Kuelekea Kutangazwa kuwa Mtakatifu Pier Giorgio Frassati
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika matayarisho ya kutangazwa Mwenyeheri Pier Giorgio Frassati kuwa Mtakatifu, tukio litakalofanyika tarehe 7 Septemba 2025, Kitengo cha Chama cha Matendo ya Kikatoliki cha Italia kimetangaza safari ya tafakari na sala ambayo itahitimishwa na mkutano wa hadhara utakaoongozwa na kauli mbiu: "Ndani ya Maisha, Ndani ya Historia: Utakatifu wa Pier Giorgio Frassati," uliopangwa kufanyika Jumamosi, tarehe 6 Septemba 2025, saa 11:00 jioni jijini Roma, katika Ukumbu Mkuu wa Chuo Kikuu Uria (LUMSA) kilichopo Njia ya (Borgo Sant'Angelo, 13).
Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa Kitaifa wa Chama cha Matendo ya Kikatoliki, Giuseppe Notarstefano, na kutakuwa na hotuba ya Mwadhama Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza la Watakatifu. Tafakari itafuata kutoka kwa Roberto Falciola, makamu Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza wWtakatifu, kuhusu: Pier Giorgio na urafiki; Luca Liverani, mwandishi wa habari wa Avvenire, na Rosanna Tabasso, rais wa Sermig, kuhusu: Pier Giorgio na kujitolea kwake kwa amani; Tatiana Giannone, Rais wa Libera, kuhusu: Pier Giorgio na kujitolea kwake kwa haki ya kijamii. Gennaro Ferrara, mwandishi wa habari wa TV2000, atasimamia mkutano huo.
Siku itaendelea saa 2:30 usiku kwa Mkesha wa sala kwa ajili ya maandalizi ya kutangazwa kuwa Mtakatifu,itakayoongozwa na Askofu Claudio Giuliodori, Msimamizi wa kikanisa wa Chama cha Matendo kikatoliki Kitaifa ( AC,) katika Basilika ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji wa Fiorentini(Kupitia Acciaioli, 2).
Kutangazwa kuwa watakatifu Frassati na Acutis
Dominika tarehe 7 Septemba 2025, Baba Mtakatifu Leo XIV anatarajia kuwatangaza wenyeheri, Pier Giorgio Frassati na Carlo Acutis kuwa Watakatifu.