杏MAP导航

Tafuta

Askofu Mkuu Peter Chung Soon-twa Korea Kusini akiwa katika kambi la vijana nchini Korea. Askofu Mkuu Peter Chung Soon-twa Korea Kusini akiwa katika kambi la vijana nchini Korea. 

Maaskofu Nchini Korea: 'Ukimbie uovu na utende mema;utafute amani na uifuate!

“Baada ya miaka 35 ya mateso wakati wa ukoloni wa Japan,taifa letu hatimaye lilipata ukombozi kutokana na majaliwa ya Mwenyezi Mungu na ulinzi wa Bikira Maria.Kwa bahati mbaya,furaha ya ukombozi ilikuwa ya muda mfupi na mgawanyiko uliofuata unaendelea kusababisha maumivu hadi leo."Ni maneno ya Maaskofu wa Korea wakati wa kuadhimisha miaka 80 baada ya migawayiko ya Peninsula ya Korea mbili itakayofanyika tarehe 15 Agosti 2025.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika ujumbe uliotayarishwa kwa ajili ya tukio la maadhimisho ya Miaka 80 tangu mgawanyiko wa Peninsula ya Korea, kufuatiwa na mauaji ya Vita vya Korea, Tume Maalum ya Upatanisho wa Kitaifa ya Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Korea, jumuiya ya kikanisa ya Korea Kusini imekumbatia hamu ya kudumu na ya uchungu ya umoja wa watu ambao leo hii wametenganishwa na kuwekwa chini ya serikali mbili tofauti. Katika ujumbe huo wanabainisha kuwa: "Tutaunga mkono na kushiriki kikamilifu katika mabadilishano na Korea Kaskazini kulingana na ushirikiano na usawa. Tutaunganisha nguvu kufanya kazi pamoja na wale wote wanaotamani Kaskazini na Kusini waishi pamoja katika 'nyumba ya pamoja.'  Kwa njia hiyo ni kumbatio ambalo pia limeonesha katika dhana ya ahadi madhubuti. Kauli mbiu ya Ujumbe huo imechukuliwa kutoka maneno kutoka Zaburi 34: "Ukimbie uovu na utende mema; utafute amani na uifuate."  Tarehe iliyo chini ya maandishi hayo imewekwa tarehe 15 Agosti 2025, katika Sherehe ya Kupalizwa kwa Bikira Maria Mbinguni ambaye ni mlinzi wa Kanisa la Korea.

Baada ya miaka 35,bado mateso yanaendelea!

Katika hati hiyo inabainisha: “Baada ya miaka 35 ya mateso wakati wa ukoloni wa Japan, taifa letu hatimaye lilipata ukombozi kutokana na majaliwa ya Mwenyezi Mungu na ulinzi wa Bikira Maria. Kwa bahati mbaya, furaha ya ukombozi ilikuwa ya muda mfupi, na mgawanyiko uliofuata unaendelea kusababisha maumivu hadi leo." Mnamo tarehe 25 Juni 1965, Tume Maalum ya Upatanisho wa Kitaifa ya Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Korea ilianzishwa kama "Siku ya Kuombea Kanisa la Kimya, ambayo ikawa Siku ya Maombi ya Upatanisho na Umoja wa Kitaifa mnamo 1992.” Kwa njia hiyo kila mwaka, karibu na tarehe hiyo, mipango na Misa huongezeka ili kuomba uponyaji wa majeraha ambayo bado hayajapona kikamilifu na kuombea Kanisa la Kaskazini."

Shukrani kwa Tume  ya upatanisho Kitaifa nchini Korea

Ijapokuwa miaka ya 1990 iliona vipindi vya maendeleo katika mazungumzo na ushirikiano kati ya Kaskazini na Kusini, ya Korea kwa mara nyingine ilijikuta ikiwa imesimama kabla hatujaweza kulima mashamba kwa 'jembe na mundu', maaskofu wanaeleza katika ujumbe wao. Ujumbe huo unasisitiza kuwa: “Shukrani kwa Tume za Kitaifa za Upatanisho zilizoanzishwa katika kila Jimbo, Kanisa la Korea, limeanza kutoa usaidizi mpana na wa pande nyingi kwa Wakorea Kaskazini wanaokabiliwa na matatizo kutokana na majanga ya asili na matatizo ya kiuchumi, likiendeleza kikamilifu kubadilishana kwa njia ya mazungumzo.”

Kanisa linaitwa kufanya kazi ya amani

“Kwa mfano wa Yesu Kristo, ambaye alipata amani ya kweli kwa kujitoa nafsi yake, Kanisa linaitwa kufanya kazi ya kupitisha ufalme wa amani kwa vizazi vijavyo, amani ambayo haitokei kwa kuwatiisha wengine kwa silaha na nguvu za kijeshi, katika hali ya kutoaminiana na chuki.” Hatimaye Maaskofu wanawaalika waamini kusali ili neema ya Mungu iweze kuponya machungu ya mifarakano. Katika Mwaka Mtakatifu (2025) unaokwenda sanjari na kumbukumbu ya miaka themanini ya mgawanyiko huo, ujumbe unawaalika Wakorea wote kuamini upendo na neema ya Mungu, kama “Mahujaji wa Matumaini." Mtu anaweza "kutumaini," Tume inatukumbusha, kwa sababu "kisichowezekana kulingana na maslahi na mantiki ya dunia kinawezekana kulingana na mapenzi ya Mungu." Na ikiwa Papa Francisko aliifafanua Dunia kujeruhiwa na kuwa hatarini, pamoja ni “nyumba ya pamoja” ya wanadamu, vivyo hivyo, “katika maadhimisho ya miaka 80 ya mgawanyiko, Maaskofu wanajitolea “kukimbia mbali na maovu na kufanya mema, kutafuta amani na kuifuata” (Zaburi 34:15) katika Ghuba ya Korea.

Ujumbe wa Maaskofu wa Korea
11 Agosti 2025, 16:07