杏MAP导航

Tafuta

2025.09.07 Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya Kutangazwa Watakatifu Acutis na  Frassati. 2025.09.07 Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya Kutangazwa Watakatifu Acutis na Frassati. 

Frassati "alikuwa kaka kweli"aliyetangazwa kuwa Mtakatifu na Papa Leo XIV

Ushuhuda wa vijana wa Chama cha Matendo ya Vijana Wakatoliki:Kutangazwa kuwa Mtakatifu,kunaadhihirisha umuhimu wa Pier Giorgio Frassati,aliyeyaita maisha kuwa "furaha kupitia maumivu"akionesha kwamba amani na matumaini huzaliwa kutoka katika mpenzi anayesema"ndiyo"kila siku kwa Mungu na kwa wengine.

Eleanna Guglielmi na Angella Rwezaula – Vatican.

1925: Jubilei ya Amani. 2025: Jubilei ya Matumaini. Katikati, karne ya migogoro, vita, na mpasuko. Kijana kutoka Torino, Italia, aliyefariki akiwa na umri wa miaka ishirini na minne, anashikilia Jubilei hizi mbili pamoja. uyu ni Pier Giorgio Frassati ambaye aliishi kama rafiki wa Kristo na ndugu kwa kila mtu, kwa jina na jina. Je, alikuwa  kijana wa aina gani huyu ambaye Papa Leo XIV amemwandikwa katika kitabu cha watakatifu tarehe 7 Septemba?

Sauti  kutoka Chama cha Matendo ya Kikatoliki nchini Italia, zaidi, wahusika wakuu katika tasnifu hiyo, zinasimulia historia yake kutoka Italia, Hispania na Argentina. Vijana na wanaowajibika humwita ndugu na mwalimu wa maisha ya kila siku: hali ya kawaida ambayo inakuwa utakatifu, sala ambayo inainama kwa Mungu na kwa ndugu, siasa kama upendo.

Amani gani?

Jeneza lililopitia Torino  mnamo tarehe 6 Julai  1925, lilisindikizwa sio na watu mashuhuri, lakini na umati usiojulikana wa watu masikini. Miaka mia moja baadaye, kutangazwa kuwa Mtakatifu si ibada ya wateule walio wachache, bali ni ukumbusho wa hadharani wa kijana aliyeichukua Injili kwa uzito na bila kuyumba yumba. Frassati alikufa katika Mwaka Mtakatifu wa Amani na akawa Mtakatifu katika Mwaka Mtakatifu wa Matumaini. Enzi mbili za mbali, lakini ambazo zimeunganishwa na swali ambalo bado linatafuna akili za watu kwamba: ni aina gani ya amani ambayo inawezekana kutumaini?

La tomba di Pier Giorgio Frassati a Torino

Kaburi la  Pier Giorgio Frassati huko Torino

Alikuwa katika mapenzi

Ni nani huyu kijana anayezungumza nasi miaka mia moja baadaye? Sio sanamu au shujaa wa kufikirika. "Kwetu sisi, yeye ni kaka wa kweli," walisema vijana wa  Chama cha Matendo katoliki, ambao walichukua jukumu muhimu katika maoni hayo. Si peke yake, lakini pamoja na mashirika mengine ya kikanisa kama(FUCI,) Shirikisho vya Vijana wakatoliki wa Vyuo Vikuu,  Dominika, Vicentians, “Shady Guys,” na Majimbo ambao wanachukua  kama kijiti chake cha kupitisha na kukipyaisha siku hadi siku. Kutoka upande mmoja wa dunia hadi mwingine, kutoka Italia hadi Argentina kupitia Hispania, na  urithi wake unaendelea kuvuma. "Habari za kutangazwa kwake kuwa Mtakatifu zilishangaza wakati wa Mkutano Mkuu wa  Kitaifa la 2024," alikumbuka Lorenzo Zardi, makamu rais wa Chama cha Matendo Kikatoliki (AC) cha Vijana Italia. "Kuanzia wakati huo, tulianza kufurahi: ilikuwa habari iliyosubiriwa kwa muda mrefu."

Kwa ajili yake, Frassati ni mpenzi wa Kristo na mikono yake katika unga wa historia: "Njia yake ya utakatifu ni uaminifu kwa sasa, kuishi Injili katika maisha ya kila siku. Hakuwa mfadhili, lakini kijana ambaye hakuwangojea maskini kuwa majirani: alikwenda kwao mwenyewe." Na matendo mema yaliyofanywa kutokana na misukumo ya ukarimu hayakumtosha: alitaka ishara zenye uwezo wa kuleta manufaa zaidi. Mwanafunzi ambaye alichagua "kumtumikia Kristo kati ya wachimba migodi," kijana aliyeishi siasa kama shauku ya kiraia, "siku zote katika huduma ya manufaa ya wote, kuanzia na wasio na bahati. Urafiki ambao ulikuwa msingi wa amani." Kwa sababu hiyo alisema Zardi, maandalizi ya kutangazwa kuwa Mtakatifu yalikuwa ni "mafunzo ya moyo": mahujaji kwenye Njia za Frassati, nafasi ya makumbusho huko Torino, uchapishaji wa kitabu "Sababu Takatifu. Na Frassati katika barabara hadi kwa aliye Juu". Tuliendelea kuwaambia vijana kile ambacho sisi pia tulikuwa tumegundua tena kwa kutafakari juu yake."

Lorenzo Zardi, vicepresidente nazionale per il settore giovani ACI

Lorenzo Zardi, Makamu rais wa Chama cha Matendo Kikatoliki,cha Italia kitengo cha vijana wadogo(ACI).

