杏MAP导航

Tafuta

Kardinali Zuppi, aongoza Ibada ya Misa katika Basilika ya Mtakatifu Clara wa Assisi tarehe 11 Agosti 2025. Kardinali Zuppi, aongoza Ibada ya Misa katika Basilika ya Mtakatifu Clara wa Assisi tarehe 11 Agosti 2025.   (ANSA)

Italia/Assisi:Kard.Zuppi,tufuate mfano wa Mtakatifu Clara:bila silaha tunaweza kupokonya uovu!

Katika Sherehe ya Mtakatifu Clara wa Assisi,tarehe 11 Agosti 2025,Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Italia,Kardinali Matteo Zuppi na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Bologna nchini Italia aliongoza Misa katika Basilika ya Mtakatifu Clara.Katika mahubiri yake alisema:“nilazima tujitoe kujenga si kuzimu lakini mbingu za kweli,zilizopatanishwa na dada aliyepatanishwa na maisha yetu.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali Matteo Maria Zuppi, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI),Jumatatu tarehe 11 Agosti 2025 aliongoza ibada ya Misa Takatifu katika maadhimisho ya Sherehe ya Mtakatifu Clara wa Assisi   katika Basilika ya  Mtakatifu Clara huko Assisi. Katika mahubiri yake alikazia juu ya kuiga mfano wa Mtakatifu Clara, ambaye alikabiliana na uovu bila silaha na kupokonywa silaha. Hii ni kukumbuka tukio la Jiji kuzingirwa, na Wasaraceni ambapo a wananchi walikimbilia nyuma ya kuta, huku watawa wa Mtakatifu  Damiano, wakiongozwa na Mtakatifu Clara, walisali kwa ajili ya wokovu.

Mtakatifu Clara kufukuza jeshi 

Kipindi hiki kinajulikana kwa kuingilia kati kwa Mtakatifu Clara ambaye, kulingana na utamaduni, aliwafukuza Wasaracens. Hii ni kwa sababu katika historia ya enzi za kati nchini Italia  mara mbili huko Assisi ilitishiwa na jeshi la Mtawala Frederick II ambaye aliyekuwa anahesabiwa kuwa katili kati ya askari wake, pia Wasaracens. Mtakatifu Clara akiwa, mgonjwa wakati huo, walipavamia Monasteri yao, alipeleka kwenye kuta za jiji akiwa ameshikilia (monstrance iliyokuwa na Sakramenti Takatifu mkononi mwake. Waandishi wa wasifu wake wanasema kwamba jeshi, wakati huo, lilikimbia. Kwa hiyo tangu wakati huo, tukio hilo hukumbukwa na kuadhimishwa huko Assisi katika siku kuu kubwa ya  Waklara Maskini, kila ifikapo tarehe 22 Juni ya kila mwaka.

Kwa njia hiyo  katika Sherehe hiyo ilihudhuriwa na mamlaka ya juu ya kiraia na kijeshi na kwaya ya Assisi ilitumbuiza. Kardinali Zuppi, akifafanua juu ya kielelezo cha Mtakatifu Clara alisema kinaweza kuwasaidia Wakristo, lakini pia Kanisa na ulimwengu:  “Antafoni ya sherehe ya leo, yenye mashairi makuu, inasema: ‘Leo nyota imezuka; leo Mtakatifu Clara, maskini mdogo wa Kristo, ameruka kwa utukufu wa mbinguni.” Na kwa  hiyo na tuinua macho yetu ili kuelewa jambo fulani kuhusu sisi wenyewe na dunia, na tuongozwe na upendo mmoja wa Mungu. Hebu tutoke nje tuone nyota tena, kama Dante alivyosema, ili tusibaki tumefunikwa na giza la kutisha na jeuri ambalo hatuwezi kulizoea, la kutisha; na jehanamu ya mateso tunayoona karibu nasi, sio tu wale walio mbali."

Kardinali Zuppi alikumbuka: "Wakati mwanadamu anajifanya kuwa Mungu na kujiamini kuwa mwenye uwezo wote na kuwa tamaa, ambayo ni kikomo chake na njia ya kuishinda, anaishia kujenga kuzimu za kweli duniani. Na bado, kama Papa Francisko alivyosema, "mwanadamu hana uwezo wote; hawezi kufanya hivyo peke yake. Na ikiwa anamtenga Mungu, anaishia kuabudu vitu vya kidunia. Lakini sio sababu za ulimwengu." Na kwa sababu hiyo katika siku kuu hiyo, Kardinali Zuppi, alisisitiza kuwa tunapaswa kuongozwa na Clara mzuri na thabiti  na kama masisita  binti zake, ambao kwa nuru ya uwepo wao ni mwanga wa ubinadamu, wa kukaribisha na wa sala.”

