杏MAP导航

Tafuta

2021.10.04 Papa Francisko na Patriaki Bartolomeo I 2021.10.04 Papa Francisko na Patriaki Bartolomeo I 

Ujumbe wa Papa kwa Patriaki Bartholomeo katika Siku kuu ya Mtakatifu Andrea

Papa Francisko ametuma ujumbe wake uliowakilhswa na Kardinali Kurt Koch akiongoza uwakilishi wa Vatican katika siku kuu ya Upatriki wa Kiekumene kuadhimisha Siku kuu ya Mtakatifu Andrea Instanbul Uturuki.Papa kuwa wakati wanaendelea mchakato wa kuwa na muungano kamili kati ya makanis kwa kuongozwa na maombezi wasimamizi wa makanisa Bwana asaidie kuwa tayari kukumbatia zawadi ya uongofu na kutoa msamaha.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Katika utamaduni wa kubadilishana, uwakilishi kwa ajili ya siku kuu za watakatifu Wasimamizi, mnamo tarehe 29 Juni Roma katika fursa ya Maadhimisho ya Watakatifu Petro na Paulo na tarehe 30 Novemba huko Instanbul kwa ajili ya maadhimisho ya Mtakatifu Andrea, Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Umoja wa Kikristo, ameongoza Uwakilishi wa Vatican katika siku kuu ya Upatriaki wa Kiekumene. Kardinali Koch amesindikizwa na Askofu Brian Farrell, Katibu wa Baraza hilo, Askofu Andrea Palmieri, Katibu msaidizi. Wakiwa Istanbul, ameunganika na  Uwakilishi wa Monsinyo Walter Erbi, mhusika wa mambo ya ndani katika Ubalozi wa Kitume huko Uturuki. Uwakilishi wa Vatican, umeshiriki Siku Kuu Takatifu ya Liturujia iliyoongozwa na Patriaki wa Kiekumene BartolomeoI katika Kanisa la Upatriaki la Mtakatifu George huko Fanar. Kardinali Koch amekabidhi Patriaki wa Kiekumene ujumbe ulioandikwa na Baba Mtakatifu ambapo umesomwa mara baada ya Maadhimisho ya Liturujia.

Na kwa upande wa Ujumbe wa Papa Francisko amewatumia anatoa matashi mema na kwamba anafanya hivyo, si tu kwa kuzingatia urafiki wetu wa kndugu bali pia uhusiano wa kale na wa kina wa imani na mapendo kati ya Kanisa la Roma na Kanisa la Constantinople. Kwa hakikisho la ukaribu wake wa kiroho, anatuma wajumbe kuwasilisha matashi mema ya furaha na amani kwao, ndugu Maaskofu, na wakleri, watawa na waamini walei waliokusanyika katika Kanisa la Upatriaki la Mtakatifu George kwa ajili ya Liturujia ya kumbukumbu ya Mtume Andrea. Baba Mtakatifu anaelezea jinsi ilivyokuwa ni furaha kwake wakati wa ziara yake ya hivi karibuni ya Patriaki wa Kiekumene jijini  Roma mahali ambapo waliweza kubadilishana mawazo yanayohusu wakati uliopo na ujo wa ulimwengu, lakini pia hata kuelezea juu ya jihada za pamoja katika masuala muhimu ya familia yote ya kibinadamu, ikiwemo ya utunzaji bora wa mazingira, elimu kwa wakati ujao wa kizazi, mazungumzo kati ya tamaduni nyingi za kidini na ujenzi wa Amani. Kwa njia hiyo wao ni wachungaji pamoja na Makanisa yao wanaunganika kwa kina na ambao wako tayari wameunganishwa kuanzia na uwajibikaji wao katika kukabiliana na changamoto, wanazoshirikishana katika Imani ya Mungu na Baba, Mwenyezi, muumba wa mbingu na dunia.

Katika Bwana mmoja Yesu Kristo, Mwana wake ambaye alijifanya mtu kwa ajili ya wokovu wetu, alikufa na kufufuka katika wafu; na katika Roho Mtakatifu Bwana mleta uzima ambaye atakuja kuleta maelewano bila kuondoa utofauti wao. Kwa kuuunganishwa na imani hii, Papa aanaandika ni kuombea kwa uthibitisho ili kuweza kuwa na muungano huo. Wakati wanajitahidi kushughulikia masuala ya kitaalimungu na kikanisa katika moyo wa kazi inayoendelea ya Mazungumzo ya kitaalingu. Ni matumaini ya Papa kuwa Wakatoliki na Waorthodox wataweza kuongeza jitihada ya kazi ya pamoja katika sehemu zile ambazo haiwezekani, lakini ambazo ni muhimu kufanya hivyo. Baba Mtakatifu Francisko ameandika kuwa wakati wanaendelea kwenye mchakato wa kuwa na muungano kamili kati ya makanisa yao, kwa kuongozwa na maombezi ya kaka Petro na Andrea ambao ni watakatifu wasimamizi wa makanisa yao wawe na moja kamili ambao wanatarajia kwa hakika na ni zawadi kutoka kwa Mungu kupitia neema ya Roho Mtakatifu. Papa ameandika “Bwana atusaidie kuwa tayari kukumbatia zawadi hii kupitia maombi, uongofu wa kina na uwezo wa kuona na kutoa msamaha.” Kwa hisia za moyo amepyaisha matashi yake mema katika siku kuu ya Mtakatiifu Andrea na kuwatakia Amani.

30 Novemba 2021, 16:11