Hija ya Kitume ya Papa Francisko Cyprus na Ugiriki: Siku ya pili ya hija yake
Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.
Katika ziara ya kitume ya Papa Francisko aliyoanza tarehe 2 Desemba kuelekea Cyprus, amepokelewa kwa shangwe kuu. Mwaliko wa nguvu wa kufuata mantiki ya kutojali ambazo zinakwenda kinyume na Injili na kile ambacho ni chema kinachoweza kuhatarisha umoja, upendo mkuu na ulazima wa kibinadamu. Wito wa kuachilia mbali nadharia hasi na kufanya kazi kwa pamoja karibu katika upendo, katika elimu, katika kuhamasisha hadhi ya binadamu; kwa kufanya hivyo inawezekana kabisa kutembea kidugu na umoja unaweza kukomaa. Hayo yameoneka katika hotuba ya Papa Francisko akizungumza na ndugu yake Chrysostomos II, Askofu Mkuu wa Cyprus na kumshukuru kwa ajili ya ufunguzi wa moyo na jitihada za kiekumene katika hotuba yake Baba Mtakatifu kwa Sinodi ya Kanisa la Kiordhodox katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Mtaalimungu huko Nicosia. Video fupi inaonesha matukio mbali mbali kama vile kufika, kutia saini, kupokea zawadi ya mshumaa na kubariki.