杏MAP导航

Tafuta

2025.07.30 Maandamamo makubwa Jijini Luanda nchini Angola dhidi ya kupanda kwa bei za Petroli na bidhaa nyingine. 2025.07.30 Maandamamo makubwa Jijini Luanda nchini Angola dhidi ya kupanda kwa bei za Petroli na bidhaa nyingine.  

Angola:Watu 22 wamekufa katika uasi dhidi ya gharama kubwa za maisha.Maaskofu watoa wito

Baraza la Maaskofu nchini Angola na S?o Tomé (CEAST) linatoa wito wa kuwa na utulivu na mazungumzo,huku machafuko yakiendelea kupamba moto katika mitaa ya Jiji la Luanda,mji Mkuu wa nchi hiyo.Maelfu ya waandamanaji wamekamatwa kwa tuhuma za uporaji.Maandamano hayo yalichochewa na kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Maandamano makali nchini Angola yote dhidi ya kupanda kwa bei ya mafuta yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 20 na kusababisha kukamatwa kwa zaidi ya 1,200, huku ghasia ikiendelea bila kusita tangu Jumatatu iliyopita katika baadhi ya maeneo ya mji mkuu, Luanda.

Machafuko nchini Angola
Machafuko nchini Angola   (ANSA)

Bei za mafuta kupanda

Vurugu hizo, zilizo na sifa ya uporaji, uharibifu, na mapigano na polisi, zilifuatia uamuzi wa serikali mapema mwezi huu wa kupandisha bei ya dizeli kwa theluthi moja ili kupunguza shinikizo la fedha za umma kutoka kwa ruzuku ya gharama kubwa ya mafuta. Vyama vya mabasi madogo, ambavyo pia vimeongeza nauli kwa hadi asilimia 50, vimeitisha mgomo wa siku tatu kupinga uamuzi huo. Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika inayozalisha mafuta imepunguza hatua kwa hatua ruzuku ya mafuta tangu 2023, wakati maandamano dhidi ya kupanda kwa bei ya petroli yalisababisha vifo.

Wito wa Kanisa

Askofu Mkuu wa Saurimo na Rais wa Baraza la Maaskofu la Angola na São Tomé (CEAST), Mhashamu José Manuel Imbamba, alisema licha ya viwango vya umaskini na umaskini vilivyorekodiwa nchini humo, aina hii ya uharibifu na machafuko yanayohatarisha ustawi wa kijamii wa familia na mali za umma na binafsi, haiwezi kuvumiliwa kwa namna yoyote ile. Kwa hivyo, Baraza la Maaskofu SAngola (Ceast) inataka mazungumzo ya haraka ili kurejesha hali ya kawaida. “Nawaomba vijana wetu wawe na tabia ya ustaarabu na kuanza upya mazungumzo kati ya wananchi na taasisi zetu,” alisisitiza kiongozi huyo.

Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini Angola
Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini Angola

Mfumuko wa bei

Katika nchi hiyo inayozungumza lugha ya Kireno yenye wakazi wapatao milioni thelathini, mfumuko wa bei ni mkubwa sana, ambao unakaribia 20% kwa mwezi Juni, wakati kiwango cha ukosefu wa ajira kimefikia karibu asilimia 30%. Ghasia zilizozuka mjini Luanda siku ya Jumatatu tarehe 28 Julai 2025  zimeenea nchini kote. Chama cha madereva wa TAX (Anata) kilijitenga na ghasia hizo lakini kilithibitisha mgomo huo utaendelea kwa muda usiojulikana. Katika maandamano ya Jumatatu iliyopita huko Luanda, mji mkuu wa nchi hiyo, takriban watu 2,000 waliitikia wito wa mashirika ya kiraia kupinga ongezeko la bei ya mafuta na athari zake katika ununuzi wa umeme. Nyingi za kauli mbiu za waandamanaji, hata hivyo, zilikuwa dhidi ya "ufisadi" wa MPLA, chama tawala. Hasira za waandamanaji hazikumuacha hata Rais João Lourenço, aliyechaguliwa tena kwa muhula wa pili wa miaka mitano mnamo 2022.

Maaskofu Angola watoa wito wa Utulivu katika ghasia
31 Julai 2025, 16:25