杏MAP导航

Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Misa takatifu amewashukuru watu wa Mungu nchini Cyprus kwa moyo wao wa ukarimu na mapokezi makubwa waliyomkirimia. Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Misa takatifu amewashukuru watu wa Mungu nchini Cyprus kwa moyo wao wa ukarimu na mapokezi makubwa waliyomkirimia. 

Hija ya Papa Francisko Cyprus na Ugiriki: Shukrani Kwa Cyprus

Papa mara baada ya Misa Takatifu, amewashukuru watu wote wa Mungu kwa uwepo wao, lakini kwa namna ya pekee, uwepo na ushiriki wa Rais wa Cyprus. Amewashukuru wote kwa ukarimu na upendo waliomwonjesha. Ameonja umoja na utofauti wa Mapokeo ya Kikristo. Hizi ni jumuiya za Kikristo zinazoishi kwa matumaini hali ya sasa, huku zikiwa wazi kwa kesho iliyo bora zaidi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Askofu mkuu Pierbattista Pizzaballa, Msimamizi wa kitume wa Upatriaki wa Yerusalemu, katika salam zake za kumkaribisha Baba Mtakatifu Francisko ili aweze kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu, tarehe 3 Desemba 2021 kwenye Uwanja wa Uwanja maarufu wa “Il Pancyprian Gymnastic Association Stadium” maarufu kama New GSP, Kwa lugha ya Kigiriki “Στ?διο Γυμναστικ?? Σ?λλογο? "Τα Παγκ?πρια") ameelezea kwa umuhimu Cyprus katika mchakato wa uinjilishaji na utamadunisho wa Injili, changamoto na matatizo yaliyojitokeza, lakini hata hivyo Habari Njema ikatangazwa na kushuhudiwa kwa watu wa Mataifa. Cyprus ni nchi ambayo imeendeleza kwa kiasi kikubwa majadiliano ya kitamaduni na kiekumene na hivyo kuvuka mipaka ya kinzani za kidini, kitamaduni na kikabila. Leo hii majadiliano ya kiekumene yanaendelea kupewa kipaumbele cha pekee katika huduma ya ukarimu kwa wakimbizi, wahamiaji na wale wanaotafuta hifadhi ya kisiasa. Hii ni nchi ambayo imegeuka na kuwa ni kisima cha huruma ya Mungu kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii.

Kwa upande wake, Askofu mkuu Selim Sfeir wa Kanisa la Wamaroniti wa Cyprus amemshukuru na kumpongeza Baba Mtakatifu Francisko kwa kufika ili kuwaimarisha katika imani, matumaini na mapendo thabiti. Kwa kufuata nyayo za Bikira Maria, wanapenda kufunga safari na kumwendea Kristo Yesu, Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho, nyakati zote ni zake. Wanataka kuzima kiu ya imani kutoka katika chemchemi ya imani kwa Kristo Yesu na Kanisa lake! Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya maadhimisho ya Misa Takatifu, amewashukuru watu wote wa Mungu kwa uwepo wao, lakini kwa namna ya pekee kabisa, uwepo na ushiriki wa Rais wa Cyprus. Amewashukuru wote kwa ukarimu na upendo waliomwonjesha. Ameonja umoja na utofauti wa Mapokeo ya Kikristo. Hizi ni jumuiya za Kikristo zinazoishi kwa matumaini hali ya sasa, huku zikiwa wazi kwa kesho iliyo bora zaidi. Amewashukuru wale wote waliocharika usiku na mchana ili kuandaa hija yake ya kitume nchini Cyprus.

Shukrani
03 Desemba 2021, 15:16