Habari mpya ya kusimikwa kwa makardinali tarehe 28 Novemba!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Leo hii tarehe 28 Novemba 2020 ,saa 10.00 jioni majira ya Ulaya Papa Francisko atasimika makardinali wapya 9 wenye haki ya kuchaguliwa uchaguzi wa upapa ujao na 4 ambao wamemaliza muda wao. kutokana na umri. Wawili kutoka Asia hawatakuwapo katika tukio hili, wa hivyo wataungana na makardinali wengi wa Baraza hili kushiriki maadhimisho kwa njia ya mtandao. Makardinali wateule ambao hawatakuwapo ni askofu Mkuu Jose Fuerte Advincula, wa Jimbo Kuu Katoliki Capiz na Msimamizi wa Kitume huko Brunei, Askofu Mkuu Cornelius Sim, kwa sababu ya janga la kiafya. Lakini watasimkwa sawa na makardinali wengine mara tu itakapowezekana kwa kutmwa mwakilishi wa Papa katika wakati mwingine ili kuwakabidhi vikofia, pete na Hati ya utambulisho wa ukadinali.
Hata hivyo familia nyingine ya kitawa imeingia katika Baraza la makardinali kama ile ya Shirika la Ndugu wadogo wafransican wa Kikomventuali ambaye ni Frt. Mauro Gambetti, Msimamizi wa Komventi Takatifu ya Assisi na kufanya kuwa makardinali 51 watawa wa mashirika ambamo 29 wanayo haki ya kuchaguliwa katika uchaguzi wa upapa ujao na 22 hawana haki hiyo. Kati ya wawakilishi wa nchi mpya katika Baraza la Makardinali ni huko Brunei, Kardinali Mteule Cornelius Sim, Malta (Kardinali Mario Grech), eneo ambalo halikuwa na mwakilishi yoyote baada ya kifo cha Kardinali Prosper Grech na nchini Rwanda (Kardinali Antoine Kambanda). Kwa ujumla baada ya hao nchi zinazowakilishwa na makardinali ni 90.
Ilikuwa ni Dominika tarehe 25 Oktoba 2020 mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Papa aliwatangazia waamini na mahujaji wote waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro majina ya Makardinali wapya wateule 13 kutoka mabara tofauti ambao na ambao wanasimikwa rasmi katika kikao cha Baraza la Makardinali cha Jumamosi tarehe 28 Novemba 2020, katika mkesha wa Dominika ya kwanza ya Majilio. Makardinali 9 karibu hawajafikia miaka 80 na wanayo haki ya uchaguzi wa Papa wa wakati ujao
Majina ya Makardinali wapya wateule 13 ni: Kardinali mteule Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu; Kardinali mteule Marcello Semeraro, Rais wa Baraza la mchakato wa kuwatangaza watakatifu; Kardinali Antoine Kambanda, Askofu Mkuu wa Kigali (Rwanda);Kardinali mteule Wilton Gregory, Askofu Mkuu Washington (Marekani). Kardinali mteule José Advincula, Askofu Mkuu wa Capiz,(UFilippine); Kardinali mteule Celestino Aós Braco, Askofu Mkuu wa Santiago ya Santiago ya Cile;(Amerika ya Kusini); Kardinali mteule Cornelius Sim, Askofu wa Puzia ya Numidia na Msimamizi wa Kitume wa Brunei, Kuala Lumpur;(Asia); Kardinali Mteule Augusto Paolo Lojudice, Askofu Mkuu wa Siena-Colle Val d’Elsa-Montalcino (Italia);
Kardinali mteule Mauro Gambetti,(OFM)konv) Mfransikani wa Kikonventuali, na Msimamizi wa Comventi Takatifu na pia Jumuiya ya Wafransiskani Assisi. Katika orodha mpya hiyo pia kuna majina mengine 5 ya Makardinali wateule ambao ni Askofu na Askofu Mkuu na wengine watakaojiunga na Baraza la Makardinali hao: Kardinali mteule Felipe Arizmendi Esquivel, Askofu mstaafu wa Mtakatifu Cristóbal de las Casas(Mexico); Kardinali Mteule Silvano M. Tomasi, Askofu Mkuu wa Aslo, na Balozi wa Kitume; Kardinali Mteule Raniero Cantalamessa, Mkapuchini, na Mhubiri Mkuu wa Nyumba ya Kipapa; Kardinali Mteule Enrico Feroci, Paroko wa Madhabahu ya Bikira Maria wa Upendo wa Mungu(Castel del Leva),Italia.