Papa:Mtakatifu Yosefu alikuza maisha ya haki na ufunguzi katika ishara za Mungu
Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko ameomba kuendelea kutazama sura ya Mtakatifu Yosefu kwa waamini na mahujaji waliofika katika ukumbi wa Paulo VI, jijini Vatican, Jumatano tarehe Mosi Desemba 2021 katika katekesi yake, ikiwa ni mwendelezo wa tafakari ya Mtakatifu Yosefu katika mwaka wake unaokaribia kuhitimishwa mnamo tarehe 8 Desemba. Papa Francisko kwa maana hiyo amejikita kufafanua juu ya ahadi ya mchumba Maria na kutoa ujumbe kwa wachumba hata wanandoa wapya. Ni matukio mengi yanayohusu Yosefu ambayo yanasimuliwa na Injili ambazo sio za Kanoni ya Sheria ya Kanisa na ambazo zilitoa chachu hata katika sanaa na maeneo mengi ya ibada. Papa Francisko amefafanua kwamba maandiko hayo hayapo katika Biblia ni simulizi ambazo kwa ibada ya wakristo wa zamani walikuwa nazo na zilikuwa zinaendana na shauku ya kutuliza ule utupu ambao unaachwa katika Injili za Kisheria, na ambazo ziko kwenye Biblia zinazotuita kufuata kile ambacho ni muhimu wa imani na maisha ya Kikristo. Papa amesisitiza hiyo ni muhimu. Je Injili inaeleza nini kuhusu Yosefu? japokuwa si yale yasemwayo na Injili nyingine zisizo za kisheria hata kama si mambo mabaya au katili hapa, ni mazuri lakini sio Neno la Mungu. Kinyume chake Injili ambazo ziko kwenye Biblia ni Neno la Mungu. Kati ya Injili hizi ni Mwinjili Matayo ambaye anamfafanua Yosefu mwanaume wa haki. Katika simulizi yake anasema: “Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Maria mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. (rej Mt 1,18-19). Hii ni kwa sababu, kipindi cha uchumba ikiwa mchumba hakuwa mwaminifu au alipata ujauzito, ilikuwa lazima ashitakiwe. Na wanawake wa wakati huo walikuwa wanapigwa mawe. Lakini Yosefu alikuwa mwenye haki. Na kusema kuwa "mimi sitafanya na hivyo ninakwenda zangu kimya kimya", Papa amefafanua.
Ili kuelewa tabia ya Yosefu mbele ya Maria ni vizuri kukumbuka tamaduni za Ndoa ya zamani huko Israeli. Wakati wa kufanya ndoa kulikuwa na hatua mbili zinazofafanuliwa vizuri. Ya kwanza ilikuwa ni ile ya uchumba rasimi ambao ulikuwa tayari mpya kwa namna ya pekee wa haki ya kuwa mwanamke licha ya kuendelea kuishi katika nyumba ya wazazi kwa mwaka mzima alikuwa anafikiriwa tayari kuwa ni mke ahadi ya mchumba kijana wake. Hata kama walikuwa hawaishi pamoja lakini alikuwa kama vile ni mke wake. Katika hatua ya pili ilikuwa ni kuhama sasa mchumba kwenda katika nyumba ya mchumba wake kijana. Hapo ilifanyika siku kuu kubwa ya kutimiza ndoa. Na marafiki wa bi harusi walimsindikiza huko. Katika muktadha wa matumizi hayo tendo la Maria kukutwa na mimba kabla hajaenda kuishi pamoja, bikira huyo alikuwa ashitakiwe kuwa mzinzi. Na kosa hili kwa mujibu wa sheria ya zamani alikuwa lazima apate adhabu kwa kupigwa mawe (Dt 22,20-21). Lakini hatua iliyofuata baadaye ya kiyahudi kwa kulegeza adhabu hiyo waliweka kuacha mchumba hiyo lakini akipewa adhabu bila kuuawa.
