杏MAP导航

Tafuta

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Cyprus na Ugiriki:Kukutana na wakimbizi

Papa Francisko ameanza ziara yake ya 35 ya kimataifa kuelekea huko Cyprus na Ugiriki kuanzia tarehe 2-6 Desemba 2021.Kabla ya kuondoka amekutana na makundi mawili ya wakimbizi.La kwanza katika nyumba ya Mtakatifu Marta. Kundi la pili amekutana nalo katika Parokia ya Mtakatifu Maria karibu na uwanja wa Ndege wa Kimataifa Fiumicino.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko aliondoka uwanja wa Ndege wa kimataifa saa 5.5 asubuhi Alhamisi tarehe 2 Desemba kuelekea kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Cyprus mahali ambapo amewasili mchana baada ya masaa matano ya safari. Video fupi inaonesha matukio hayo.

Kabla ya kuondoka katika nyumba ya Mtakatifu Marta Vatican amekutana na kundi la watu 12 wakimbizi wakizindikizwa na Msimamizi wa sadaka ya Kitume Kardinali Krajewski. Baadhi ya wakimbizi hao walifika na Papa Francisko katika ndege moja wakati alipotembelea Lesbos mnamo 2016. Papa pia alikutana na kundi jingine la wakimbizi 15 wanaoshughulikiwa na Parokia ya Mtakatifu Maria karibu na uwanja wa Ndege Kimataifa wa Fiumicino Roma. Papa amewza kusali kwa sanamu ya Bikira Maria wa Loreto na kuwasalimia wakimbizi hao kabla ya kuendelea na safari yake.

02 Desemba 2021, 17:30