragha na Rais wa Ugiriki Bi Katerina, Sakellaroupoulou, kukutana na waziri Mkuu, baadaye viongozi wa mamlaka, raia na kundi la wanadiplomasia. Video fupi inaonesha tukio la afla ya kuagwa na baadaye tutaendelea kuwajuza.

04 Desemba 2021, 11:00