Injili inasema kuwa Yosefu alikuwa ni mwenye haki kwa sababu alikuwa chini ya sheria kama kila mwanaume wa Israeli. Lakini ndani yake upendo kwa ajili ya Maria na imani ambayo alikuwa nayo kwa ajili yake ilikuwa inamshauri namna ambayo angeweza kuokoa dhidi ya sheria na sifa ya mchumba wake, aliamua kumwacha kwa siri, bila kelele na bila kumdhalilisha mbele ya umma. Yosefu alichagua njia ya siri, bila mchakato wowote. Ni utakatifu gani huu wa Yosefu! Papa ameongeza, kuwa sisi mara tu tunapopata habari fulani ya moto au kidogo mbaya kuhusu mtu fulani, tunakimbilia kusengenya kwa haraka! Lakini Yosefu alikaa kimya tu”. Na Mwinjilia Matayo anaongeza haraka kwamba: “Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Maria mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao” (Mt 1,20-21). Katika kufanya mang’amuzi ya Yosefu, sauti ya Mungu inaingilia kati kwa njia ya ndoto ambayo inamwonesha maana kuu zaidi ya haki yake aliyo nayo mwenyewe.
Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa ni jinsi gani ilivyo muhimu kwa kila mmoja kukuza maisha ya haki na wakati huo huo kuhisi daima kama wahitaji wa msaada wa Mungu ili kuweza kupanua peo zetu na kufikiria muktadha wa maisha kwa mtazamo tofauti, ulio mpana zaidi. Mara nyingi tunahisi kuwa wafungwa wa kile kilichotokea: “ Tazama kile kilichonipata”, na hapo tunabaki tumefungwa kwa kile kibaya ambacho kilitokea. Lakini mbele ya mambo mengi ya maisha, yanayotokea mwanzoni kama makubwa, ndani mwake unajificha uwezo wa Mungu ambaye kadiri ya muda unavyopita ndivyo anaunda na kuangaza maana yake hata uchungu ambao ulitupata. Papa Fancisko amesema kwamba kishawishi kikubwa ni kile cha kujifunga ndani ya uchungu,na kuwa mawazo mabaya mara kadha yaliyotutokea. Hilo si jambo jema. Hili linakupelekea kuwa na huzuni na uchungu. Moyo mchungu ni mbaya sana. Papa Francisko amependa kusimama na kutafakari kinagaubaga cha historia hiyo iliyosimuliwa na Injili na ambayo mara nyingi inaachwa hivyo. Maria na Yosefu walikuwa wachumba ambao bila shaka walikuza ndoto na matarajio kulingana na maisha yao na wakati wao ujao. Mungu aliingilia kati kama vile kwa ghafla katika maisha yao hata kama mwanzo ilikuwa ni vigumu wao kuelewa, wote wawili walifungulia moyo wazi kwa uhalisia wa mambo yaliyokuwa mbele yao.
Baba Mtatifu Francisko amesema: “Ndugu wapendwa kaka na dada, mara nyingi maisha yetu sio kama tunavyoyafikiria. Hasa kwa upande wa uhusiano wa upendo, kwani inakuwa ngumu kupita mantiki ya upendo la kitoto kufikia upendo uliokomaa. Ni lazima kutoka katika pendo la kitoto ili kufikia upendo uliokomaa. Kwa kuwagekia wanandoa wapya, Papa Francisko amewaomba watakafari vizuri hilo. Akiendelea amesema katika hatua ya kwanza daima imejaa uhakika wa kushangaza na ambao unatufanya kuingia katika kudhania na mara nyingi mawazo hayo hayaendani na hali halisi ya vitendo. Kuangukia katika upendo na mara tu unapoanguka katika upendo na matarajio yake yanaonekana kuisha, hapo upendo wa kweli unaweza kuanza au upendo wa kweli huja. Kiukweli, kupenda haimaanishi kutarajia mwingine au maisha kuendana na mawazo yetu; badala yake, inamaanisha kuchagua kwa uhuru kamili kuchukua jukumu la maisha kama inavyotolewa kwetu. Ndiyo maana Yosefu anatupatia fundisho muhimu, ambapo anamchagua Maria kwa macho yaliyofunguliwa wazi. Papa kwa kuongezea amesema tunaweza kusema kwa wote kuwa ni hatari. Fikiria katika Injili ya Yohane, kejeli aliyoipta kutoka kwa walimu wa sheria kwa Yesu kwa kumwambia kuwa: “sisi siyo watoto wa yule(...) wakiimaanisha wa malaya. Kwa maana walikuwa wanajua kuwa Maria alipata mimba na walikuwa wanataka kumchafua mama wa Yesu. Kwa upande wa Papa amesema hii ni sehemu chafu, iliyo ya ibilisi zaidi katika Injili. Na hatari ya Yosefu inatupatia fundisho. Anachukua maisha jinsi yalivyo. Mung ualiingilia kati hapo, na kumshika mkono. Na Yosefu alifanya kama alivyo ambiwa na Malaika wa Bwana. Akamchukua mchumba wake ,na ambaye alikua hamjuhi na wala kuishi naye akiwa anasubiri mtoto ambaye alimzaa mwanaume na akamwita Yesu (Mt 1,24-25).
