杏MAP导航

Tafuta

Tarehe 4 Oktoba 2019 wamewekwa wakfu maaskofu wateule katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Tarehe 4 Oktoba 2019 wamewekwa wakfu maaskofu wateule katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro 

Papa:Maaskofu pyaisheni maisha ya watu wa Mungu!

Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican tarehe 4 Oktoba 2019 Baba Mtakatifu amewaweka wakfu Maaskofu wateule: Antoine Camilleri,Askofu mkuu mteule Paolo Rudelli;Askofu mkuu mteule Paolo Borgia.Papa amekumbushia maana ya nafasi ya uaskofu kuwa ni kutoa huduma na siyo sifa.Wamehimizwa hata aina tatu za ukaribu wa kiaskofu na kuongezewa ya nne!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 4 Oktoba 2019 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro imeadhimishwa misa kwa ajili ya kuwekwa wakfu Maaskofu wakuu wateule ambalo Antoine Camilleri aliyekuwa ni Katibu mkuu Msaidizi wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican. Askofu mkuu mteule Paolo Rudelli aliyekuwa ni Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Ulaya. Askofu mkuu mteule Paolo Borgia, aliyekuwa ni Afisa mwandamizi Sekretarieti kuu. Baba Mtakatifu Francisko akianza mahubiri yake, kama ilivyo utamaduni wa amesema ni vema kutafakari juu ya uwajibikaji wa Kanisa ambao umewekwa kwa ajili ya hao ndugu. Bwana  wetu Yesu Kristo aliyetumwa na Baba ili kuwakomboa watu, aliwatuma kwa mara nyingine tena mitume kumi na mbili duniani, kwa maana wakiwa wamejazwa na nguvu ya Roho Mtakatifu wawe kutangaza Injili kwa watu wote na kuwaunganisha chini ya mchungaji mmoja, ili awatakatifuze na kuwaongoza katika wokovu.

Baba Mtakatifu anasema ili kuwa na mwendelezo  kizazi hadi kizazi cha huduma kama hiyo, mitume kumi na mbili waliwapokea wahudumu wengine na kuwawekea mikono yao kwa njia ya Roho waliyo ipokea kutoka kwa Kristo ambaye anaitimiza kwanjia ya sakrametni ya wakfu. Kwa njia hiyo maaskofu wote waliopita katika utamaduni huo wa Kanisa, wameendeleza kuhifadhi huduma hii ya kwanza na shughuli ya mwokozi ili kuendelea na kukua hadi katika nyakati zetu. Katika nafasi ya skofu kutoka kwa wakuhani wake, yupo katikati yao Bwana mwenyewe ambaye ni kuhani mkuu hata miele. Ni Kristo ambaye katika huduma ya uaskofu anaendelea kutangaza Injili ya wokovu na kutafatifuza waamini, kwa njia ya sakramenti ya imani. Ni kristo ambaye katika ubaba wa Askofu, anakuza viungo vipya vya mwili wake, ambao ni Kanisa. Ni Kristo ambaye kwa hekima na busara ya kiaskofu anaongoza watu wa Mungu katika hija hii duniani hadi kufikia furaha ya milele!

Kwa kuwapokea kwa furaha na shukrani hawa ndugu  ambao, kama maaskofu kwa kuwawekea mikono leo, wanaunganisha katika baraza la maaskofu. Hiyo ikiwa pia ni hao wataule wa Bwana ambao wanaangazwa na  wamechaguliwa kati ya waamini na kwa ajili ya waamini, wamechaguliwa si kwa ajili yao binafsi, bali kwa ajili ya mambo yanayotazama Mungu. Uaskofu ni jina la huduma na siyo la utukufu kwa sababu askofu anapaswa kuhudumu zaidi kuliko madaraka, kwa mujibu wa amri ya Mwalimu: “aliye mkubwa kati yenu, awe mdogo. Anayeongoza ni kama anayehudumia”

Baba Mtakatifu anawataka watangaze neno kwa kila fursa. Iwe muafaka na wakati usio muafaka. Watangaze Neno la kweli na siyo hotuba za kuchosha na ambazo hakuna mtu anaelewa bali watangzwe neno la Mungu. Wakumbuke kuwa, kwa mujibu wa Petro katika kitabu cha Matendo ya Mitume, kazi mbili msingi za maaskofu ni sala na kutangaza Neno la Mungu ( Mdo 6,4);  pia zinafuata shughuli nyingine za uongozi. Lakini zile mbili ndiyo nguzo anaisitiza Baba Mtakatifu Francisko. Kwa njia ya sala na sadaka kwa ajili ya watu, watachota katika kisima cha ukamilifu wa utakatifu wa Kristo ulio mwingi wa utajiri na neema za Mungu. Katika Kanisa ambalo wao wamekabidhiwa kulinda na kutoa mafumbo ya Kristo , kuwekwa kama Baba aliye kichwa cha familia yake kwa kufuata mfano wa Mchungaji mwema na ambaye anajua kondoo wake na katika yeye ametambuliwa na hakukosa kamwe kutoa maisha kwa ajili yake.

Ukaribu kwa watu wa Mungu. Baba Mtakatifu Francisko amerudia kuelezea juu ya ukaribu wa aina tatu wa Askofu. Kwanza ukaribu na Mungu katika sala, ndiyo kazi ya kwanza; ukaribu na makuhani katika baraza la makuhani; ukaribu na watu wa mungu. Aidha wasisahau kwamba wamechukuliwa na wamechaguliwa kutoka katika zizi. Wasisahau hata mizizi yao; ya wale ambao wamewarithisha imani yao, na ambao wamewapatia utambulisho. Wasisaliti watu wa Mungu. Baba Mtakatifu Francisko amekazia kuwa, wawapende kwa upendo wa ubaba na kindugu wale wote ambao Mungu anawakabidhi. Hawali ya yote makuhani, mashemasi wao na wahudumu wengine katika huduma; lakini zaidi wawapende maskini, wale wasio kuwa na mlinzi na wenye kuhitaji kukaribishwa na kusaidiwa. Wawashauri waamini katika kushirikiana kwenye jitihada za kitume na kuwa na shauku ya kuwasikiliza.

Baba Mtakatifu katika mahubiri hayo aidha amewaomba wawe makini na wale ambao hawashiriki katika zizi moja la Kristo, kwa sababu hata hao wamekabidhiwa na Bwana pia. Wakumbuke kwamba Kanisa Katoliki, linalokusanyika katika mfungamano wa upendo mmoja  na wao wameunganika katika baraza la Maaskofu hivyo na hii  ni kama ukaribu wa aina ya nne, ambapos wanapaswa kuhamasisha katika makanisa yote kukaribisha kwa ukarimu wale ambao wanahitaji msaada.  Aidha walinde zawadi hiyo ambayo wameipokea ya kuwekwa wakfu kwa njia ya kuwekewa mikono na maaskofu wote. Wakeshe kwa upendo kwa zizi zima ambalo Roho Mtakatifu anawapatia kusimamisha Kanisa la Mungu. Wakeshe kwa jina la Baba  na ambaye  wao wapo kwa sura zao; kwa jina la Baba na la Mwana ambalo wao wamewekwa kuwa walimu,  mapadre na wachungaji; na hatimye katika Roho Mtakatifu anayetoa maisha kwa Kanisa na nguvu inayowasaidia udhaifu wetu.

05 Oktoba 2019, 09:37