Vituo vya ziara na mikutano ya Papa Francisko nchini Iraq!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Safari ya Papa aliyotamani sana kwenda Iraq itaanza tarehe 5 Machi na ndege kutoka Roma -Fiumicino kwenda Baghdad kwa kuongozwa na kauli mbiu “Ninyi nyote ni ndugu” inayooneeshwa kwenye nembo ya ziara hiyo. Mapokezi rasmi yatakuwa katika uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Iraq, ambapo Papa Francisko atakuwa na mkutano wake wa kwanza katika Chumba maarufu cha uwanja wa ndege na waziri mkuu, baadaye kuendelea huko Ikulu ya Rais kwa sherehe rasmi ya kukaribisha itafanyika!
Mara baada ya ziara ya faragha na heshima kwa Rais wa Jamhuri katika ofisi yake, hapo Papa atatoa hotuba rasmi ya kwanza kwa mamlaka, uwakilishi wa asasi za kiraia na Kikosi cha Kidiplomasia kwenye ukumbi wa Ikulu ya Rais. Siku ya kwanza ya Papa Francisko itamalizika kwa kufanya mkutano na maaskofu, mapadre, watawa, wanaseminari na makatekista ambao Papa Francisko atahutubia hotuba katika Kanisa Kuu la Katoliki la Mama yetu wa Wokovu huko Baghdad.
Katika siku ya pili akiwa nchini Iraq, Papa anatarajia kwenda katika maeneo ya Najaf, Nassirya na Uwanda wa Uru. Asubuhi, Jumamosi tarehe 6 Machi, Papa Francisko atatoka Baghdad kwenda na ndege katika mji wa Najaf kusini mwa mji mkuu, moja ya maeneo matakatifu katika dini ya Uislamu wa Washia. Hapo kutakuwa na ziara ya heshima kwa Ayatollah Mkuu, Sayyd Ali Al-Husaymi Al-Sistani, na mwishoni Papa ataondoka kwenda Nassiriya, ukingoni mwa Mto Frati, kwa ajili ya mkutano wa kidini katika Uwanda wa Uru. Huko anatarika kutoa hotuba katika fursa hiyo. Mchana, baada ya kurudi Baghdad, anatarajia kuongoza Misa ikifunga siku hiyo, katika Kanisa Kuu la Wakaldayo la Mtakatifu Yosefu, Baghdad, moja ya Makanisa makuu 11 nchini humo.
Jumapili tarehe 7 Machi ni siku ambayo imejaa matukio mengi ambayo yatamwona Papa akitoka kwenda kati ya Kurdistan ya Iraq na Bonde la Ninawi. Asubuhi hiyo itaanza kwa kuondoka na ndege kwenda Erbil. Papa Francisko atakaribishwa katika uwanja wa ndege na mamlaka ya kidini na ya kiraia ya Mkoa wa Uhuru wa Kurdistan ya Iraq. Kutoka hapo, kwa helikopta, uhamisho wa kwenda Mosul, jiji ambalo kwa miaka ilikuwa mikononi mwa waliojiita serikali ya Kiislamu, ambapo atasali pamoja na mamlaka ya kidini, raia kuwaombea waathiriwa huko Hosh al - Bieaa, uwanja wa Kanisa.
Bado tena asubuhi, hiyo uhamisho wa Papa kwa helikopta kwenda mji wa Ashuru ya Qaraqosh katika tambarare ya Ninawi kilomita chache kutoka Mosul, iliyochukuliwa na Dola la Kiisilamu hadi 2016. Baada ya kutua kwenye uwanja, Papa Francisko atakwenda katika Kanisa Bikira safi wa Moyo kwa ajili ya kutembelea jumuiya ya Waqaraqosh ambapo atawahutubia na baadaye kusali sala ya Malaika wa Bwana. Hatimaye Alasiri Papa atahamia tena huko Erbil kwa ajili ya Misa Takatifu itakayoadhimishwa katika Uwanja wa “Franso Harir”. Wakati wa jioni, atarudi Baghdad, na kesho yake siku ya Jumatatuasubuhi tarehe 8, Papa Baba Francisko ataondoka kurudi Romaa baada ya afla fupi ya kuagana.
Kauli mbiu ya ziara ya kitume na nembo: “Ninyi nyote ni ndugu”, ndiyo kauli mbiu iliyochukuliwa kutoka Injili ya Mathayo kuongoza ziara ya Papa Fracisko nchini Iraq na ambayo nembo yake inamwonesha Papa katika ishara ya kusalimiana na nchi, iliyowakilishwa kwenye ramani na alama zake, mtende na mito ya Tigris na Frati. Nembo hiyo pia inaonesha njiwa mweupe,akiwa na tawi la mzeituni kwenye mdomo wake, ambayo ni ishara ya amani, ikipeperusha bendera za Vatican na Jamhuri ya Iraq. Juu ya picha hiyo, kauli mbiu ya ziara hiyo imeandikwa kwa lugha ya Kiarabu, Kikurdi na Kikaldayo.