杏MAP导航

Tafuta

Waraka wa kitume wa Fratelli tutti Waraka wa kitume wa Fratelli tutti 

Papa Francisko:Nafasi ya kwanza ni upendo na usihatarishwe!

Kila mtu anatakiwa kutambua kuwa nafas ya kwanza ni upendo na hautakiwi kuhatarishwa.Ni ujumbe wa Papa Francisko kwa njia ya mitandao ya kijamii, katika muktadha wa Waraka wake wa kitume wa Fratelii tutti au wote ni ndugu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika mitandao ya kijamii, Ijumaa, tarehe 9 Oktoba 2020, Papa Francisko ametoa ujumbe wake  na kusema “sisi sote waamini tunatakiwa kujua hili: nafasi ya kwanza kuna upendo, yaani suala ambalo halitakiwi kuwekwa hatarini ni upendo. Hatari zaidi ni ile ya kuokupenda (1Kor 13,1-13). Ni katika muktadha wa Waraka wake wa ‘Fratelli tutti’ yaani wote ' wote ni  ndugu. Aidha Papa anasema “ni upendo wa mwingine ambao unatusukuma kutafuta ubora zaidi wa maisha yake. Ni kwa njia ya kukuza mtindo  huo wa kuleta uhusiano ili kufanya uwezekane ule urafiki wa kijamii na ambao haubagui yoyote na udugu uliofunguliwa wazi kwa wote.

09 Oktoba 2020, 14:35