杏MAP导航

Tafuta

Balozi wa Vatican nchini Ghana,Askofu Mkuu Julien Kabore Balozi wa Vatican nchini Ghana,Askofu Mkuu Julien Kabore  (Vatican Media)

Ghana,Ask.Mkuu Kabore:Juhudi za Kanisa Katoliki kutoa usaidizi kwa watu waliopoteza makazi

Kufuatia na kuzuka kwa mzozo katika eneo la kaskazini-mashariki mwa Ghana,Waziri wa Ukanda wa Juu Mashariki mwa nchi hiyo aliwataka viongozi wa eneo wa Kanisa Katoliki kutumia ushawishi wao kufikia amani.Hata hivyo alishukuru Kanisa kuwasidia wakimbizi na juhudi zake endelevu za kujenga katika eneo hilo.Alisema hayo wakati wa kutembelewa na Balozi wa Vatican Nchini humo Ask.kuu Kabore wakati wa kutelembelea wakimbizi kwa mujibu wa ripoti ya FIDES.

Na Angella Rwezaula  - Vatican

Mzozo wa muda mrefu ulitawala eneo la kaskazini mashariki mwa Ghana kufuatia mauaji ya vijana watatu na watu wenye silaha huko Bawku, (Upper East Ghana). Mamlaka zilijibu kwa kutekeleza amri ya kutotoka nje na kuweka maafisa wa usalama katika eneo hilo. Vifo hivi vilianzisha mzozo miongo kadhaa juu ya jukumu la viongozi wa makabila ya Mamprusi na Kusasi katika kanda. Kihistoria, Wamamprusi walidai mamlaka ya jadi juu ya eneo la Bawku, wakati Wakusasi walitetea haki zao kama watu wengi. Kutokana na vurugu hizo zinazoendelea, Kanisa Katoliki katika eneo hilo limekuwa likifanya kazi ya kutoa misaada kwa watu waliopoteza makazi yao na kutetea amani katika eneo hiloKwa mujibu wa  shirika la Vatica la  habari za Kimisionari Fides,

Waziri wa Eneo la Juu Mashariki mwa Ghana alisifu kazi hii

Waziri Donatus Akamugri Atanga, wa Kanda ya Juu Mashariki, alisifu kazi hiyo, na alifanya hivyo wakati wa ziara yake ya  heshima iliyofanywa na Askofu Mkuu Julien Kabore, Balozi  wa Vatican nchini Ghana. Balozi wa Vatican  nchini Ghana, Askofu Mkuu Julien Kabore, alifanya ziara katika eneo hilo la kaskazini-mashariki mwa Ghana lililoharibiwa na migogoro. Eneo hili pia ni nyumbani kwa mamia ya watu waliokimbia makazi yao kutoka Burkina Faso ambao wamekimbia ghasia kutoka kwa makundi ya Kiislamu-ambayo, kama Shirika la habari za kimisionari Fides lilivyoripoti, sasa inatishia kuenea katika eneo hili la Ghana. Akihimiza Kanisa la eneo litumie uvutano wake ili kusukuma umoja, Waziri huyo alisisitiza kwamba “pande zote mbili zinazohusika katika mzozo huo zina mwelekeo zaidi wa kusikiliza sauti ya viongozi wa kidini kuliko ile ya wanasiasa.” Mgogoro huu ulianza nyakati za kabla ya ukoloni na kuwa mbaya zaidi baada ya Ghana kupata uhuru mwaka 1957 huku serikali moja baada ya nyingine ikitumia ushawishi wa machifu kujiendeleza kisiasa.

Balozi wa Vatican nchini Ghana

Askofu Mkuu Kabore alitoa shukrani zake kwa serikali ya Ghana na watu wa Kanda ya Juu Mashariki kwa kuendelea ukarimu na usaidizi kwa wale wanaokimbia hali mbaya ya Burkina Faso. Katikati ya ghasia zinazoendelea, alipongeza usaidizi usioyumba wa nchi kwa ajili ya kuwakaribisha na kuwahifadhi wakimbizi walio katika dhiki. Hofu iliyopo sasa ni kwamba makundi ya wanajihadi katika nchi jirani ya Burkina Faso yanaweza kutumia mvutano kati ya makundi hayo mawili kupata nafasi nchini Ghana, kupanua eneo lao la ushawishi na kuhatarisha biashara ya mipakani kati ya Ghana, Burkina Faso na Togo. Mzozo huo pia ni mgumu kusuluhishwa kwa sababu makabila yote mawili yanashutumu vikosi vya usalama kwa upendeleo. Wamamprusi wanadai jeshi linapendelea maslahi ya Kusasi, huku wa pili wakiishutumu serikali kwa kushindwa kutekeleza sheria za kimila zinazolenga kuzuia ghasia.

06 Agosti 2025, 09:26