Talitha Kum,huruma na hatua ya matendo ya kukomesha biashara haramu ya binadamu
Na Sr Bernadette M. Reis;Pauline Sisters na Angella Rwezaula – Vatican.
Mtandao wa Watawa wa Talitha Kum Asia ulifungua Mkutano wake wa Kikanda mnamo tarehe 26 Agosti 26 katika Hoteli ya Erian katikati mwa Jakarta, nchini Indonesia ikiwaalika wajumbe 60—Watawa wa kike wa Mashirika, washirika, na mabalozi wa vijanakutoka nchi 16 za Asia kutafakari mada: "Huruma Katika Vitendo: Kukomesha Biashara Haramu wa Binadamu." Mkutano huu wa siku tano, ambao ulihitimishwa mnamo Agosti 30, ulionesha nguvu ya watawa wa Kikatoliki, vijana, na ushirikiano wa watawa katika kushughulikia moja ya migogoro ya haki za binadamu barani Asia. Sr Prisca, ADM, rais wa Chama cha Wanawake Watawa nchini Indonesia, aliwakaribisha washiriki kwa uchangamfu, huku akisisitiza dhamira isiyoyumba ya wanawake wa Wawa wa Kikatoliki kuwa mstari wa mbele wa mapambano dhidi ya Biashara haramu ya binadamu, pamoja na kuongezeka kwa ushirikiano na washirika watawa mbalimbali wanaofanya kazi kwa ajili ya haki na wa hadhi ya binadamu.
Biashara Haramu ya Binadamu Barani Asia:Mgogoro Unaokua
Barani Asia inasalia kuwa kitovu kikuu cha biashara haramu ya binadamu. Kulingana na Shirika la Kazi Duniani, zaidi ya watu milioni 25 duniani kote ni waathiriwa wa kazi za kulazimishwa, na idadi kubwa katika eneo la Asia-Pasifiki, kutokana na uhamiaji usio salama, umaskini, unyonyaji wa kidijitali, na ulinzi dhaifu wa kitaasisi. Katika Asia ya Kusini-mashariki pekee, maelfu ya watu wananaswa katika unyanyasaji wa kingono na ulaghai wa mtandaoni kila mwaka, mara nyingi na mitandao ya uhalifu ya kimataifa iliyopangwa vizuri. Sr Abby Avelino, MM, mratibu wa kimataifa wa Talitha Kum, aliripoti kwamba mwaka 2024, mtandao huo ulifikia karibu watu milioni moja kupitia shughuli za kuzuia, elimu, usaidizi wa manusura na shughuli za utetezi. "Dhamira yetu si kuokoa tu," alisema, "lakini pia kutoa changamoto kwa mifumo, kutetea hadhi ya binadamu, na kuwaweka katikati waathirika."
Kuwasikiliza Walionusurika
Ushuhuda wa kusisimua wa mwathiriwa uliwakumbusha wajumbe kuhusu hali halisi aliyoishi: "Wasafirishaji haramu wanafanya kazi kuvuka mipaka kama mtandao wenye nguvu. Mtandao wa Talitha Kum lazima uwe na nguvu zaidi kupitia neema ya Mungu." Wajumbe walisisitiza haja ya huduma ya kiwewe, usaidizi wa muda mrefu, kupunguza unyanyapaa, uongozi wa vijana, na ushirikiano wenye nguvu-sio tu ndani ya mitandao ya Kikatoliki lakini pia katika imani na mataifa-ili kusawazisha ufikiaji na uratibu wa shughuli za usafirishaji haramu wa binadamu.
Mpango wa Utendaji, Mwitikio wa Imani
Mkutano huo uliwasilisha mpango kazi wenye vipengele sita, unaokita mizizi katika maadili ya Kikatoliki:
1. Kutoa usaidizi kamili kwa walionusurika.
2. Kuhakikisha usindikizaji wa muda mrefu.
3. Kuimarisha ushirikiano wa kuvuka mpaka na dini mbalimbali.
4. Kupambana na unyanyapaa kupitia elimu.
5. Kuwezesha uongozi wa vijana.
6. Kujenga mitandao yenye nguvu zaidi ya kikanda inayoongozwa na Watawa na watetezi walionusurika.
Kuongozwa na Injili
Kwa msukumo wa Nyaraka za Fratelli Tutti na Laudato Si’, Sr Dada Paula Phonprasertruksa, SPC, mratibu wa eneo la Talitha Kum Asia, aliwaalika washiriki wote kukumbatia uongozi wa watumishi: "Tuwe viongozi wanaosikiliza, kutumikia, na kutenda kwa ujasiri." Tukitazama siku za usoni, dhamira ya Talitha Kum Asia inabakia kuwa wazi: kusuka mitandao ya matumaini—inayoongozwa na watawa wa Kikatoliki, ikiimarishwa na mshikamano wa kitawa na yenye mizizi katika huruma. Mkutano huo ulihitimishwa tarehe 30 Agosti 2025 kwa adhimisho Takatifu la Ibada ya Misa iliyoongozwa na Kardinali Ignatius Suharyo, Askofu Mkuu wa Jimbo la Jakarta, huku akithibitisha tena dhamira ya dhati ya Kanisa katika kutetea utu, kuandamana na waokokaji, na kujenga ulimwengu ambapo kila mtu yuko huru, anaheshimiwa na yuko salama. Kwa njia ya imani, uthabiti, na umoja wa moyo, Kanisa linaendelea kuitikia wito wa Kristo anayesema : “Talitha Kum—Msichana mdogo, nakuambia, Inuka”(Marko 5:41).
Mtandao wa Talitha Kum
Mtandao wa Kimataifa wa Mashirika ya Kitawa dhidi ya Biashara Haramu ya Binadamu Ni TALITHA KUM. Jina la Mpango huo linatokana na maneno ya Biblia, "Talitha Kum. 'Msichana mdogo, nakuambia, Inuka!'" (Mrk5:41). Maneno haya yanakaribisha mitandao yote kusimama pamoja na waathiriwa na waathirika wa biashara haramu ya binadamu. Tunajali ubinadamu waliojeruhiwa na unyonyaji na kuchukua hatua dhidi ya ukosefu wa usawa unaosababishwa na mifumo ya kiuchumi na kiutamaduni.
Utambulisho
Talitha Kum ilianzishwa rasmi mwaka 2009 kama mpango wa Kimataifa dhidi ya biashara haramu ya binadamu na unyonyaji, ambap umepangwa katika mitandao zaidi ya 60 ya ndani katika takriban nchi 90, ikisaidia kikamilifu waathiriwa, walionusurika na watu walio katika mazingira magumu. Kila mtandao wa Talitha Kum hudumisha utambulisho wake wa kipekee na hufanya kazi ndani ya nchi au eneo lake, wakati Kamati ya Uratibu ya (UISG) inasaidia kujenga uwezo na mafunzo ya mitandao na wanachama wake, kuwezesha kushiriki habari, rasilimali, na uzoefu.
Utume
Dhamira ya Talitha Kum ni kukomesha biashara haramu ya binadamu kupitia mipango shirikishi inayolenga kuzuia, ulinzi, ujumuishaji upya wa kijamii, na urekebishaji wa walionusurika, ukaribu na utetezi, na kukuza vitendo vinavyoshughulikia sababu za kimfumo. Tunaratibu juhudi za Watawa kupambana na biashara haramu ya binadamu, kuwezesha mitandao, mawasiliano, na mafunzo, kwa mujibu wa mpango mkakati wa UISG na mafundisho ya mafundisho ya kijamii ya Kanisa Katoliki.
Kwa maelezo zaidi tembelea mtandao huu wa kimataifa: