Ziara ya kitume Cyprus na Ugiriki:Papa Francisko ameomba kusali kwa ajili ya ziara yake
Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.
Matarajio ya safari yake kwenye vyanzo vya imani na udugu wa kiekumene, yaani katika safari ya kwenda kugusa miili ya maelfu na maelfu ya wahamiaji ambayo imekaribia, Papa Francisko ameomba sala kwa ajili ya hija yake ya kitume kwenda kisiwa cha Cyprus na Ugirikia ambayo anaanza Alhamisi tarehe 2 Desemba 2021 hadi Jumatatu ijayo tarehe 6 Novemba 2021. Mara baada ya katekesi yake Tarehe Mosi Desemba Baba Mtakatifu Francisko amependa kushirikishana na waamini na mahujaji wote waliofika katika Ukumbi wa Paulo VI kuhusu matarajio hayo na matumaini yake kwenye ziara yake ya 35 kimataifa ambayo itamwona anagusa vituo vya Nicosia, Atene, Lesvos.
Papa amesema: “Kesho ninaondoka kwenda Cyprus na Ugiriki kutimiza ziara kwa watu wapendwa wa nchi mbili zenye utajiri wa kihistoria, tasaufi na ustaarabu. Itakuwa ni safari katika vyanzo vya imani ya kitume na udugu kati ya wakristo na madhehebu mengine. Nitakuwa na fursa ya pekee kukaribia ubinadamu uliojeruhiwa katika miili ya wahamiaji wengi wanaotafuta matumaini”. Papa amesema tena akigusia juu ya ziara katika kituo cha mapokezi na utambulisho cha Mytilene, ambacho itakuwa ni kwa mara ya pili baada ya ile ya mnamo Aprili 2016 katika kambi ya wakimbizi wa kisiwa cha Ugiriki ambacho ni kitovu cha janga la uhamiaji na ambacho kinaelemewa na kuisumbua Ulaya
Papa Francisko amesema: "ninaomba kunisindikiza kwa sala” na huo ni mwuti ulioanza mwanzo na ambao ni dharura katika kila ziara yake ya kitume. Hata katika ujumbe wake kwa njia ya video alioutoa mnamo tarehe 27 Novemba kwa watu wa Ugiriki na Cyprus. Papa Franciko aliomba kusindikizwa na sala ya pamoja juu ya hija hiyo katika vyanzo imani na udugu, ambayo ni mizizi ya Ulaya na ubinadamu. “Nitakwenda Lesvos tena, kwa imani kwamba vyanzo vya maisha ya kawaida ya kuishi pamoja vitastawi tena katika udugu na ufungamanishwaji pamoja. Hakuna njia nyingine na kwa 'udanganyifu' huu ninakuja kwenu” alisema Papa katika ujumbe wake kwa njia ya video.
Akiwasilisha ziara yake ya kitume Jumatatu tarehe 30 Novemba 2021 katika Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican, msemaji Mkuu wa Vatican, Dk Matteo Bruni alionesha miongozo miwili muhimu ambayo inaelekeza mbele ya ziara nzima ya Papa. Kwa upande mmoja, majadiliano ya kiekumene katika nchi ambazo Jumuiya za kikatoliki ni wachache ukilinganishwa na Waorthodox walio wengi, kwa maa hiyo, umoja wa Makanisa yanayokaliwa ni sehemumsingi na ishara ya ulimwengu wa Magharibi pamoja na tasaufi ambayo ustaarabu wa Ulaya umestawi. Kwa upande mwingine, kukumbatiwa kwa watu ambao maisha yao yanawakilisha janga kubwa zaidi la kibinadamu tangu Vita vya Pili vya Dunia ni lile la uhamiaji.
Kama ilivyokuwa kwa mwaka wa 2016, lakini kwa njia tofauti, Papa anaweza kupeleka msaada halisi kwa watu hawa. Miaka mitano iliyopita, itakumbukwa, baadhi ya familia za wakimbizi zilipanda ndege ya Papa ili kuja Roma na kuanza maisha mapya. Wakati huu, pia kwa sababu ya sheria kali zaidi na vizuizi vya UVIKO - 19, wako wanatafuta njia ya kupitia mikondo ya kibinadamu, lakini baada ya ziara ya Papa wataweza kuletwa wakimbizi wengine nchini Italia ili kusambazwa tena barani Ulaya, shukrani kwa kazi ya upatanisho ambayo inaona walio mstari wa mbele Jumuiya ya Mtakatif 'Egidio. Katika ziara ya Askofu wa Roma, kama alivyosema Dk. Bruni, pia kutakuwa na kumbukumbu ya jeraha la wazi la Cyprus lililogawanyika, kwa matumaini ya kuunganishwa tena.