Wachumba wa Kikristo wanaalikwa kuwa mashuhuda wa upendo kwa namna kwamba wawe na ujasiri wa kupitia mantiki za kuangukia katika upendo na kufikia upendo uliokomaa. Hii ni uchaguzi unaofaa ambao badala ya kujifungia maisha, unaweza kukuza upendo kwa sababu uweze kudumu mbele ya majaribu ya kila kipindi. Kwa kusisitiza zaidi Papa amesema upendo wa wanandoa unakwenda mbele katika maisha na kukomaa kila siku. Upendo wa wachumba kinyume chake kidogo ni wa kimapenzi. Wao wanasahau, lakini pia kuna kuanza upendo uliokomaa wa kila siku, wa kazi, wa watoto ambao wanazaliwa… Na wakati mwingine, mapenzi yanatoweka kidogo. Papa ameuliza swali, lakini hakuna upendo? Ndiyo upendo upo lakini uliokomaa. Na kuhusu suala la kugombana Papa amesema linakuwapo kwasababu hilo lilianzia kwa Adamu na Eva hadi leo hii. Kwa maana hiyo tendo la wanandoa kugombana ni mkate wetu wa kila siku. Swali je hatupaswi kugombana? ndiyo inafanyika ,lakini hata kama hasema wafanye hivyo lakini inawezekana. Wengine wanasema: "Padre sisi wakati mwingine tunaamsha sauti"… Ndiyo inatokea Papa amesema na kuongeza kuwa hata wakati mwingine sahani zinarushwa juu". Akiendelea na mifano Papa Francisko amesema: “Je ni kufanya nini ili nisije kuharibu maisha ya ndoa? Sikiliza kwa makini: usimalize siku bila kufanya amani". Kwa kusema kuwa "Tumegombana, nilikuambia maneno mabaya Mungu wangu, nimekwambia mabaya. Lakini sasa siku inaisha lazima nifanye amani."
Papa Francisko ameuliza: “Je mnajua kwanini? Kwa sababu vita baridi siku inayofuata ni hatari sana. Msiruhusu siku inayofuata kwenda vitani. Kwa hili lazima kufanya amani kabla ya kwenda kulala.” "Oo lakini Padre, unajua sijui jinsi ya kujieleza ili kuleta amani baada ya hali mbaya ambayo tumeishi”. Ni rahisi sana Papa ameeleza kwa ishara ya kubembeleza na kwamba amani tayari imetengenezwa! " Lakini daima kumbuka kwamba kila wakati msimalize siku bila kufanya amani. Na hii itawasaidia katika maisha ya ndoa. Kwao na kwa watu wote wa ndoa waliokuwapo kwenye ukumbi. Suala la kutoka katika penzi hadi kufika pendo lililokomaa ni chaguo la lazima, lakini lazima wote kupitia njia hiyo. Papa ameomba kuhitimisha kwa sala ya Mtakatifu Yosefu. “Mtakatifu Yosefu, wewe uliyempenda Maria kwa uhuru na ukachagua kuacha mawazo yako ili kutoa nafasi kwa ukweli, utusaidie kila mmoja wetu ashangazwe na Mungu na kukaribisha maisha, sio kama jambo lisilotarajiwa ambalo tunapaswa kujilinda, lakini kama fumbo inayoficha siri ya furaha ya kweli. Uwajalie wapate furaha na kusimika mizizi wachumba wote wa Kikristo huku kila mara akidumisha ufahamu kwamba huruma na msamaha pekee ndio hufanya upendo uwezekane. Amina.