杏MAP导航

Tafuta

2025.08.29 Mkutano wa Urafiki Kimataifa 2025 kwa vijana wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio. 2025.08.29 Mkutano wa Urafiki Kimataifa 2025 kwa vijana wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio. 

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio:Toleo la Urafiki wa Kimataifa wa Vijana wa Amani 2025

Mkutano ulionza tarehe 28 hadi 30 Agosti 2025 jijini Roma,ukiwaona zaidi ya vijana 1,200 kutoka Ulaya yote na maeneo yenye migogoro mikali zaidi kwa kushirikishana nyakati za kukutana,mijadala na tafakari iliyolenga upatanisho na matumaini.Agosti 29 jioni tamasha la flashmob huko Pantheon lilifanyika na Jumamosi,30 Agosti:Hija ya kupita Mlango Mtakatifu Petro:Waandaji:"Tunataka kuishi siku hizi tukiwa na uhakika kwamba kwa pamoja tunaweza kubadili Ulimwengu."

Vatican News.

Zaidi ya vijana wa kiume na wa kike 1,200 wenye umri wa kati ya miaka 15 na 25 kutoka  Ulaya, na vile vile kutoka sehemu zenye maumivu na migogoro kama vile Ukraine, Nchi Takatifu, na Syria, ni Vijana wa Amani wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ambao walikusanyika katika kituo cha mikutano cha La Nuvola huko Roma kuanzia Agosti 28 hadi 30 kwa toleo 2025 la ("Global Friendship" for Peace-Hope), yaani Urafiki wao Amani wa Kimataifa mwaka huu.

Nyakati za Nguvu

Alifungua kwa hotuba yake Bwana Marco Impagliazzo, rais wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, tukio hilo lililojumuisha mikutano, mijadala, na ziara za kiutamaduni za jiji la milele ,pamoja na umati wa tamasha la amani lililofanyika Ijumaa tarehe 29 Agosti  katika mazingira ya kupendeza ya Pantheon. "Uamuzi wa kufanya tukio hili katika jiji la Roma," kwa mujibu wa  Stefano Orlando, mkuu wa Vijana kwa ajili ya Amani wa Jumuyia ya Mtakatifu Egidio, alieleza kwa vyombo vya habari vya Vatican, "pia unahusishwa na ukweli kwamba mji mkuu ni mwenyeji wa Jubilei ya Matumaini. Jumamosi asubuhi, ni kushiriki pamoja katika hija na kupita kwenye Mlango Mtakatifu wa Mtakatifu Petro, na jioni katika Adhimisho la Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro."

Uharaka wa Mazungumzo

Mkutano huu una lengo kuu la kuitaka dunia nzima kukomesha migogoro yote, hata ile iliyosahaulika. Na hakuna anayeelewa zaidi ya vijana hawa jinsi hatua ya haraka ya upatanisho kati ya watu wote ilivyo haraka. “Mara nyingi sana, wengi wao, ambao ni sehemu ya makundi ya kitaifa, ni wavulana na wasichana ambao Jumuiya ya Mtakatifu Egidio iliwakaribisha kama wahamiaji, kwa mfano, kutoka maeneo yenye matatizo kama vile Syria na Iraqi. Na sasa, wao ndio wanaowakaribisha wengine, wanaofanya kazi kwa ajili ya maskini, wazee, na walio hatarini zaidi."

Mkutano wa vijana wa Mtakatifu Egidio 28-30 Agosti
30 Agosti 2025, 10:17