Tupendane kama alivyoagiza Yesu

Kardinali Zuppi anaamini kwamba wao bado wanatetea jiji na “ni lazima tujitoe kujenga si kuzimu, lakini mbingu za kweli, zilizopatanishwa na dada aliyepatanishwa na maisha yetu. Furaha ya kuangaza ya Mtakatifu Clara," ilikuwa ni kifungu kingine kutoka kwa mahubiri ya Rais wa CEI,  kwamba ikuwa tabia daima ya dada zake. Mtakatifu Clara alikuwa bibi arusi ambaye lakini mwenyewe akiwa katika ushirika na jumuiya. Na ni kiasi gani tunahitaji jumuiya, ambayo si kujifikiria yenyewe bali pamoja, na mahusiano ambayo si ya ushirika tu,  bali ya upendo, mahali ambapo tunaweza kuishi amri ya "Tupendane " ambalo ni chaguo la Yesu aliloliacha.” Maisha ya ndani kwa mujibu wa Kardinali  Zuppi:  "kwa hakika si kutengwa au umbali kutoka katika maisha halisi, bali ni nafasi ya kupata ushirika kikamilifu na Mungu, bila kuingiliwa. Jibu la dhiki tunayopitia sisi sote sio kujifanya kuwa haipo, ustawi usiowezekana, au mbingu ambazo zinakuwa magereza; jibu la dhiki ni kubaki pamoja na Yesu, tumaini letu, likiimarishwa na upendo wake na sababu inayotufanya tusivunjike moyo."  Kardinali  Zuppi alisema: “Mtakatifu Clara, masisita wapendwa, tusaidieni kwa hali ya kiroho ambayo hatuwezi kuishi bila hiyo."

'kuitwa Dada kulika mama mkuu'

Mtakatifu Clara anatukumbusha kwamba upendo unamaanisha huruma. Mtakatifu Clara hatafuti suluhuisho za ushirika, bali  zile za kifamilia tu, zisizo na jukumu lolote la kimabavu au la kusumbua, lakini za kila wakati kwa uangalifu na unyenyekevu: na kiukweli, Clara  alipendelea kuitwa dada, iliyoonekana kuwaa muhimu zaidi kwake kuliko jina la mama.

Jubilei ya matumaini 2025

Katika Jubilei hii ya Matumaini, (mwaka Mtakatifu 2025), Mtakatifu Klara anatusaidiea kuchagua njia ya amani. Anatukumbusha kwamba maombi yana nguvu zaidi kuliko vita, na hii inatutia moyo kuthubutu kumfuata Bwana, ambaye anakabili uovu. Katika hali ya vurugu, tuige mfano wa Clara, ambaye anakabiliana na maovu bila silaha na kuwapokonya silaha, kama vile pia Papa Leo XIV alivyotuomba. Mtakatifu Clara, asiye na silaha na kupokonya silaha, anakabiliana na uovu ambao hapo awali ulichochea woga: tufuate mfano wake," Kardinali Zuppi alihimiza kwamba "tunapokuwa hatuna silaha, tunaweza kupokonya uovu."

Siku kuu ya Mtakatifu Rufino,Msimamizi wa Mji wa Assisi

Baada ya Sherehe ya Mtakatifu Clara wa Assisi, Jimbo zima liliingia katika sherehe hai kwa kwa ajili ya Msimamizi wa mji, Mtakatifu Rufino. Kwa njia hiyo tarehe 12 Agosti 2025, Jijini Assisi na Jimbo kwa ujumla linaadhimisha Msimamizi wake Mtakatifu Rufino katika Kanisa Kuu ambapo Misa Takatifu ilioongozwa na Askofu wake Domenico Sorrentino, saa 5.00,  kamili asubuhi masaa ya Ulaya, na misa nyingine inatarajiwa kufanyika saa 12.00 Jioni na wakati huo saa 3,00 usiku majiara ya Ulaya katika Kanisa kuu, lifanyika tamasha kwa heshima ya Msimamizi wa Mtakatifu kwa kuongozwa na Kikundi cha Muziki cha Mtakatifu Rufino.

Kardinali Zuppi(CEI)- Assisi
12 Agosti 2025, 11:51