Siku ya Jumatatu Mtakatifu

Kwa upande wa Agnese Palmucci, mkuu chama cha Vijana katoliki ( AC) huko Roma, alisema: "Frassati kama ndugu,  si mtakatifu wa mbali. Kijana wa kweli, wa kawaida ambaye anatuonesha utakatifu wa maisha ya kila siku. Tunajiambia: sisi ni watu wa Jumatatu. Kwa sababu Dominika  lazima iendelee kila siku. Na yeye ndiye mtakatifu wa Jumatatu ambaye anatuonesha jinsi ya kutakasa kila siku." "Uzuri wake ni kwamba anatuonesha chanzo cha kazi yake yote. Bila chanzo hicho, hata kujitolea kwa ushirika ni utupu." Na tena: "Urafiki wake ulikuwa mwili, upendo wake umefichwa. Katika mazishi yake, umati wa watu maskini uliwaambia wazazi wake yeye alikuwa nani hasa. Alikasirishwa na ukosefu wa haki, hakuinama kwa ufashisti, lakini daima aliweka macho yake juu. Bado anatupatia changamoto leo: si mtakatifu kwenye madhabahu, lakini mfano halisi unaotusukuma kusema: Nataka kuwa hivyo pia." Jijini Roma, kumbukumbu yake ilifanyika ya maonesho ya kusafiri katika parokia na mikutano yakizingatia barua zake. Ndani yake, anasema Agnese, "tunaona kwamba sala inainama kwa Mungu na kwa ndugu yetu, kwa sababu yeye na mimi ni sawa, ndugu".

Giovani dell'Azione Cattolica di Argentina

Vijana wa Chama cha matendo Katoliki cha Argentina

Kutoka milimani hadi ulimwengu wa kidijitali

Kutoka Buenos Aires, Claudia Carbajal, rais wa AC Argentina, alisisitiza "Jambo muhimu cha urithi wake: kutuonesha kwamba urafiki ulioanzishwa katika Kristo ni njia ya utakatifu wa pamoja." Sio tu kama watu wa kawaida waliojishughulisha na wakati wao, lakini kama watu waliobatizwa walizama katika ukweli halisi. Katika matayarisho ya kutawazwa kuwa mtakatifu, vijana wa Argentina wanatayarisha wiki ya ushuhuda na podikasti ya kusindikiza sherehe hiyo.

Kutoka Hispania, Daniel Díaz Rincón Muelas, mkuu wa sekta ya vijana wa AC, alisema: "Tunaipitia kwa furaha kubwa: kwetu sisi, ni fursa kwamba kijana kutoka Chama hiki cha matendo ya ya kikatoliki kuinulia altareni. Ujumbe wake ni wazi: kuwa Mkristo katika moyo wa maisha ya chuo kikuu, kwa ujasiri wa kutangaza imani katika mazingira yasiyofaa, kukuza mazingira ya pamoja ya vijana, kushiriki katika jumuiya ya pamoja, kuishi pamoja, kijana: mtu anayesoma, mpenda milima, mwenye shauku ya Ekaristi, na karibu na maskini. Ninavutiwa na ukweli kwamba wao, maskini wa Torino, walikuwepo kwenye mazishi yake."

Giovani dell'Azione Cattolica spagnola

Vijana wa Matendo Katoliki, wa Hispania.

Pamoja na mtu wa Heri nane

Mnamo Septemba 6, huko Roma, Chama cha matendo ya Kikatoliki cha Italia kiliandaa mkutano kuhusu: "Ndani ya Maisha, Ndani ya Historia. Utakatifu wa Pier Giorgio Frassati" katika Ukumbi wa Mtakatifu Pio X, uliozingatia njia tatu: urafiki, amani, na haki ya kijamii. Jioni, hiyo pia kulikuwa na mkesha wa maombi katika Kanisa la Mtakatifu Maria huko Traspontina, ukiongozwa na Askofu Claudio Giuliodori. Injili ya Heri za Mlimani ilisomwa, kwa sababu, kama Askofu wa Krakow, yaani Matakatifu Yohane Paulo II alivyo mwita Frassati kuwa alikuwa "mtu wa Heri nane." Hii ilifuatiwa na ibada ya Ekaristi, urafiki wa kimya na Kristo, na maombezi kwa ajili ya vijana, maskini, na amani. "Walibaki  mbele ya Yesu kama Pier Giorgio alivyokuwa, wakisikiliza maneno yake kuhusu amani na urafiki na Bwana.

Amani inatuacha na wasiwasi

"Mimi ni maskini kama maskini wote," Frassati alisema. Si pozi, bali utambulisho unaotuacha tukiwa na wasiwasi, ambao unavunja vizuizi vya kijamii, kitamaduni na kisiasa. “Ubinadamu ulikuwa tatizo lake,” aliandika dada yake Luciana. Hiyo  haikuwa hotuba ya mawazo, lakini mawasiliano: kuwapa wengine haki yao ya kuzaliwa, kama kaka na dada, kama wana na binti. Sio matumaini, lakini furaha ipitayo mateso. Moja ya nukuu zake zimechapishwa kwenye fulana za vijana wa Roma: "Unaniuliza ikiwa nina furaha? Na ningewezaje kuwa?" Frassati aliandika. Kwa Frassati, hii ni tumaini, hii ni amani: kuegemea kwa Mungu na kwa kaka na dada zako, kubadilisha sala kuwa maisha, siasa kuwa upendo wa kisiasa na kwa hivyo swali kuu: ni "ndiyo" iliyofichwa tuko tayari kusema, ili tumaini liwe mwili na amani isibaki kuwa neno tu?

Giovani e adulti dell'Azione Cattolica spagnola

Vijana na watu wazima wa Chama cha matendo Katoliki Hispania.

Ushuhuda wa Frassati
Ushuhuda wa Sr Tadea
08 Septemba 2025, 10:34