Vijana watajiunga na hija ya Jimbo Kuu la Roma kwenda Lourdes!
Vatican News
Kwa mara ya kwanza katika utamaduni wa Jimbo Kuu la Roma, katika hija ambayo uhandaliwa na Kazi ya Hija ya Roma (Opera Romana Pellegrinaggi,) wataungana shukrani kwa Ofisi ya Jimbo Kuu, kwa ajili ya Uchungaji wa Vatican, hata vijana 150 wenye umri kuanzia miaka 16 hadi 28. Vijana hao watasafiri kwa Mabasi tarehe 28 Agosti 2025 na kurudi jijini Roma kunako tarehe 2 Septemba 2025. Katika mji wa Ufaransa vijana hao watakuwa na kikundi cha watu wazima ambao watafika katika madhabahu ya Mama Maria kwa ndege tarehe 29 Agosti 2025 na kubaki huko hadi tarehe Mosi Septemba.
Kunako 1858, Bikiria Maria alimtokea kijana Bernadette katika Groto ya Massabielle.
Vituo vya Njia ya Msalaba viliandikwa na Vijana
Kwa njia hiyo Mahujaji mia sita watasindikizwa na Kardinali Baldo Reina, Makamu wa Papa, Jimbo kuu la Roma. Sr Rebecca Nazzaro, mkurugenzi wa 'Opera Romana Pellegrinaggi' (ORP), pia atakuwa pamoja na kundi hilo. Kwa upande wake alishangazwa na ushiriki wa vijana kwa shauku katika mpango huo: "Mwitikio kutoka kwa vizazi vichanga umekuwa mkubwa sana, kiasi kwamba tulilazimika kusitisha hata usajili," alitoa maoni yake katika taarifa kutoka Vicariate ya Roma. Kwa kuongeza: "Itakuwa vizuri sana kuomba pamoja na kikundi kingine; shughuli nyingi zitafanywa pamoja, wakati zingine zitakuwa tofauti. Sr Nazzaro alisisitiza kwamba, Vituo vya Njia ya Msalaba "viliandikwa na vijana, na pia wameandaa sherehe ya mwisho ya kushiriki na kikundi." Kwa kuzingatia mafanikio ya muundo huo mchanganyiko, unaoleta pamoja vijana na watu wazima, ‘Opera Romana Pellegrinaggi’ inazingatia kurudia muundo huu kwa hija nyingine. "Tunaweka kituo chetu kikubwa katika huduma ya programu maalum kwa ajili ya vijana kwa bei nafuu sana, na kuwapa fursa ya kushiriki. Kwa sababu hija, kama Papa Leo XIV alivyosema huko Tor Vergata, Roma "ni chombo kikubwa cha uinjilishaji, urafiki, na udugu," alihitimisha mkurugenzi huyo wa ORP.
Ratiba ya pamoja ya vijana na watu wazima katika hija ya Lourdes ya Jimbo Kuu Roma
Ratiba ya pamoja
Ni Ratiba iliyojaa mambo ya pamoja kwa wote: Kuanzia njia ya Msalaba hadi Katekesi, Misa ya kimataifa hadi kutembelea maeneo aliyoishi Mtakatifu Bernadetta, kusali Rozari Takatifu ambayo itatangazwa na kuoneshwa mbashara tarehe 30 Agosti 2025 kwenye chaneneli ya TV2000, kuzunguka na mienge wakati wa kusali Rozari hadi kufanya siku kuu tarehe 31 Agosti 2025, itakayohuishwa na vijana wenyewe.
Lourdes, Tumaini kwa Vijana
Kwa mujibu wa Padre Alfredo Tedesco, Mkurugenzi wa Ofisi ya Jimbo Kuu kwa ajili ya Huduma ya Vijana alisema: “Uwepo wa vijana unathaminiwa ndani ya hija ya kijimbo. Tayari tumejaribu kuwashirikisha katika siku za nyuma, lakini wakati huu tutafanya hivyo kwa kina na nguvu zaidi. Kuna uhusiano mkubwa, kati ya vijana na suala la afya ya kimwili, ya kiakili na ya kiroho. Mateso ni sehemu ya maisha yao: kuna ugumu, upweke, na shida ya elimu. Lourdes inaweza kuwa mahali pa mfano, kwa mama Yetu, ufunguo wa uponyaji, na uwepo, unaweza kuwakilisha ishara yenye nguvu kwao.” Na kwa kuhitimisha taarifa yake kutoka Vicarieti ya Roma Padre Tedesco alisema “ Hija hii pia ni jibu madhubuti kwa kizazi kinachohitaji kuhisi kusikilizwa, kuungwa mkono, kuponywa, na kupendwa."