杏MAP导航

Tafuta

2025.08.14 Chuo cha Mtakatifu José cha Watawa wa Josephine. 2025.08.14 Chuo cha Mtakatifu José cha Watawa wa Josephine. 

Nicaragua:Serikali yanyakua Chuo cha Mtakatifu José cha Masista wa Josephine

Serikali ya Daniel Ortega na Rosario Murillo imetaifisha jengo hilo,ikilituhumu kuwa lilikuwa eneo la uhalifu wa zamani.Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imejibu kwa ukali.

Vatican News

Serikali ya Nikaragua ya Daniel Ortega na Rosario Murillo imetaifisha rasmi Chuo cha Mtakatifu José huko Jinotepe, Milayani Carazo, shule yenye umri wa miaka 40 inayosimamiwa na Shirika la  Masista wa Josephine. Kulingana na Rosario Murillo, watawa hao, kama ilivyoripotiwa na shirika la habari la EFE, wanahusika na "uhalifu" wakati wa maandamano ya 2018. Rais huyo mwenza alidaiwa kudai kwamba wana Sandinista "waliteswa na kuuawa" katika kituo hicho wakati wa maandamano ya kuipinga serikali yaliyozuka mnamo Aprili 2018. Murillo alisema zaidi kwamba shule hiyo kuanzia sasa itaitwa kituo cha elimu cha "Bismarck Martínez", kwa heshima ya mwanamgambo wa Sandinista aliyeuawa wakati wa maandamano hayo hayo.

Shughuli za watawa

Uamuzi huo, kulingana na tovuti huru ya Despacho 505, ulilaaniwa na mtafiti wa kidini Martha Patricia Molina, ambaye alimshutumu rais mwenza kwa kukashifu waamini. Alieleza kwamba watawa hao, "tangu walipoishi Nicaragua mnamo Februari 1915, wamewaelimisha wavulana na wasichana katika maadili ya Kikristo na ya kibinadamu yanayotegemea upendo wa jirani na mazoezi ya upendo."

Hukumu ya Marekani

Kutoka Washington, Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ya Masuala ya Ulimwengu wa Magharibi, kupitia akaunti yake ya X, ilisema unyakuzi huo ulioamuliwa na serikali ya Nicaragua "uthibitisho zaidi kwamba upotovu wa udikteta wa Murillo-Ortega hauna kikomo."

Hii si mara ya kwanza kwa Managua kunyakua mali ya shirika la Kitawa au Kanisa Katoliki. Mnamo  Januari iliyopita, majengo mawili yanayomilikiwa na Kanisa Katoliki nchini Nicaragua: Seminari ya Mtakatifu Alois Gonzaga, katika Jimbo Katoliki la  Matagalpa kaskazini mwa nchi, na kituo cha mafungo cha La Cartuja, vilipokonywa na serikali ya Ortega-Murillo. Baada ya muda, maaskofu na mapadre wengi walikamatwa na kufukuzwa shuleni, na pia marufuku ya utendaji na maandamano ya kidini.

18 Agosti 2025, 14:46