Papa Leo XIV awasha mwenge kwa ajili ya maandamano ya mbio za mwenge kutoka Roma hadi Lecco
Vatican News
Mwenge uliowashwa asubuhi, ya tarehe 3 Septemba 2025 na Papa Leo XIV wakati Katekesi yake katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, sasa uko njiani kuelekea Lecco. Mwenge huo unabebwa na wakimbiaji wapatao hamsini, vijana kwa wazee, ambao kwa siku chache zijazo watasafiri zaidi ya kilomita 600 wakitenganisha Mji wa Milele kutoka mji wa Ziwa Como, wakisimama huko Rieti, Prato Vecchio, Massa Carrara, na Piacenza.
Tamaduni tangu 1975
Mashindano ya mbio za Mwenge Roma-Lecco ni mpango unaoandaliwa kila baada ya miaka kumi tangu 1975 (isipokuwa mwaka 2000 tu kwa sababu ya Jubilei) na parokia ya Mwenyeheri Serafino kwa Wilya za Lecco ya Chiuso na Maggianico.
Wajibu na Zawadi
"Mwenge unawakilisha jukumu, lakini wakati huo huo zawadi iliyokabidhiwa kwetu na Baba Mtakatifu," alieleza Gianluca Castelnuovo, mratibu wa hafla hiyo ya kimichezo ya kidini wakati akihojiana na Vatican News. “Tumekabidhiwa utume wa kupeleka ujumbe kwa jumuiya yetu, yaani,” alilisisitiza mratibu huyo mbio za marathoni, “kuwa mashahidi wa maisha ya Kikristo katika maisha yetu ya kila siku.”
Toleo Lingine kwa Vijana
Maandamano ya mwanga wa mwenge huo, yaliyozaliwa kutokana na utamaduni wa muda mrefu uliochochewa na mila ya Shirika la Waambrosian na ambayo ni "fursa kwa jumuiya mbalimbali mahalia zinazokaribisha wakimbiaji katika kila hatua ya kukutana," na wakati huo huo, huko Castelnuovo, "toleo ni kwa vijana wa parokia yetu,” alifafanua. Wakimbiaji hao hamsini wanajikita na kutembea kwa kilomita 120-140 kila siku, wakifuatiwa na gari la kusindikiza na baiskeli kuwasaidia. Kila mkimbiaji anakimbia kilomita moja kabla ya kukabidhi mwenge kwa mkimbiaji mwingine. "Leo, wajukuu wa wale walioanza tamaduni hii mwaka 1975 wanashiriki," alihitimisha mratibu huyo kwamba, "lakini pia kuna wale ambao walikuwa na umri wa miaka kumi na sita miaka 50 iliyopita na bado wanakimbia hadi leo. Ni mpango mzito; fikiria tu kwamba kwa mwanamke kijana ambaye alishiriki katika maandamano ya mwenge mwaka 1985, ilikuwa ni fursa ya kibinafsi ya kuingia katika nyumba ya kiroho ambayo baadaye alianzisha safari yake ya kiroho katika Konventi."